Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) imesonga mbele katika michezo ya raundi ya kwanza kwa kanda ya Afrika ya mchujo wa kombe la dunia litakalofanyia huko nchini Urusi mwaka 2018.
Taifa stars wakicheza ugenini huko nchini Malawi walikubali kulala kwa kichapo cha bao1-0 dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya Malawi The Flames.
Bao lao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakia ya 41 na mchezaji Dave Banda.
Licha ya kuchapwa kwa bao hilo Tanzania wamesonga mbele kwa hatua ya pili baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Stars watacheza Raundi ya Pili na timu ya taifa ya Algeria, ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko Algiers hapo Novemba 17.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja