Sunday, October 19, 2014
TMT MOVIE KULETA MAPINDUZI MAKUBWA BONGO
ILE Filamu kubwa kabisa kutengenezwa katika viunga vya Tanzania ya Tmt movie imeanza maandalizi yake kwa kurekodi filamu mpya huku wasanii waliopatikana kutokana na shindano la Tanzania Movie Talent kuibeba sinema hiyo wakiwashirikisha wasanii wengine waliochaguliwa katika sinema hiyo. Akiongea na FC mratibu wa filamu hiyo Staford Kihore amesema kuwa moja ya malengo makubwa ya Proin Promotion ni kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa, katika kuwasimamia wameanza nao kurekodi sinema TMT Movie. “Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford. Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahilihood. Filamu kubwa ya Tmt Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo. Sterring wa sinema hiyo ni milionia wa kutoka Mtwara Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Bongo wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima. &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&& LETA FILAMU YAKO DAR FILAMU FESTIVAL 2014 SASA KAMPUNI ya Haak Neel Production na Filamucentral waandaaji wa Tamasha la Dar Filamu Festival wanawakaribisha watengenezaji wote wa filamu zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutuma au kuwakilisha filamu zao katika ofisi za Haak Neel Production zilizopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere. TAMASHA kubwa kabisa la filamu Swahilihood hilo linapokea kazi zilizotoka mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha kubwa linalounganisha wadau na watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwengu na kutoa fursa kwa wadau wengi kutengeneza soko lingine. Akiongea na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula amesema kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani litafika kila kona ya Wilaya za Dar es Salaam na kutoa burudani ya kazi nzuri zinazotengenezwa na watanzania. “Kama ilivyo kauli mbiu yetu inasema “FILAMU ZETU, MAISHA YETU” ni kauli mbiu ya kutia matumaini kwa watengenezaji na watazamaji kwani filamu tuaamini kuwa ni kazi inayoweza kutengeneza ajira kubwa kwa kila mtu,”anasema Katula. Tamasha hili ambalo limelenga kukuza Lugha ya Kiswahili na kufanya kuwa ni biashara na alama kubwa kwa filamu zetu zinateka soko Afrika ya Mashariki kwa kuongea Kiswahili kitamu na kinzuri kinachovutia kwa wanaAfrika mashariki na Ulaya. Mtengenezaji wa filamu au mtayarishaji unatakiwa kuwakilisha filamu nakala mbili za filamu ambayo imetoka mwaka na kuonyeshwa kwa mwaka 2014, ikiwa samba na utambuzi wa mtayarishaji, imekaguliwa na Bodi ya Filamu pamoja na taratibu husika katika taasisi za filamu. Kwa mawasiliano na jinsi ya kuwakilisha filamu zenu wasiliana na +2552773113, +255754 578 730, +255754 260 688 Ongea na Dada Unce anakupatia maelekezo ya kufika katika ofisi za Haak Nell Production.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments