Mwana hip hop Nay wa mitego amesema hakupenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike kama baadhi ya mashabiki wa Wema wanavyodai.
Wiki chache zilizopita mkali huyo wa hip hop aliachia wimbo wa "Shika adabu yako" ambao ndani yake amemchana Wema "una mimba kweli au ndio kiki za msimu, miezi tisa sio mingi isje ikakugharimu" kauli ambayo imetafsiriwa kwa namna mbalimbali.
Kupitia kipindi cha Ubaoni ..Efm jana Nay alisema hawezi kumuombea Wema mabaya kwa yeye anapenda sana watoto.
"Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda sana watoto nampa pole sana dada yangu kama ilikuwa mimba kweli kama ilikuwa kiki basi imefika mwisho nilichoimba kwenye wimbo wangu ilikuwa ni swali tu una mimba kweli au drama?" Nay aliongea.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments