Wednesday, February 24, 2016
Wimbo wa Edu Boy "Dumange" toka Classic sound waingia kitaani kwa kasi.
Msanii wa bongo fleva Edu Boy ameachia wimbo mpya aliomshirikisha Mr T "Dumange" msanii huyo ambae alikuwa namba moja katika mashindano ya serengeti fiesta mwaka 2012 na kuachia hit song kadhaa kama "Pata pesa tujue tabia yako" ambayo amemshirikisha Belle 9.Edo ambae anaiwakilisha Rock City Mwanza ameachia wimbo huu tofauti na miondoko yake ya hip hop ambayo amezoeleka ambayo imetengenezwa na producer Mr T Free Nation studio.
Wednesday, February 17, 2016
Sijapenda mimba ya Wema iharibike...Nay wa mitego
Mwana hip hop Nay wa mitego amesema hakupenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike kama baadhi ya mashabiki wa Wema wanavyodai.
Wiki chache zilizopita mkali huyo wa hip hop aliachia wimbo wa "Shika adabu yako" ambao ndani yake amemchana Wema "una mimba kweli au ndio kiki za msimu, miezi tisa sio mingi isje ikakugharimu" kauli ambayo imetafsiriwa kwa namna mbalimbali.
Kupitia kipindi cha Ubaoni ..Efm jana Nay alisema hawezi kumuombea Wema mabaya kwa yeye anapenda sana watoto.
"Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda sana watoto nampa pole sana dada yangu kama ilikuwa mimba kweli kama ilikuwa kiki basi imefika mwisho nilichoimba kwenye wimbo wangu ilikuwa ni swali tu una mimba kweli au drama?" Nay aliongea.
Wiki chache zilizopita mkali huyo wa hip hop aliachia wimbo wa "Shika adabu yako" ambao ndani yake amemchana Wema "una mimba kweli au ndio kiki za msimu, miezi tisa sio mingi isje ikakugharimu" kauli ambayo imetafsiriwa kwa namna mbalimbali.
Kupitia kipindi cha Ubaoni ..Efm jana Nay alisema hawezi kumuombea Wema mabaya kwa yeye anapenda sana watoto.
"Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda sana watoto nampa pole sana dada yangu kama ilikuwa mimba kweli kama ilikuwa kiki basi imefika mwisho nilichoimba kwenye wimbo wangu ilikuwa ni swali tu una mimba kweli au drama?" Nay aliongea.
JamboSquad......DigiDigi kutoka Noiz
Bofya HAPA dowload https://mkito.com/song/digi- digi/18840 #DigiDigi by Manjeree Machalii ya Ara #JamBoSquad @chaliijambo @odiijambo Produced by @defxtro @noizmekah huku tukisubiri Official Video Directed by #EmpireStatemedia @Director_Nezar Wiki Ijayo kwa Mahojiano/mawasiliano zaidi check na @jambosquad kwa nambari au 0653 610 249 au 0762 164 241 Powered by @vmgafrica @defxtro @j4cinyo @djhaazu @fredy_temu follow #vmgafrica #SupportUrOwn #LoveAfricanMusic
Tuesday, February 16, 2016
Ben Paul na Jux wapeana makavu kwenye 'Nakuachana'
Dar es Salaam, Tanzania – February 15, 2016 Ujumbe wenye dalili za ukweli uliojificha ndani ya mzaha umezaa wimbo mkubwa kati ya wakali wawili wa RnB Tanzania, Benard “Ben Pol” Paul
na Juma “Jux” Khaleed.
‘NAKUCHANA’ ni wimbo mpya wa RnB ambao ndani yake Ben Pol na Jux wanasikika wakipeana ‘makavu’ kuhusu mambo kadhaa hasi kuhusu wao, huku kila mmoja akitafuta kile anachoamini ni kona dhaifu ya mwenzake.
“Nakuchana ilizaliwa baada ya mimi na Jux kwenda studio, na tulienda studio tulitaka kwenda kurekodi kabisa wimbo rasmi, lakini tukawa tunajivuta vuta, tukaona bana eh hebu lets just have fun umeona, sababu tulikaa muda mrefu kama masaa matatu hatujapata kitu. Kwahiyo tukasema ngoja tujifurahishe (kwa kuchanana) kama watu ambao wanakuwa wana have fun wanavyochill sehemu, unajua wanazinguana wanafanyaje. Kwahiyo kwenye ku-have fun ndio tukaandika mstari mmoja mmoja tunau record, tunaandika mmoja tunau record yaani tumeandika yote kwa pamoja. Kwahiyo hivyo ndivyo ambavyo ‘Nakuchana’ ilivyozaliwa.” Alieleza Ben Pol kuhusu wimbo huo.
Ben Pol ameongeza kuwa wamelazimika kuitoa ‘NAKUCHANA’ kipindi hiki kutokana na demo ya wimbo huo kuvuja siku chache baada ya kurekodiwa na kuonekana kupendwa na mashabiki wengi.
‘NAKUCHANA’ ni wimbo uliopikwa
na producer Bob Manecky wa studio ya A.M Records, na ndio collabo ya kwanza kwa Jux na Ben Pol kufanya.Sunday, February 7, 2016
Lyrics za wimbo wa Krikinchi krakancha wa Kck supremacy hizi hapa
KRIKINCHI KRAKANCHA LYRICS
Artist :kck supremacy
Track:fekeche fekeche
Studio:Noiz mekah prod.
VERSE 1 SPAC DAWG
Fekeche fekeche krikinchi krakancha,
Kwikwichi kwikwichi mchuchuu anakacha,
Krikinchi hii punch mbuchuchuu mbakacha,
Kifukuchu fukuchu krikinchi chuchu mkuchu jax,
Raff kibrooklyn krukuchuu crooklyn,
Fekeche fekeche prukuchuu church,
Bike yake cheche kudaka kicheche,
Krikinchi ndichi kufekeche feke,kwichi kwichi kwichi
Krokoncho chocho kupecha peke oga mavirokocho,
Kirikuu wa mapocho mletee ma dogydogy,
Hata kiforokocho kifo cha kokorochi,
Kumbonji ni kinky anataka double clickich
Krikinch krakancha
VERSE 2 BOOX
Fekeche fekeche krikinchi clutch
Click kichele besa trasa scratch
Mbele,switch krikinchi punch
Maushirodachi,sotohachijidachi
Nakaa shikodachi ni set lunch
Nikae musubidachi
Peleka wasanii kwa magetsadanii
Na Kwa getsadaichi
Ichi Née San Shi Go Rock Hach Sichi
Krikinchi pinchi ni tensi ya mjate
Krakancha Ten Atalokota ngada
Akose ya mkate fekeche fekeche
Shop akakate Anatwe ang'atwe
Afanywe kwikwichi kwikwichi
Krikinchi cheche
Chorus
Fekeche Fekeche krikinchi krakancha ,
Kwikwichi kwikwichi krikinchi krakancha,
Fekeche Fekeche krikinchi krakancha,
Kwikwichi kwikwichi krikinchi krakancha,
Fekeche fekeche krikinchi krakancha kwikwichi kwikwichi krikinch kra,
Fekeche fekeche krikinchi krakancha kwikwichi kwikwichi krikinchi kra,
Smaina Ft. Mariana - Landaa
Wimbo wa LANDAA wimbo uliobeba maneno ya kabila jamii ya Wasandawe na wimbo wa asili ambao umejumuisha mila, desturi, vyakula, vijiji na Koo za Kisandawe... Link to share: http://www.audiomack.com/song/
Saturday, February 6, 2016
BEN POL NA PETER MSECHU WATOA ZAWADI HII YA VALENTINE KWA MASHABIKI WAO - ‘NYOTA YA SAMBOIRA’
Dar es Salaam, Tanzania – February 3, 2016: Waimbaji mahiri wa muziki kutoka Tanzania, Ben Pol na Peter Msechu wameachia ‘mash-up collaboration’ ya hatari, ‘NYOTA YA SAMBOIRA’ kama zawadi ya msimu huu wa Valentine kwa mashabiki wao wa dhati.
‘NYOTA YA SAMBOIRA’ ni muungano wa nyimbo mbili, ‘NYOTA’ ya Peter Msechu pamoja na ‘SAMBOIRA’ ya Ben Pol zilizoweka historia kwa kila mmoja kwa kufanya vizuri kipindi zilipotoka.
Kuhusu mash-up hii Ben amesema, “Katika msimu huu wa Valentines, mimi na Msechu tumeona tuwaunganishe mashabiki wetu wawe kitu kimoja kama ishara ya upendo, kwa kuwaletea Nyota ya Samboira ambayo ni muunganiko wa kazi zetu mbili zilizofanya vizuri. Hivyo ni matumaini yetu kwamba wataendelea kusambaza upendo kwa wawapendao kupitia zawadi hii.
SABABU ZA KUREKODI MASH-UP HII:
Moja ya sababu zilizochangia wimbo huu (mash-up) urekodiwe, kwanza ni kutokana na Ben Pol na Peter Msechu kuwa marafiki na kila mmoja kuwa shabiki wa mwenzie. Ndio maana katika ‘NYOTA YA SAMBOIRA’, Ben ameimba verse ya Msechu na Msechu ameimba verse ya Ben za kwenye nyimbo zao halisi.
JINSI MASH-UP HII ILIVYOPATIKANA:
Mradi wa mash-up hii ulianza kama utani.
Ben na Peter walikutana kwenye studio ya Downvillah Records ambapo kila mmoja alienda kwa ratiba yake binafsi ya kurekodi nyimbo tofauti, lakini kama ujuavyo wasanii wanapokutana studio huwa panakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya kitu. Hivyo wakaamua kufanya kazi lakini kwa kurudia nyimbo zao kwa mtindo wa mash-up ambayo imesimamiwa na producer Teaz Villah.
KUHUSU NYIMBO HALISI ZA ‘NYOTA’ NA ‘SAMBOIRA’
‘Samboira’ ni moja ya hits za Ben Pol iliyotoka mwaka 2011 na inayopatikana kwenye album yake ya kwanza ‘MABOMA’.
‘NYOTA’ ni wimbo wa Peter Msechu uliofanya vizuri sana mwaka jana (2015) ambao uliachiwa mwaka 2014 mwishoni.
Samboira pia ni jina la msichana aliyeimbwa kwenye wimbo wa Ben, huku Nyota ni kama ilivyo maana halisi ya nyota ing’aayo angani.
Subscribe to:
Posts (Atom)