Thursday, December 10, 2015

Ngoma Mpya | Nipende Kama Nilivyo - Ram Life ft Makamua & B the Boss Man

Msanii  wa hip hop "Ramlife" ameachia ngoma mpya maskioni mwa watu ambayo ameitambulishwa rasmi kupitia www.eriqure.com , Wimbo unaitwa NIPENDE KAMA NILIVYO ulioandaliwa na Producer KAJU BEATS, Amemshirikisha "Makamua na B The Boss Man"
Download & Share Link > http://bit.ly/1Nacj50

Best Nasso kuja na mkwaju mpya


Baada ya Kusemekana Best Nasso amekamatwa nchini Congo na madawa ya kulevya hatimae ameweka wazi wa mashabiki wake kua tuhuma hizo si za kweli na kutambulisha  wimbo wake mpya.

Wimbo huo ameupa jina la "RUMBA" na ameshafanya video yake amesema kuwa wimbo huo utaanza kupatikana kwenye mtandao wa Mkito.com kuanzia jumamosi tarehe 12 mwezi wa 12 ambayo ni siku yake ya Kuzaliwa.

EWI (Environmental Warriors Of Ilboru) yaachia ngoma "Kumbusho kwa Rais"

EWI (Environmental Warriors Of Ilboru)  yaachia ngoma mpya "KUMBUSHO KWA RAIS" HipHop yenye sauti ya mkali Bounak, Spac Dawg, Boox, Chindo pamoja na Gnako mkono toka kwa defxtro noizmekah Studios.

Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli atangaza baraza la mawaziri wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza. 

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. 

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

WIZARA
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina

Ajira, walemavu: Jenista Joakim Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Abdallah Possi. M ambae ni mhadhiri Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.
Endelea hapa http://www.jamiiforums.com

Tuesday, December 8, 2015

Manispaa ya mji Unguja yaombwa kuondosha majaa yaliopo maeneo ya makazi ya watu.

Kibao kinacho onya utupaji wa taka eneo hili.


Wakati mvua zikiendelea kuonyesha mjini Zanzibar huku magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu ikiwemo kipindu pindu yanaendelea kujitokeza.
Baadhi wa wakazi wa Mombasa Unguja wanakabiliwa na wakati mgumu pindi inaponyesha mvua kutokana na maeneo ambayo wanaishi kuwa ni sehemu ya kutupa taka.
Wananchi hao wamesema pamoja na manispaa kudhiti watu wasitupe taka eneo hili kwa kuweka vibao vinavyokataza lakini wamekuwa wakiendelea kutupa taka nyakati tofauti hasa usiku.
Hivyo wameomba Serikali ifanye jitihada ya kuziondosha taka hizo na kusafisha eneo hilo.

Friday, November 27, 2015

Wednesday, November 25, 2015

Amini aachia ngoma mpya

Amini msanii ambaye anafanya vizuri katika anga ya muziki wa kizazi kipya ambaye pia anaongoza katika wasanii wanaofanya vizuri anaposhirikishwa na msanii mwingine ameachia ngoma yake mpya inayoitwa 'FURAHA'

Wimbo huo ambao umetayarishwa katika ubora wa hali ya juu umefanyika chini ya mtayarishaji C9 ameuachia rasmi katika raduio pamoja na mitandao ya kijamii.

Monday, November 23, 2015

UTAMBULISHO WA MSANII FEMI ONE KUTOKA KENYA NA NYIMBO YA "WANJIKU KIMANI"

Msanii kutoka nchini Kenya chini ya uongozi wa Kaka Empire, anyeimba katika miondoko ya rap maarufu kama 'Femione' (pichani juu) anakuja na kibao chake kipya kinachojulikana kama 'Wanjiku Kimani' ambacho amekitambulisha hivi karibuni huko nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kibao hicho cha wanjiku kimani kinafanya vizuri sana pande za Nairobi na Kwenye mitandao kiujumla kwa kusikilizwa watu wengi sana.

HISTORIA FUPI YA MSANII FEMI ONE:

Femione alizaliwa Wanjiku Kimani huko nchini Kenya. Ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya kati ya watoto watatu. Yupo katika tasnia ya muziki kwa kipindi kirefu na hakuchagua rap bali rap ndio iliyomchagua.

SAFARI YAKE YA KIMUZIKI;

Femione alianza kurap akiwa na umri wa miaka 15. Alianza kufahamika alipojiunga na kundi lijulikanalo kama Young Star ikiwa na maana ya "Nyota Wadogo", waliofundishwa namna ya kurap na kundi maarufu la marappa wa Kikenya liitwalo Wenyeji. Baada ya mafunzo hayo walihitimu na kufanikiwa kuunda kundi la watu watatu wote wakiwa wasichana. Kundi hilo liliundwa na Samantha, Mary and Femione kuanza kurap. Watatu hao walibahatika kutumbuiza katika matamasha kadhaa kama "WAPI" lakini watu walionyesha kuto tosheka nao baada ya show hiyo kuisha.
Wakati wa utumbuizaji wa tamasha la "WAPI" waandaaji wa tamasha hilo kutoka Afrika ya Kusini waliwaomba kuwa nao pamoja tena ili kwenda kutumbuiza katika tamasha kubwa huko Afrika Kusini lijulikanalo kama Fire on the Mountain kwa kipindi kile. Baada ya show hiyo ya Afrika Kusini Femione aliona kuwa anafursa nyingi kwa muziki anaoufanya.
Mara tu baada ya shoo nchini Afrika Kusini kundi la watatu hao lilivunjika kutokana kurudi tena masomoni. Mary alijotoa lakini Femione na Samantha walibaki pamoja mpaka ilipofikia wakati Samantha kuamua kufanya shughuli nyingine na kuachana na muziki.
Ijapokua Femione aliendelea kutumbuiza katika tamasha la WAPI ambapo King Kaka alipomuona, King Kaka alimuomba Femione kumshirikisha katika remix ya nyimbo yake ya "Ligi Soo" na baadae kufanikiwa kuwa remix nzuri kuliko zote nchini Kenya. Kipaji chake hapo ndio kikawa mwanzo wa kuzaa matunda na kufanikiwa kuingia mkataba na Lebo ya Kaka Empire na hata kuendelea kuwa maarufu zaidi.

NYIMBO ALIZOTAMBULISHA;

-Wanjiku Kimani - Femione (Nyimbo mpya ameitambulisha Septemba)
-Good times - Femione and Samantha,
-Maumbile - Femione ft Ms Kerry,
-Ligi Soo remix akishirikiana na wasanii wengine,
-Karata - Femione ft. DJ Jr Kaka Empire.

VIDEO RELEASED; https://www.youtube.com/watch?v=Zq6ZCBdblUg
MAWASILIANO:

-Email: angiroakumu@gmail.com,
-Facebook: Shikow Femione,
-Twitter: femi_one,
-INSTAGRAM: femi_one,
-Web: www.kakaempire.com

Sunday, November 15, 2015

Euro Man ft Ruff G-True Love (NOIZ)

Bofya HAPA https://mkito.com/song/true-love-ft-ruff-g/17306 kupakua wimbo wa Euroman ft Ruff G Katika ngoma kwa Jina "True Love" ikiwa ni Reggae Category toka @noizmekah kwa @defxtro.

Ruff G - Tucheze Wote (NOIZ)

@jambosquad Presents #RuffG: Bofya HAPA https://mkito.com/song/tucheze-wote/17298 kupakua wimbo wa @ruffgmusic kwa jina #TuchezeWote Produced by @defxtro @noizmekah

NEW SONG FROM PETER MSECHU "MALAVA"



PETER MSECHU

Peter Msechu was born in 1988 in Kigoma region, in the northern part of Tanzania close to the border with Burundi. He started singing aged ten when his father took him to join Kigoma Lutheran Church Choir, where at the time his father was the choir teacher.
Peter’s mother meanwhile was a teacher at Katubuka Primary School. She wanted her son to study hard while his father wanted him to be a musician.
In 2009 Peter Msechu’s talents came under the national spotlight in Bongo Star Search (BSS), a weekly TV talent competition. He faced many challenges as his experience was limited to choir singing whilst fellow contestants were singing a range of popular music styles.
After delivering his own first composition, feedback from the judges (Madam Rita, Salama Jabir, P Funk and Master J) helped Msechu to find a new confidence.  He changed tactics, started reinterpreting old hits with energetic performances. He quickly developed a wide fan base of young Tanzanians, eagerly tuning in to BSS every week to see what Msechu would deliver next.
Finally Msechu came in at number two. His dream had been to front a band, and said to himself “now is the time”. Within months he had released two major hits, “Hasira Hasara” and “Relax” (collaborating with Kenya-based Burundian musician Kidumu).
After becoming popular all over Tanzania by 2010, he joined Tusker Project Fame; similar to Bongo Star Search but this time including contestants from all over East Africa. Peter Msechu soon accumulated more fans throughout East Africa.
A year after Msechu joined Tusker Allstars competion where by those winners who won on the previous tusker project fame seasons where grouped together and compete again in celebrating five years of tusker project fame.. in this competition  Msechu became a winner among three winner who crowned on grand finale.
For these competition, Msechu chose classics by legendary African musicians including Oliver Mtukudzi, the late Marijani Rajab and Mbaraka Mwinshehe, and mixed these with new beats. Ultimately he came in again at number two, with an even greater confidence and resolve to pursue his career in music.
During the past year Msechu has performed all over East Africa and more recently in USA.

D-Hood-Moyo (NOIZ)

Bofya HAPA https://mkito.com/song/moyo/17165 kupakua wimbo wa D-Hood kwa jina "MOYO" ikiwa ni BongoFleva Category.

NEW AUDIO NILLAH - YUMBA YUMBA


OFFICIAL RELEASE(NEW SONG) - CHRIS BEE ft PETRONIA - BASHEE

Anaitwa CHRIS BEE hitmaker WalaWala kutoka Nchini Tanzania, ameachia wimbo wake wa Tano unaoitwa BASHEE aliomshirikisha PETRONIA.

Chris ameshatoa ngoma kadhaa kama WalaWala, Coconut, Urudi na Walawala remix, ambazo zimemtambulisha vema katika soko la muziki hapa nchini.
download ngoma hiyo kupitia https://www.hulkshare.com/12n1xx3ttq9i

Wednesday, November 11, 2015

Brand new song Jan B - My Life

Kupata ngoma hii Downolad hapa 

Tuesday, November 10, 2015

BASHEE FROM CHRIS BEE feat PETRONIA

CHRIS BEE hitmaker WalaWala from Tanzania, the guy that gave us hits like Coconut and Urudi is back again with another monster street hop hit, this one he titles ”Bashee” featuring labelmate PETRONIA

Brand new song Malaika "ZOGO"

"I hope uko Ok, mi naitwa Malaika ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania baada ya kimya cha muda mrefu leo nimezima ukimya huo kwa kuachia wimbo mpya unaitwa "Zogo" umetengenezwa katika Studio za Chaiderz Records chini ya mtayarishaji Abby Daddy, nimeachia pamoja na video iliyofanyika chini ya Director Hanscana"
Ni maneno yake Malaika fanya hima uskie wimbo huo kwani hakika amedhihirisha kuwa anavunja ukimya.

Sunday, November 8, 2015

Today Is My Day by Bac-t ft Pacson

Bac-t akiwa ame mshirikisha Pacson atambulisha nyimbo mpya iliyopo katika miondoko ya hip hop ambayo ime tengenezwa nchini Rwanda Kigali katika studio za Eagle Eyes Records na Producer B-Buster a.k.a DJB. Utamu zaidi wa wimbo huo lugha tatu zimehusika Kiswahili,Kingereza na Kinyarwanda na inagusa maadili ya watu wa Afrika MAshariki.

Monday, October 12, 2015

Taifa Stars yasonga mbele

Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) imesonga mbele katika michezo ya raundi ya kwanza kwa kanda ya Afrika ya mchujo wa kombe la dunia litakalofanyia huko nchini Urusi mwaka 2018.
Taifa stars wakicheza ugenini huko nchini Malawi walikubali kulala kwa kichapo cha bao1-0 dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya Malawi The Flames.
Bao lao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakia ya 41 na mchezaji Dave Banda.
Licha ya kuchapwa kwa bao hilo Tanzania wamesonga mbele kwa hatua ya pili baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Stars watacheza Raundi ya Pili na timu ya taifa ya Algeria, ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko Algiers hapo Novemba 17.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja

Dismond Platnumz, Vanesa Mdee, Ommy Dimpos wajinyakulia tuzo za Afrima

Diamond Platnumz akishow love na moja ya tuzo alizoshinda pamoja na mchekeshaji kutoka Nigeria Basketmouth.
"I do know what to say"
Picha hii Platnumz ameipost mtandao wa Twitter akionyesha hajui aseme nini kwa furaha alio nayo kwa kushinda tuzo hizo tatu.
Vanessa Mdee akiwa na tuzo.

Wanaboa - Samata



Msanii wa kizazi kipya Samata ambae pia ni mhandisi,mbali na kazi yake ya uhandisi anapenda sana muziki hali inayompelekea kutenga muda wake vizuri kwa ajili ya muziki.
"Wanaboa" ni wimbo wake ambao amehusisha hali ya maisha halisi ya  kila siku hasa uswahilini ambapo kuna tabia tofautitofauti za watu na tabia nyingi ni za ajabuajabu.

Bofya hapa upate kuicheki nyimbo hii WANABOA YOUTUBE LINK

Bonie-Norini + Ngina

 Bofya hapa kudownload https://mkito.com/song/ngina-ft-mamsi/16675 kupakua "NGINA" wa Bonie na HAPAhttps://mkito.com/song/norini/16676 kupakua "NORINI" kwa mahojiano/mawasilano zaidi check na Bonie kwa nambari +255 754 422 764 powered by @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com  @defxtro #vmgafrica #SupportYourOwn
--

Thursday, October 8, 2015

NEW HIT TRACK: KINGKAPITA FT. CANNIBAL - VIZABIZABINA


Baada ya kimya cha muda mrefu msanii King Kapita ambaye kwa mara ya mwisho ulimsikia katika wimbo wake wa "Kuna tatizo kwani?" ambao amemshirikisha Godizilla, amerudi nchini kutoka Africa ya Kusini ambako alikuwapo kimasomo.

Msanii huyo anaefanya muziki ni ujasilia mali amerudi kwa kasi mpya na kufanya ngoma ya VIZABIZABINA aliyomshirikisha Cannibal Shatta kutoka nchini Kenya iliyotengezwa na John B pamoja na Kanyeria. 
Baadhi ya nyimbo ambazo jamaa amewahi kufanya pia ni Shikamoo pesa, Mtoto mlito na Here we go alipokuwa ndani ya kundi la Wakacha kabla ya kuwa msanii wa kujitegemea.


Monday, October 5, 2015

Jojo aanza kueleweka na "Nakuhitaji"


Mwanadada Jojo ameanza kusomeka kitaani na ngoma yake Nakuhitaji ambayo siku chache zilizopita imeingia kitaa na kuanza kuchezwa na vituo mbalimbali vya radio

UTAMBULISHO WA NYIMBO YA 'SITAKI SHARI', RIZ CONC FEAT. SIR ZULU


Riz Conc anatambulisha nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la 'SITAKI SHARI', ambayo amemshirikisha rappa Sir Zulu. Itasikika katika Radio mbali mbali za Bongo na nje ya nchi kuanzia tarehe 05/10/2015. Nyimbo ya 'Sitaki Shari' imefanywa na producer ALONAME na kusimamiwa na Sudy Baya_KingMaarifa chini ya uongozi wa Pesasina Co. LTD.

Wednesday, September 30, 2015

Nu Single SMILE FT. BOB JUNIOR-Naona Raha

Muradaiz yaachia ngoma mpya toka Mazuu Rec

Kundi jipya la music wa kizazi kipya toka kisiwani Zanzibar Muradaiz limeachia nyimbo yao ya pili ikiwa imefanyika studio ya mazuu records chini ya usimamizi wa producer Mazuu & Boy David, ngoma iko vizuri sn na tayari imeanza kusikika katika vituo mbalimbali vya Radio hapa nchini kwa sapoti zaidi ya muziki wa nyumbani usikose kuusaka wimbo huo.

Sunday, April 26, 2015

Lady Jaydee ft. Mazet & Uhuru - GIVE ME LOVE

This is a brand new single from Lady Jaydee called "Give Me Love" featuring South Africa's Mazet and the Infamous Uhuru. Give me love, which is a follow up to her riddim driven smash hit 'Forever", is produced by Dj Maphorisa Uhuru. Be on the Look out for the Video which is slated to drop at the end of the month.

Thursday, April 23, 2015

Bongoflava Anthem 2015

Ni kipindi kirefu toka ngoma moja ikatuunganisha watanzania wote kwa pamoja, mwaka jana kulikuwa na Mwana ya Ali Kiba, Mwaka wa nyuma yake Number One ya Diamond na Mwaka huu hii ngoma kutoka kwa msanii KICHE LEGEND anayekuja kwa kasi juu. wimbo unaitwa Angalia Juu, ni wimbo wa celebration, ni hustlers anthem, ni wimbo mzuri kwa ujumla

SHIRIKA LA HOTELI YA WYNDHAM LAFUNGUA HOTELI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI

Ramada Resort yafunguliwa Dar es Salaam, Tanzania- Hoteli ya kwanza Afrika kuendeshwa na shirika la hoteli la Wyndham kwa mkataka ya usimamizi.
Shirika la Hoteli la Wyndham, ambalo linaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya hoteli na moja kati ya vitengo vitatu vya kibiashara vya Kampuni ya Wyndham Worldwide (http://www.wyndhamworldwide.com), leo limetangaza kufunguliwa kwa Ramada Resort yenye vyumba 139 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/whg.jpg Photo: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1898 (Ramada Resort Dar es Salaam) Ufunguzi huu unaongezea kwenye hoteli nyingine nchini Morocco, Ghana, Nigeria na Tunisia, na kuendeleza upanuzi wa hoteli ya Wyndham katika kanda ya Afrika Mashariki. Pia hii ni hoteli ya kwanza AfriKa kuendeshwa kupitia kitengo cha usimamizi cha kampuni kinachoendelea kukua. “Ufunguzi wa Ramada Resort jijini Dar es Salaam una umuhimu mkubwa kimkakati kwetu” alisema Bw. Dan Ruff, ambaye ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli ya Wyndham katika eneo la Ulaya, Mashariki ya Kati, AfriKa na Bahari ya Hindi. Aliendelea kusema, “Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya malazi yenye ubora wa kimataifa katika Afrika Mashariki, pamoja na dhamira yetu ya kuwa karibu na wageni na wateja wetu kupitia upanuzi katika kitengo cha usimamizi wa mali, hii ni hatua muhimu sana katika ukuaji wetu katika kanda hii. " Pia Ruff alisema, “Ramada Resort ya Jijini Dar es Salaam, yenye vifaa vya kipekee na iliyoo kwenye eneo lenye mandhari mazuri ya ufukweni, imeweka viwango vipya kwa mahoteli yenye kiwango cha kati nchini Tanzania na tuna hamu ya kuwakaribisha wageni wetu wa kwanza kwa ukarimu wa kipekee wa Ramada” Kati ya jumla ya vyumba 139, vyumba 117 ni vyenye ubora mkubwa na viko mkabala na ufukwe au na bustani, vyumba 21 ni vya kiwango cha hadhi ya juu na chumba kimoja cha hadhi ya ‘presidential suite’. Vyumba vyote vina TV aina ya flatscreen na channel za satellite na mtandao wa Wi-Fi unapatikana bila malipo. Kadhalika, kuna baa ndogo, vifaa vya kukuwezesha kujitengenezea chai au kahawa na bafu binafsi vyumbani. Sanaa za michoro ya Tinga-tinga inaongezea mandhari ya Afrika mashariki. Vifaa vya burudani ni pamoja na bwawa la kuogelea, gym yenye vifaa vya kisasa na njia ya moja kwa moja inayoelekea ufukweni wa mchanga tifutifu. Kwa wateja wenye mikutano au matukio, tuna vyumba saba vya mikutano vinavyoweza kukaliwa na hadi watu 375 na maeneo matano ya vyakula na vinywaji yanayoandaa vyakula aina mbalimbali vya kiafrika na kimataifa vile vile. Tangu ujenzi ulipoanza 2009, tumezingatia mipango endelevu ikiwemo kutibu na kutumia upya asilimia 100 ya maji taka. Tumesistiza kutumia maji yaliyotumika kwa asilimia 100, matumizi ya nishati ya jua, kutumia mwanga wa taa za LED na ulinzi wa ufukwe ili usimommonyoke. Pia Hoteli inapanga jinsi ya kutumia mabaki ya chakula kama virutubisho kwa ajili ya kukuza mbogakwa ajili ya matumizi ya Hoteli, bustani hiyo iko katika Ghorofa ya juu kabisa ya Hoteli. Bw. Murtaza Fazal, mmiliki wa Ramada Dar Es Salaam, alisema “Ninafurahi kusaini mkataba wa muda mrefu na Wyndham Hotel Group, kampuni yenye Hoteli Kubwa duniani. Pia najivunia kuwa mwekezaji wa kwanza kuitambulisha Ramada katika soko la Afrika Mashariki. Ninaamini kuwa hii Ramada mpya iliyoko katika ufukwe wa Jangwani itakuwa ni kimbilio la wenyeji na hata watalii wa kimataifa na wageni wa kibiashara, tunajivunia mazingira bora, ubunifu na huduma bora. “Najivunia pia kuwa mwanzilishi wa matumizi ya nishati mbadala ili kulinda mazingira, ni matumaini yangu kuwa wamiliki wengine wa Hoteli watakuwa waiga mfano” Aliongeza Fazal,. Wageni watakaokaa katika hoteli ya Ramada Resort Dar es Salaam ambao ni wanachama wa Wyndham Rewards®, mpango wa kujiunga bure wa kuzawadia uaminifu wa wageni wa Ramada, wataweza kupata alama za thamani wakati wa ukaaji wao. Zawadi hizo ni kama vile malazi na chakula bila malipo, tiketi ya ndege bila malipo, kadi ya kufanya manunuzi na mengine mengi. Maelezo yanapatikana katika tovuti yetu, www.wyndhamrewards.com. Distributed by APO (African Press Organization) on behalf Wyndham Hotel Group. MAWASILIANO:Pegi AmarteifioPublicasityWyndham@publicasity.co.uk+44 20 3757 6800 Roz Money Wyndham Hotel Group The Triangle, 5 Hammersmith GroveLondon, W6 0LGUnited Kingdom +44 20 8762 6600roz.money@wyn.comWAHARIRI: Picha ziada na nembo zetu zinaweza kupatikana kutoka www.wyndhamhotelgroup/media . Kwa taarifa zaidi kuhusu Wyndham Worldwide Corporation na biashara zake, tembelea www.wyndhamworldwide.com . Kuhusu RamadaRamada Worldwide® ni sehemu ya kampuni ya hoteli za Wyndham na ina zaidi ya hoteli 830 duniani zenye ubora wa kati na wa juu. Hoteli hizi zinatoa huduma, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa intaneti ya kasi ya Wi-Fi, migahawa, vyumba vya mapumziko, huduma za chumbani , huduma ya bawabu, huduma za mikutano na vyakula, vifaa na vituo vya biashara . Ramada pia inatoa fursa kwa wasafiri kupata na kukomboa pointi kwa njia ya Wyndham Rewards®, programu ya uaminifu wa wageni, ambayo wanaweza kujiunga bila malipo katika www.wyndhamrewards.com . Ramada aliadhimisha miaka 60 ya kuwepo kwake mwaka 2014. Kila hoteli ya Ramada inajitegemea kwa umiliki na uendeshwaji, isipokuwa kwa baadhi ya hoteli za Ramada zilizopo nje ya Marekani ambazo zinasimamiwa na wabia. Ramada Worldwide ni kampuni tanzu ya Wyndham Hotel Group na kampuni mzazi ya Wyndham Worldwide Corporation ( NYSE: Wyn ). Taarifa zaidi zinapatikana kwa kutembelea tovuti yetu www.ramada.com . Kuhusu Kampuni ya Hoteli za WyndhamKundi la Hoteli la Wyndham, ambalo linaongoza duniani kwa umiliki wa idadi ya hoteli na moja kati ya vitengo vitatu vya kibiashara vya Wyndham Worldwide (NYSE: WYN). Kampuni ya hoteli inayoongoza duniani ya Wyndham inamiliki takriban majengo 7,650 na vyumba 661,000 katika nchi 70 chini ya majina yafwatayo; Dolce Hotels and Resorts® (ilimilikiwa February 2015), Wyndham Grand® Hotels and Resorts, Wyndham Hotels and Resorts®, Wyndham Garden® Hotels, TRYP by Wyndham®, Wingate by Wyndham®, Hawthorn Suites by Wyndham®, Microtel Inn & Suites by Wyndham®, Ramada®, Ramada Encore®, Baymont Inn & Suites®, Days Inn®, Super 8®, Howard Johnson®, Travelodge® and Knights Inn®. Wyndham Rewards, programu ya uaminifu wa wageni imetoa nafasi kwa wateja zaidi ya milioni 38 kupata na kukomboa pointi katika maelfu ya hoteli duniani kote. Kwa taarifa zaidi temebelea tovuti yetu www.wyndhamworldwide.com. Safe Sender Instructions UNSUBSCRIBE

Wednesday, April 1, 2015

Shetta Ft Kcee - Shikorobo | Audio | Video

Hone Classic-We Mama (Official Video)


Follow @honeclassic Na utazame Official Video ya wimbo "We Mama" HAPA https://youtu.be/W3MbciIfKuk directed by @travellah toka Kwetu Studios, Co-starring @momoh_fyne_chic & @Jaqlynelameck alongside @fidovato pakua Audio HAPA https://mkito.com/song/we-mama/13233 by @defxtro @noizmekah na kwa mawasilano/mahojiano na HONE CLASSIC piga +255 767 861 349 powered by @mkitodotcom @vmgafrica www.vmgafrica.com #vmgafrica #SupportYourOwn

NEW MUSIC: Dom Down Click [DDC] Song: KIMENUKA [Audio]

NEW AUDIO: NICKRAY FT. KOKU - NIWEJE

Sunday, March 22, 2015

SITTI MTEMVU MGENI RASMI MAHAFALI YA UMOJA WA SHULE ZA SEC MOROGORO


Sitti A. Mtemvu mgeni rasmi katika mahafali ya umoja wa shule za sekondari Morogoro
Mh. Mariam Mtemvu akiongea na wanafunzi

Mariam Mtemvu akiwa na Sitti A Mtemvu wakifuatilia mahafali kwa makini ukumbini

Mgeni Rasmi akimkabidhiwa Risala kutoka kwa wanafunzi

Baadhi ya wanafunzi wahitimu wakimsikiliza mgeni Rasmi Sitti Mtemvu hayupo pichani.

Sitti A. Mtemvu akiwa katika Mahafali ya Shule za Sekondari Morogoro katika ukumbi wa Moro Sec. Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation 2015 Sitti A. Mtemvu akiwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za Mkoa wa Morogoro wanaounda umoja wa Un Club Morogoro.

SITTI Abas Mtemvu mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation (STF 2015) amepokelewa kwa shangwe katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Morogoro alipoalikwa katika mahafali yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule hiyo baada ya kupokelewa na kundi la wanafunzi. Sitti alifika katika viwanja vya shule mapema akiambatana na mama yake mzazi Mariam Mtemvu, Kheri Mkamba katibu wa vijana mkoa wa Morogoro, wafanyakazi wa taasisi hiyo pamoja na wageni waalikwa . Akihutubia wanafunzi hao Sitti aliwaomba wanafunzi kutokata tama katika kujiendleza kimasomo kwani elimu ndio ufunguo wa maisha kwa kila mwanadamu, wawe na malengo ya kufika mbalia zaidi na isiwe kufika kidato cha sita ndio mwisho wa kusoma. “Dunia ya leo inahitaji sana Elimu hivyo si vema kwa mwanafunzi ambaye tunaye leo hapa kuona kuwa elimu ndio mwisho wake, no someni kwa bidii mfike vyuo vikuu na kupata shahada za juu,”anasema Sitti. Mwenyekiti huyo kupitia taasisi yake ametoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuchangia Un Club Tanzania Network Morogoro Cluster ambayo ndio kiungo kikubwa cha wanafunzi wa shule za Sekondari za Mkoa wa Morogoro. Maafali hayo yaliyoandaliwa na shule nne yalijumuisha pia shule nyingine tano wakiwaunga mkono wanafunzi wa kidato cha sita ambao ndio walikuwa wenye shughuli hiyo, shule zilizounga na kufanya sherehe pamoja ni Shule ya Sekondari ya Morogoro wenyeji. Shule nyingine ni Shule ya Sekondari Kilakala, Shule ya Sekondari Dakawa, na Shule ya Sekondari ya Mzumbe huku shule za Sua, Sekondari ya Mgulasi, Sekondari ya Sumaya, Sekondari ya Mafiga na Sekondari ya Uwanja wa Ndege zikishiriki katika tukio hilo la kihistoria. Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 2- May- 2015 katika ukumbi wa Mlimani City, ni siku ambayo mrembo huyo amehaidi kuandika historia kubwa katika maisha yake kwani itakuwa ni sehemu kubwa kutimiza ndoto zake. Sherehe hizo zilipambwa na show kutoka kwa wanafunzi wenyewe ambao walionyesha vipaji katika uchezaji wa muziki na kuimba.

ABD Mcee ft Spac Dawg-MC (NOIZ)