NGOMA AFRICA BAND YAUNGANA NA WATANZANI KATIKA MAOMBOLEZO
YA MAREHEM JOHN KOMBA (RIP)
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya the Ngoma Africa band yenye maskani yake nchini Ujeumani inaungana na ,watanzania wote popote pale katika kipindi hiki cha msiba wa mwanamuziki marehemu John Komba (RIP) ,marehemu
alikuwa muasisi wa Kikundi cha muziki cha TOT,muhamasishaji,tutamkumbuka daima kwa mchanngo wake wa kuelemisha jamii kwa njia ya muziki.Ngoma Africa band inawapa pole ndugu na familia yote ya marehemu,pole na rambi rambi pia
ziwafikie TOT,Wapiga kura wa jimbo lake la Mbinga magharibi.Spika wa Bunge na bunge lote la Tanzania,marafiki,Uongozi na Chama Tawala CCM,wanamuziki na
watanzania wote, tupoe sote kwa msiba huu wa mwanamuziki Marehemu Kaptani
John Komba (RIP) mwenyezi mungu amlaze mahala pema.
Rambi rambi kutoka
Ngoma Africa Band
Oldenburg, Germany
The Ngoma Africa Band
www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments