Katika pita pita ya Leo kitaa nimelifumania jengo hili ambalo ndani ndio kuna studio bora ya mwaka ambayo ilijinyakulia tuzo ya Zanzibar Music Awards 2011. kilichinijia akilini ni kwamba ubora wa kazi si uzuri wa jengo naamini hata yule ambae amewahi kurekodi kazi yake analitambua hilo. Anaeonekana kwa mbali kama anaingia ndani hivi ni mmoja wa wasanii maarufu sana Znz Rico Single nae aliotewa pande hizo.
Studio ya 6 Rec ipo maeneo ya mwera lazima uvuke mto ukiwa umekunja suruali ama ubebwe kama we sharobaro upo? Nje ya studio hii kunalimwa mihogo,matembele,maboga na upupu pia nahisi utakuwepo.