Wednesday, July 16, 2014

African Reggae Ambassodor Jhikoman kutingisha jukwaa la 5th Internatinal African Festiva Tubingen 2014

wanamuziki maarufu wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania,anatarajiwa kupanda jukwaani katika maonyesho makubwa ya kimataifa ya 5th.International African festival Tubingen 2014,nchi ujerumani. Mwanamuziki huyo nguli wa reggae amepewa nafasi ya pekee ya kutumbuiza mara mbili kwa siku tofauti katika viwanja vya onyesho hilo Festplatz,Europa str. mjini Tubinge kusini mwa ujerumani, ambako maonyesho yatafunguliwa 17.julai 2014 hadi 20.Julai 2014,maonyesho ya Tubingen yategemewa kukusanya umati wa watu zaidi ya 100,000 na yanazishirikisha bendi na wasanii mbali mbali wa nchi za kiafrika.Pia Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbali mbali za kiafrika wameshaanzakuwasili katika mji huo wa Tubingen ,kuudhuria maonyesho hayo. http://www.jhikoman.com/ https://www.youtube.com/watch?v=aJJyZ3NTrts

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments