Tuesday, March 17, 2015

LINEX FEATURING DIAMOND PLATNUMZ - SALIMA

HATIMAYE LINEX AACHIA WIMBO WAKE MPYA SALIMA AKIMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ

Linex akimshirikisha Diamond Platnumz katika wimbo wake mpya Salima ambao siku chache zilizopita ameuachia katika media mbalimbali. Video na audio ametoa kwa pamoja, Linex anaonekana kutulia sana katika wimbo huu, kama kawaida yake ametumia lugha 3 ndani ya wimbo, amepanga mashairi mazito yenye hisia na utunzi na ghani za mashairi yamepangiliwa katika ubora wa aina yake, lugha imetumika kiufasaha. Wimbo ni mzuri kwa ujumla ukiusikiliza hasa pale Diamond Platnumz alipofuata nyayo za uimbaji wa linex……….. ametumbukiza maneno ya kilugha kama afanyavyo Linex katika kila nyimbo zake anazoimba. Diamond ameutendea haki wimbo huu, wimbo unagusa nyoyo za watu…..wimbo unagusa hisia……na tena wimbo unaweza ukakutoa machozi..! welldone Linex….welldone Diamond….welldone team nzima na management inayomsimamia Linex kufanikisha kuutoa wimbo huu Video ya wimbo huu inavutia sana, pongezi kubwa sana kwa aliyeandaa siclipt ya video hii kwa kuweza kuindaa katika kiwango cha kutazamika kwa kila rika, video hii……natumaini inaweza kutumika na baraza la mitihani ya taifa ya kidato cha nne ama cha sita kuwatengenezea maswali kwa somo la Kiswahili….sitashangaa nikiona wimbo wa salima wa linex ikiwa mojawapo ya maswali ya mtihani wa ngazi ya taifa, its fantastic video! Miongoni mwa video zinazotarajia kufanya vizuri zaidi hasa nje ya nchi kwani ni video inayoonyesha uhalisia wa kitanzania kabisa hakika Linex pamoja na Diamond Platnumz wamefanya kazi kubwa na wavutia kwenye hii video, Pongezi za ziada ziende kwa AJ ( huyu ni Adam Juma) amefanya kazi ya ziada kwa kushuti kwa ustadi wa hali ya juu video hii…..kwakweli naweza kusema hii ndio video bora kwangu kwa mwaka huu 2015 ingawa mwaka haujaisha.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments