Thursday, June 30, 2016

THE BEAT FESTIVAL 1. July 2016 at Paparazzi, Slipway

We are excited to announce the lineup for next edition of #THEBEATFESTIVAL. The program features Jagwa Music (mchiriku / afropunk), Peter Masima (traditional gogo music) and Mzungu Kichaa Unplugged (acoustic performance). Entrance; 10k only. Doors Open 21.00hrs.

JAGWA MUSIC – afropunk / mchiriku
Jagwa is the leading exponent of the Mchiriku style, which originated twenty years ago in the poor suburbs of Dar es Salaam. Jagwa and their peers were immediately attracted by the the small Casio keyboards lo-fi sound, adopted it, hooked it up to megaphone speakers, and the resulting gritty, edgy, distortion-laden sound became Mchiriku. Their career, which started in Mwananyamala, one of the poorer suburbs of Dar es Salaam, has taken them to some of the biggest stages across the globe.

PETER MASIMA – traditional gogo music
Peter Masima is a talented Gogo musician from Dodoma. He plays Marimba, locally known as ilimba and Zeze, a stringed fiddle, and is also a skilled instrument builder. He is fairly unknown on the cultural scene in Tanzania despite his enormous talent. We think it is about time that he is introduced to those who have yet to hear his “voice”. The late Hukwe Zawose who was signed to Peter Gabriels Real World Records made the music of the Wagogo popular globally. It has also been researched by a number of ethnomusicologists due to its rich and unique musical and cultural heritage.

MZUNGU KICHAA – unplugged performance
Debuting in 2009 with his album Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa and his band Bongo Beat have created a unique style of live Bongo Flava, which has taken them around the world. Tonight Mzungu Kichaa will perform a selection of old and new songs upfront and personal with a solo acoustic performance with his guitar after a two week songwriting retreat in Morogoro.


ABOUT THE BEAT: The Beat is a monthly festival showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is powered by: Caravan Records, Paparazzi Bistro Club, Jameson, and Goethe Institut Tanzania. Info: CRTanzania@gmail.comweb: www.facebook.com/TheBeatFestival


INSTAGRAM: @paparazzi_bistro_club, @thebeatfestival, @CRTanzania, @GoetheTanzania, @MzunguKichaa #thebeatfestival

FACEBOOK: @paparazzi_bistro_club, @thebeatfestival, @CRTanzania, @GoetheTanzania, @MzunguKichaa #thebeatfestival


Monday, June 27, 2016

Mti wenye muonekano wa kichwa cha binadamu mjini Tanga

Mti wenye muonekano wa kichwa cha binadamu na kufananashwa na hayati baba wa Taifa Mwl Nyerere, mti huo upo eneo maarufu kama Tangamano.

Ukipaki pasipo rushusiwa faini itakuhusu...Darajani

Darajani ni moja ya sehemu ambayo kumetengwa eneo maalum kwa ajili ya packing eneo ambalo zamani ilikuwa ni kituo cha daladala karibu kabisa na Markit.
Ukienda tofauti na utaratibu wa kupaki eneo lisiloruhusiwa faini kutoka kwa wasimamizi wa maeneo toka manispaa itakuhusu.

New VIDEO: Mabantu - CHAPA TWENDE (Official Music Video)

Bonyeza hapa tazama video hii https://www.youtube.com/watch?v=MeD47UiiRPA

Saturday, June 18, 2016

Thursday, June 16, 2016

Chid Benz ang'ara

Miezi kadhaa iliyopita alikuwa ni gumzo kubwa kila kona baada ya afya yake kudhoofika kwa utumiaji wa madawa ya kulevya hadi kufikia hatua ya kupelekwa Sober house Bagamoyo na kuishi kwa siku kadhaa kwa lengo la kupata tiba ya kuacha kutumia madawa.
Chid Benz akiwa na muonekano mpya 

Juni 15, 2016 Chadi Benzi alipost picha kadhaa zinazomuonyesha akiwa katika muonekano mpya ikiwa ni siku chache baada ya kutoka Sober house Bagamoyo.

"Wanachama wasubiri kauli ya vikao" Maalim Seif.


Wakati mda wa kuzima simu feki ukisubiriw....


Wednesday, June 15, 2016

Happy Birthday Lady Jay D

Mwaka 2000 ndo ulikuwa mwaka uliomtambulisha na kumfungulia milango ya mafanikio msanii wa kike kutoka Tanzania Lady Jay Dee baada ya kutoka na album yake ya kwanza aliyoipa jina la machozi.
Sio jambo jepesi kwa msanii kutoa album hasa hapa Tanzania ila kwa Jay Dee ni tofauti kwani amefanikiwa kuwa na album sita hadi sasa tangu kuanza muziki, heshima yake kwa jamii na wasanii imezidi kuongezeka kutokana na ujasiri alionao katika kupambana na harakati za muziki na changamoto za maisha yake, "hapo ndipo watu huamini kuwa huyu kweli ni komando".
Maisha yake baada ya kutengana na aliyekuwa mumewe ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Clouds fm Gadna G Habash Captain, wengi walidhani Jay Dee hawezi kufanya vizur katika muziki wake, mambo yamekua tofauti baada ya kuja na ngoma "Ndi Ndi Ndi" ambayo inazidi kufanya vizuri audio na video.
Tarehe na mwezi kama wa leo huko mkoani shinyanga katika familia ya watoto kumi alizaliwa Judith wambura Lady Jay Dee 
Happy Born Day Judith Lady Jay Dee.

Dar es Salaam kuzindua huduma ya Uber

                                                 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Dar es Salaam kuzindua Uber

Dar es Salaam yaungana na orodha ya miji mashuhuri barani Afrika kutoa huduma ya Uber

Dar es Salaam, Juni 2016. Leo, Dar es Salaam inakuwa mji wa 475 kujiunga na mtandao unaokuwa wa Uber duniani. Kwa uzinduzi wa Uber, jukwaa la ubunifu wa kiteknolojia, Dar es Salaam inaungana na orodha ya vituo maarufu vya usafiri barani Afrika. Kufuatia mafanikio ya Uber katika nchi nyingi, Uber inayo furaha kuzindua jukwa la ushirika la abiria kwa watu wa Dar es Salaam.


Uber Dar es Salaam
Jukwaa la mtandao wa ubunifu la Uber, huwaunganisha madereva na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe. Au ukiwa unatoka na marafiki kwenda mjini kibiashara, au kuangalia vivutio vya kitalii, Uber hutoa njia rahisi yenye unafuu kufika kila mahali.
Dar es Salaam Jiji linalokua kwa kasi kibiashara, linafanya iwe ni mahali sahihi kwa Uber. Taarifa za Benki ya Dunia zinasema kwamba Pato halisi la Tanzania (GDP) linakadiriwa kuwa 6.8% kwa mwaka 2017 na nchi imeweza kuhimili mfumuko wa bei. Biashara zinakua kwa kasi katika sekta za usafiri, ujenzi na fedha.   

Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits anasema:
“Tunajivunia kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua. Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda, hivyo huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa kuaminika.”
Akaongeza, “Tumeweka viwango vya kuunganisha watu katika usafiri wenye kiwango cha juu duniani, kusafirisha mamilioni ya watu duniani kote kila siku kupitia huduma zetu za usafiri  nafuu na za kuaminika kwa kubonyeza kitufe tu. Huduma zetu zinaenda sambamba na aina za usafiri uliopo, hivyo wote tunaweza kufanya kazi pamoja kupunguza foleni barabarani na kuboresha mazingira ya usafiri katika jiji.

Kwanini Uber?
Uber husaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe-hakuna kusubiri barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta basi. Ni njia bora na karibu zaidi kupata usafiri salama, nafuu na wa kuaminika.

Kabla ya kuingia ndani ya gari
  • Hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo ukisubiri gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani kusubiri taksi au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu muda wa usiku.   
  • Safari hazina kificho. Mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia kama kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua.

Wakati wa Safari
  • Julisha mahali ulipo. Unaweza kuwajulisha ndugu na marafiki zako kwa furaha zaidi juu ya mipango ya safari yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na mahali ulipo, na muda unaotarajia kuwasili. Watapokea linki ambapo wataweza kuona muda kamili, jina na picha ya dereva, gari lake na mahali ulipo katika ramani hadi utakapowasili na wanaweza kufanya haya yote bila haja ya kupakua App ya Uber wao wenyewe.

