Monday, June 3, 2013

DOGO FETY AKIWA NA KINYAMBI NA CHAMOYO

Msanii chipukizi Fatuma Abdalah Jengo aka Fety akiwa katika pozi na mastar anaowakubali kutoka Vituko Show Kinyambi na Chamoyo.
Fety ni msanii chipukizi aliopo katika kundi la King Majuto lenye maskani yake mjini Tanga.
Kwa sasa Fety ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya Seminary Hanga mkoani Ruvuma, yupo katika maandalizi ya mtihani wa kuingia darasa la tano.
Fety mpaka sasa hajawahi kushiriki katika movi yoyote kutokana na hali ya masomo kumuweka bize.

Kwa mujibu wa mipangilio yake kwa sasa hayupo tayari kucheza filamu yoyote kwa kuhofia kujisahau katika masomo "Ni kweli sipo tayari kushiriki filamu kutokana na hali ya masomo kuwa taiti, naelewa kuwa hakuna filamu ya kuchezwa siku moja kwa hiyo zile siku ambazo nitakaa kambi kwa ajili ya kushuti zitaniathiri sn kasomo".

Kitu ambacho anakitarajia ni kutumia muda wake wa likizo kuweza kushiriki filamu ambayo itakuwa inafanyila kwa kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments