Sunday, March 22, 2015

SITTI MTEMVU MGENI RASMI MAHAFALI YA UMOJA WA SHULE ZA SEC MOROGORO


Sitti A. Mtemvu mgeni rasmi katika mahafali ya umoja wa shule za sekondari Morogoro
Mh. Mariam Mtemvu akiongea na wanafunzi

Mariam Mtemvu akiwa na Sitti A Mtemvu wakifuatilia mahafali kwa makini ukumbini

Mgeni Rasmi akimkabidhiwa Risala kutoka kwa wanafunzi

Baadhi ya wanafunzi wahitimu wakimsikiliza mgeni Rasmi Sitti Mtemvu hayupo pichani.

Sitti A. Mtemvu akiwa katika Mahafali ya Shule za Sekondari Morogoro katika ukumbi wa Moro Sec. Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation 2015 Sitti A. Mtemvu akiwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za Mkoa wa Morogoro wanaounda umoja wa Un Club Morogoro.

SITTI Abas Mtemvu mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation (STF 2015) amepokelewa kwa shangwe katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Morogoro alipoalikwa katika mahafali yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule hiyo baada ya kupokelewa na kundi la wanafunzi. Sitti alifika katika viwanja vya shule mapema akiambatana na mama yake mzazi Mariam Mtemvu, Kheri Mkamba katibu wa vijana mkoa wa Morogoro, wafanyakazi wa taasisi hiyo pamoja na wageni waalikwa . Akihutubia wanafunzi hao Sitti aliwaomba wanafunzi kutokata tama katika kujiendleza kimasomo kwani elimu ndio ufunguo wa maisha kwa kila mwanadamu, wawe na malengo ya kufika mbalia zaidi na isiwe kufika kidato cha sita ndio mwisho wa kusoma. “Dunia ya leo inahitaji sana Elimu hivyo si vema kwa mwanafunzi ambaye tunaye leo hapa kuona kuwa elimu ndio mwisho wake, no someni kwa bidii mfike vyuo vikuu na kupata shahada za juu,”anasema Sitti. Mwenyekiti huyo kupitia taasisi yake ametoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuchangia Un Club Tanzania Network Morogoro Cluster ambayo ndio kiungo kikubwa cha wanafunzi wa shule za Sekondari za Mkoa wa Morogoro. Maafali hayo yaliyoandaliwa na shule nne yalijumuisha pia shule nyingine tano wakiwaunga mkono wanafunzi wa kidato cha sita ambao ndio walikuwa wenye shughuli hiyo, shule zilizounga na kufanya sherehe pamoja ni Shule ya Sekondari ya Morogoro wenyeji. Shule nyingine ni Shule ya Sekondari Kilakala, Shule ya Sekondari Dakawa, na Shule ya Sekondari ya Mzumbe huku shule za Sua, Sekondari ya Mgulasi, Sekondari ya Sumaya, Sekondari ya Mafiga na Sekondari ya Uwanja wa Ndege zikishiriki katika tukio hilo la kihistoria. Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 2- May- 2015 katika ukumbi wa Mlimani City, ni siku ambayo mrembo huyo amehaidi kuandika historia kubwa katika maisha yake kwani itakuwa ni sehemu kubwa kutimiza ndoto zake. Sherehe hizo zilipambwa na show kutoka kwa wanafunzi wenyewe ambao walionyesha vipaji katika uchezaji wa muziki na kuimba.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments