Tanga ni miongoni mwa miji iliyopewa hadhi ya Jiji nchini Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tabora.
Mji wa Tanga ni mji mkuu wa Mkoa wa Tanga
uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi. Tanga
ina bandari kubwa kabisa katika sehumu ya
kaskazini mwa Tanzania . Njia ya reli kwenda
Mji wa Moshi inaanza hapa.
Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la
Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni:
Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara
upande wa mto na Shamba juu ya mlima, neno
hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei
ambalo ni wenyeji wa mkoa huo linamaana ya
shamba, wao hulitamka N'tanga.
Vilevile Tanga ni mji ambao unapata maendeleo kila kunapokucha wawekezaji wa ndani wanajitihada kubwa ya kuwekeza majengo ya kisasa na kuonyesha mabadiliko ya mji huo.
kwenye orodha yako ya majiji toa tabora
ReplyDeletehuyo aliyekuambia Tabora jiji ni nani?
ReplyDelete