Wednesday, January 12, 2011

MAGOMENI AKA MIGO MIGO YA ZENJI

HAPA PANAITWA MAGOMENI SOKO LA SAMAKI
Tindi ndi ndi ndiiiiiii.......Picha linaanza
Hili ndio soko la samaki la magomeni
Kina mama wakiweka vizuri mizigo yao ya kuni za magamba ya mnazi tayari kwa kujitwika
Haya ni mambo ya kawaida uswazi
Kitu chauliza
Wakati mwingine unawza kusema kwa mtanzania kuishi maisha haya ni kawaida lakini kwa upande mwingine Serikali haina buni kuwageukia watu kama hawa na kuwapatia msaada

Is this life????

Bado niliendelea kushangazwa na hii staili ya nyumba za mitaani. Nyumba zote madirisha yake yamezibwa nusu nikaendelea kuchochora.

Uchochoro......
Uzalendo ulinishinda nikaweka kambi kwa wadau ambao ndio wenyeji wangu wa mtaa huo na kuanza kuwadodosa sababu za nyumba zao kuziba nusu madirisha.... mwenzangu sababu kubwa niliyopewa eti 'CHABO' tena sio za watoto za watu wazimaaa..


Umeona mambo hayo!!!

Kisa nini CHABO

Haya nayo ndio hivyo tena ukianza kujenga uswazi usiombe uishie njiani.. kitachokutokea ndio kama hivi.



Mara nyingi huwa tunaona shoti za umeme zinatokea bila ya kujua sababu, kumbe hawa ndege wanojenga kwehye nyaya za umeme huennda ikawa sababu ya shoti hizo haya wahusika kazi kwenu huku mitaani mambo ndio kama hivi nguzo za umeme zimekuwa nyumba za ndege.

Saturday, January 8, 2011

LEO KITAA ILPOIBUKA MAENEO YA DUNGA

Hapa ni eneo la kituo cha polisi Dunga kibao kidogo kinaeleza gari zote za abiria lazima zisimame eneo hilo kwa ajili ya kukaguliwa. Kitu kilichonivutia kupiga picha hii ni hiyo yebo yebo inayoonekana kwa juu ya kibao mwenzanguuu wee,,,,,, Kilometa 19 na tisa tu kutoka dunga kituo cha polisi kuelekea Kinyasin na kilimeta 14kuelekea Chwaka kama kibao kinavyoonyesha upooo..
Hivi Madaraja ya kupita gari moja na jinine lisubiri yataisha lini?????
Hili ni moja ya daraja la kupita gari moja mwingine subiri kwanza ambalo utapambana nalo ukiwa unaelekea Dunga.

Wednesday, January 5, 2011

MINI ZIFF 31 DEC 2010 NDANI YA NGOME KONGWE

Hiki ni kibao ambacho kina jina la sehemu hii na ni moja ya kivutio chenye historia yake



Nilibaini kwamba hizi picha ni za vijana toka THT ambao watatoa burudani siku ya tarehe 31 dec katika tamasha dogo la filamu la nchi za majahazi nazunguzia Mini ZIFF