Friday, June 15, 2012

ISON AGONGA VIDEO YA HALOO BABA

Msanii maarufu mjini Zanzibar aliyekuwa akiigiza kwenye kundi la Black Roots almaaruf kama Mwinchande akicheza party ya Mr President kwenye video ya Haloo baba ya Ison, Mr President akiwa kwenye kikao muhimu na kamati yake pamoja na waandishi wa habari alijikuta akipokea simu kutoka kwa mtoto wake na kusahau kama yupo kwenye kikao muhimu alijikuta akinyanyuka kikaoni na kuondoka akaacha mshangao mkubwa kwa wanakikao pasipo kujua ni kitu gani kimemsibu mheshimiwa.
Producer wa T Top Chief Elia akiwa amecheza kama mwandishi wa habari akiwemo Dj Dr B wa Coconut Fm, Hussein Hamis wa Coconut Fm, Donisia Thomas wa Bomba Fm wote wakiwa kama waandishi wa habari hapa wakiwa wamepigwa na butwaa kuona Mr President anaongea na simu na kusahau kama yupo kikaoni.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments