Friday, August 31, 2012

KUNGURU WAMEKUWA KERO KITUO CHA MABASI TANGA

Kila ifikapo majia ya jioni imekuwa ni kawaida kwa kunguru hawa kukusanyika kwenye miti iliyopo kwenye kituo cha mabasi ikiwa kama hifadhi yao kwa ajili ya kulala.

Hali hii ni yamuda mrefu ambayo imekuwa ni kero kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaokuwepo eneo hilo kwa muda wa jioni.
Mara kwa mara kunguru hao wamekuwa wakiwanyea watu na kuwapigia kelele ikikapo mida ya jioni.

Mkurugenzi wa mji hili linakuhusu sana katika kutafuta namna ya kuweza kuhamisha makazi ya kunguru hao ili wananchi wako waweze kuwa na amani wakaapo katika eneo hilo.

MANG'ATI SIO KWA AJILI YA WAMASAI TU..


BIBI BOMBA NAMBA 3 AREJEA ZANZIBAR

Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe  leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.

Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)

Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.

Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.

Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.


Thursday, August 30, 2012

BALAAAAAA