Friday, August 31, 2012

BIBI BOMBA NAMBA 3 AREJEA ZANZIBAR

Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe  leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.

Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)

Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.

Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.

Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.


No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments