Friday, April 27, 2012

MNAUTAKA AU HAMUUTAKI MUUNGANO?

Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara unaofanywa na kundi la Muamsho wakiwa wamenyoosha mikono kwa ishara ya kuukataa muungano baada ya kuulizwa swali "MNAUTAKA" wote kwa pamoja walijibu hawautaki.

Wednesday, April 11, 2012

REST IN PEACE STEVEN KANUMBA

Baadhi ya watu waliohudhuria mazishi
Makamu wa Rais, Gharib Bilal kushoto na Waziri wa Habari na Utamaduni Emmanuel Nchimbi wakiwa msibani.
LEO KITAA inatoa pole kwa Familia ya Steven Kanumba, ndugu, jamaa, marafiki na Taifa kwa ujumla kwa msiba mzito tulioupata kwani tunaamini kwamba sote tupo katika njia moja Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi.

Monday, April 2, 2012

MTI JUU YA NYUMBA

Katika pitapita zangu nilishtushwa na huu mti ulioota juu ya nyumba hii ambayo inaishi watu kama kawa, wakazi wa nyumba hii wanaonekana kutokuwa na wasiwasi wowote juu ya mti huo ulioota juu ya nyumba yao. Baada ya kumhoji mmoja wa wakazi wa nyumba hiyo alisema kwamba wao hawana hofu yoyote kuhusu mti huo kutokana na kuamini uimara wa nyumba yao.