Thursday, January 16, 2014
Mwanadada Lady Yoo ft Sanawari 'Poa'
Mwanadada Lady Yoo akiwakilisha Sanawari anakuja na new idea kwa jina "Poa" ikiwa ni hatua za awali katika kukamilisha mixtape yake inayoitwa "Nyumbani Africa" itakayodrop kabla ya pasaka, 2014, ngoma ni mkono toka Atown Records chini ya producer WaBak, bofya HAPA kuisikiliza/download.
Brand new track ya reggae toka kwa Ras Bao ft Yahsimbi "African"
Mwanamuziki wa Reggae Ras Bao pamoja na mwanadada Yahsimbi toka Sweden wakishirikiana katika ngoma yao waloipa jina "AFRICAN" ,ngoma imerekodiwa Noizmekah Studios chini ya Deftxtro, bofya HAPA kudownload.
Richie 101 aanza mwaka 2014 na "Kaa Pembeni"
Nyota njema huonekana mapema kwa kuthibitisha hilo Richie101 ameachia ngoma yake mpya "KAA PEMBENI" ambayo amemshirikisha mkali Moplus pamoja na Kiranja.
Producer Moscow toka new way music, ndio amemfungulia Richie mwaka 2014
Vocals na mixing ya wimbo huo vimefanyika Noizmekah Studios, click HAPA kuisikiliza na download.
Saturday, January 11, 2014
A +254 Rap | Dancehall | Zouk fusion Artist Mista Vina aachia nyimbo mbili kwa mpigo
A +254 Rap | Dancehall | Zouk fusion Artist Mista Vina ameachia nyimbo mbili kwa pamoja,
"Usicheze Nami" na "Good Music"
Mbali na kuachia nyimbo hizo Vina anatambulisha nyimbo zake zaidi ya tano kupitia link hapa chini
"As an artist i have several music sounds in different sites and i will be more than glad if you consider any of my work" Hayo ameyasema Vina wakati anatambulisha nyimbo zake katika mitandao.
Soundcloud
[Reverbnation -www.reverbnation.com/mistavina]
Mdundo -
[Mtv.com - www.mtv.com/artists/mista-vina]
[Hulkshare - www.hulkshare.com/mistavina]
[Youtube - www.youtube.com/user/Mistavina]
Myspace -
Twitter -
Facebook Fanpage -
[Yourlisten.com -www.yourlisten.com/MistaVina]
[NumberOneMusic -www.numberonemusic.com/mistavina]
TNG waachia wimbo mpya Ng'ae Ng'ae
Ng'ae Ng'ae ngoma mpya ya TNG -Chiwaman, La Tino iliyosimamiwa na producer Man Water Combination Sound imedondoka kitaani.
Wimbo huo wenye style tatu ndani Regge/blue/hip hop ni ubunifu mkubwa na wakipekee uliofanywa na wasanii hao katika kuhakikisha wanakupa ladha ya muziki wa Tanzania.
Saturday, January 4, 2014
North Dwellers wamerudi upya katika game
Baada ya ukimya wa muda sasa kundi la North Dwellers toka pande za Arusha warudi tena,hapa wakiwa wamemshirikisha Dee Cee.."Huu ni utangulizi tu,tumeshafanya mizigo mingi,kwa sasa hivi mambo yanakwenda,producer wetu John B yupo nyumbani so tumefanya na tutafanya vingi,tayari ngoma inayofuata ishakamilika,itakua out soon,tupo tunachapa kwanza kideo na Nezar wa Digital Media Studios,zaidi na zaidi,kuwa original" anasema Slim Deezy wa North Dwellers.
Pia akaongeza kwa kusema "Kumbuka kesho huanza leo na usiishi kwa matukio" NorthDwellerz ft Dee Cee "Original" Official Music Video
Audio Download kwenda kwenye simu yako: Credits Song: Original Artists; North Dwellers ft Dee Cee A Grandmaster Records Production Produced by Hadjihandro and John B.
Dayna afunga mwaka na "Mimi na wewe"
Mwisho wa mwaka kila mtu anafanya kitu cha kumuwekea kumbukumbu ama kumfurahisha kama ilivyozoeleka kwa wasanii wengi kutoa wimbo wa kufunga ama kufungulia mwaka mpya,
Mwadada Dayna nae hakuwa nyuma kutuacha "Mimi na wewe"
Katika kutupa ladha yake ya mwisho wa mwaka wimbo ambao offcourse umepokewa vizuri kwa asilimia kubwa sana.
Wimbo umerekodiwa katika studio za One Love FX chini ya producer TIDDY HOTTER > >
Shoti ya umeme yazua balaa mjini Pemba
Taarifa iloyonifikia muda mfupi uliopita kwa njia ya whatsapp.
Shoti ya umeme imeathiri nyumba takribani 100 katika mji wa Pemba kijiji cha Shumba mjini kwa moto mkubwa unaoendelea kuwaka.
Na mpaka hivi sasa haujawezekana kuzimwa kwa kutopatikana zima moto.
Subscribe to:
Posts (Atom)