Aisha Bui akiwa na Gabo katika moja ya scene za filamu ya Mshale wa Kifo iliyorekodiwa Morogoro
Aisha Bui na Gabo wakipumzika baada ya kazi nzito kushuti Morogoro.
FILAMU YA MSHALE WA KIFO KUINGIA SOKONI AISHA Fathi ‘Aisha Bui’ anafunguka kwa kutamba kuwa filamu yake mpya inayoingia sokoni siku ya jumatatu, itadhihiri kipaji chake katika tasnia ya filamu, kwani amewakilisha wazo lake moja kwa moja bila kupigwa alichoandika ingekuwa ni kazi ya kushirikishwa isingekuwa rahisi. “Najua kila mtu anakuwa na uwezo wake katika filamu lakini unaweza kushindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa nafasi ndio maana mimi nimeamua kutumia kampuni yangu kutimiza ndoto zangu, wiki hii Yuneda Entertainment wanasambaza kazi yangu mtaani,”anasema Aisha Bui. Sinema hiyo ya Mshale wa Kifo inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya Yuneda Entertainment ya Jijini Dar es Salaam, ikiwa imetayarishwa na Aisha Bui chini ya kampuni yake ya Badgirl Entertainment filamu yake ya kwanza mwanadada huyu. Filamu ya Mshale wa Kifo inawakutanisha wasanii nyota wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kama vile Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Mzee Korongo, Salim Ahmed ‘Gabo’, Aisha Bui na wasanii wengeine wakali, Aisha anasema pia anazindua kampuni yake ya Badgirl Entertainment inayotoa filamu ya Mshale wa Kifo
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments