Sunday, February 16, 2014

WASANII BONGO Kusambaza filamu ya Why Linah? Jumatatu hii.


Rose Ndauka

Hemed


KAMPUNI mpya ya usambazaji wa filamu Bongo ya Yuneda Entertainment imeingia katika biashara ya usambazaji baada ya kilio cha wasanii kukosa sehemu za kuuza filamu zao au kusambaziwa, kampuni hiyo inayojali ubora kwa kazi za sinema imeingia nchini kuanza kwa kusambaza filamu ya Why Linah? Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo kama Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka, Charles Magali ‘Mzee Magali’, pamoja na wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahilihood, filamu hiyo inaingia leo jumatatu.
Wasanii wamefurahia sana ujio wa kampuni hiyo kwani wanaamini kuwa wengi wataweza kusambaziwa kazi zao kwani moja ya sifa hiyo ni ya kizalendo inayojali maslahi ya wasanii, na inaongozwa na wazalendo wanaojua hali halisi ya soko la filamu nchi Tanzania.
Hivyo kwa kuzingatia umakini na ubora wa filamu Yuneda Entertainment wanakuletea filamu yenye viwango vya kimataifa ya Why Linah?.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments