Tuesday, March 17, 2015

UJIO MPYA WA PAH ONE "KIZUBANETA"

LINEX FEATURING DIAMOND PLATNUMZ - SALIMA

HATIMAYE LINEX AACHIA WIMBO WAKE MPYA SALIMA AKIMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ

Linex akimshirikisha Diamond Platnumz katika wimbo wake mpya Salima ambao siku chache zilizopita ameuachia katika media mbalimbali. Video na audio ametoa kwa pamoja, Linex anaonekana kutulia sana katika wimbo huu, kama kawaida yake ametumia lugha 3 ndani ya wimbo, amepanga mashairi mazito yenye hisia na utunzi na ghani za mashairi yamepangiliwa katika ubora wa aina yake, lugha imetumika kiufasaha. Wimbo ni mzuri kwa ujumla ukiusikiliza hasa pale Diamond Platnumz alipofuata nyayo za uimbaji wa linex……….. ametumbukiza maneno ya kilugha kama afanyavyo Linex katika kila nyimbo zake anazoimba. Diamond ameutendea haki wimbo huu, wimbo unagusa nyoyo za watu…..wimbo unagusa hisia……na tena wimbo unaweza ukakutoa machozi..! welldone Linex….welldone Diamond….welldone team nzima na management inayomsimamia Linex kufanikisha kuutoa wimbo huu Video ya wimbo huu inavutia sana, pongezi kubwa sana kwa aliyeandaa siclipt ya video hii kwa kuweza kuindaa katika kiwango cha kutazamika kwa kila rika, video hii……natumaini inaweza kutumika na baraza la mitihani ya taifa ya kidato cha nne ama cha sita kuwatengenezea maswali kwa somo la Kiswahili….sitashangaa nikiona wimbo wa salima wa linex ikiwa mojawapo ya maswali ya mtihani wa ngazi ya taifa, its fantastic video! Miongoni mwa video zinazotarajia kufanya vizuri zaidi hasa nje ya nchi kwani ni video inayoonyesha uhalisia wa kitanzania kabisa hakika Linex pamoja na Diamond Platnumz wamefanya kazi kubwa na wavutia kwenye hii video, Pongezi za ziada ziende kwa AJ ( huyu ni Adam Juma) amefanya kazi ya ziada kwa kushuti kwa ustadi wa hali ya juu video hii…..kwakweli naweza kusema hii ndio video bora kwangu kwa mwaka huu 2015 ingawa mwaka haujaisha.

Sunday, March 15, 2015

SIKU YA YA MWISHO YA NOTISI KANISA LA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA KUHAMA KAWE

9 MACHI 2015 SIKU YA MWISHO YA NOTISI KANISA KANISA LISILO RASMI KUHAMA KAWE Siku 30 za notisi zimetimia Mchungaji Josephat Gwajima Kufunga virago Kawe!


Kanisa la lisilo rasmi la mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe,wilaya ya Kinondoni,jiji Dar limeamuriwa kuondoka mara moja na kuwacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa kawe. Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo. Katika Barua iliosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la nyumba la Taifa imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo limeshaanza kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k Bw Masika ametoa siku 30 tu ambazo leo 9 Machi 2015 Mchungaji Gwajima anatakiwa kufunga virago na kuwacha viwanja hivyo wazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Mchungaji Josephat Gwajima afunge virago

Friday, March 13, 2015