Kibao kinacho onya utupaji wa taka eneo hili.
Wakati mvua zikiendelea kuonyesha mjini Zanzibar huku magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu ikiwemo kipindu pindu yanaendelea kujitokeza.
Baadhi wa wakazi wa Mombasa Unguja wanakabiliwa na wakati mgumu pindi inaponyesha mvua kutokana na maeneo ambayo wanaishi kuwa ni sehemu ya kutupa taka.
Wananchi hao wamesema pamoja na manispaa kudhiti watu wasitupe taka eneo hili kwa kuweka vibao vinavyokataza lakini wamekuwa wakiendelea kutupa taka nyakati tofauti hasa usiku.
Hivyo wameomba Serikali ifanye jitihada ya kuziondosha taka hizo na kusafisha eneo hilo.