Baada ya Safari
  • Fanya mrejesho na toa alama kila baada ya safari.  Baada ya kila safari, wewe na dereva wako mnahitaji kupeana alama na kufanya mrejesho. Timu yetu ya usalama hupitia taarifa hizi na kufanya uchunguzi juu ya kila jambo.
  • Msaada masaa 24 kwa wiki. Endapo jambo litatokea ndani ya gari, kama ni ajali ya barabarani au kutoelewana kati yako na dereva, mfanyakazi wetu wa huduma kwa wateja yupo tayari kukusaidia kwa suala lolote masaa 24 kwa wiki.
  • Msaada wa Haraka. Tuna timu mahiri inayoshughulika na matukio kujibu suala lolote linalohitaji ufumbuzi wa haraka. Tukipokea taarifa kuwa dereva au abiria amesababisha tukio la hatari au hayupo njia sahihi, tunafunga akaunti zao na kumzuia asiweze tena kuingia katika jukwaa la Uber wakati tukifanya uchunguzi.

Nyuma ya Pazia
  • Muda wote kwenye ramani. Kukubali kuwajibika ni moja ya mambo yanayofanya wasafiri kujisikia wako salama ndani ya Uber. Tunatumia teknolojia ya mawasiliano ya GPS kuweka taarifa za mahali madereva wanakotakiwa kwenda wakati wa safari, ili kutuwezesha kuthibitisha njia zinazotumika ni bora, kitu kichanachojenga uwajibikaji na ushawishi mkubwa kwa utendaji mzuri.
  • Utendaji na mamlaka za sheria. Endapo mamlaka za kisheria zinatupa taratibu za kisheria, tunatafanya kazi kutafuta vielelezo, mfano kwa kutoa taarifa za safari. Hata hivyo uwazi na uwajibikaji upo katikati ya mafanikio ya Uber.       
  • Upimwaji wa madereva. Madereva wote lazma awapitie mchakato wa upimwaji kabla ya kuanza kutumia App ya Uber

Alon Lits aliongeza:
“Uber ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya usafirishaji. Dar es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana mahiri wenye nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti huduma yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”
Uber inasherehekea uzinduzi mjini Dar es Salaam kwa kutoa huduma ya bure ya usafiri. Tanzania wanaweza kujaribu huduma mpya kwa kupata huduma ya bure kwa kuingia kwenye App ya Uber. .

MAKUBALIANO (vigezo kwa usafiri wa bure)
  • Ni lazima upakue App ya Uber na weka kificho cha promosheni MoveTanzania ili upokee usafiri wa bure
  • Usafiri wa bure utapatikana kutoka Alhamisi Juni 16 saa 6 mchana mpaka Jumapili Juni 19 katikati ya usiku.
  • Watumiaji watapata usafiri wa bure kwa safari sita tu na kila safari isizidi kiasi cha shs 12,000
  • Usafiri wa bure utapatikana tu kwa safari zinazoanzia na kuishia maeneo ya Dar es Salaam yaliyopangwa.

- Mwisho -
Kuhusu Uber
Uber ni kampuni ya teknolojia inayowaunganisha wasafiri na madereva kwa kiasi cha kubonyeza kitufe. Hupatikana kwenye miji 475 katika nchi 73, jukwaa la Uber hujumuisha jinsi dunia inavyokwenda. Malengo ya Aber ni kubadilisha mtazamo wa watu jinsi wanavyokwenda duniani, kufanya kazi na kuishi. Inajihusisha kubadilisha jinsi watu wanavyoungana na familia zao, hivyo huleta uaminifu na ukaribu kwa kutoa nafasi katika mipango ya usafiri.

Monday, June 13, 2016

NYIMBO KWAAJILI YA SIKU YA MAADHIMISHO YA ALBINISM DUNIANI

LEO NI SIKU YA MAADHIMISHO YA WATU WENYE ALBINO DUNIANI nachukua fulsa hii ya kuwaomba watanzania mniunge mkono juu ya mapambano haya kwa kudownload nyimbo hii na kuisambaza ilitupinge mauaji ya ndugu zetu...please please usi like tuu nakuipita picha hii download nyimbo hii BUREE AU KWA KULIPIA SH 250/= kutoa mchango wako kwenye mapambano haya.. Kwa pamoja tunaweza.. DOWNLOAD HAPA https://mkito.com/song/11609  
Today is world albinism day please join me the fight agaist killing of albinos by downloading my song and share it to join the movement DOWNLOAD THE SONG HERE https://mkito.com/song/11609
COMMENT NAMBA YAKO TUKUTUMIE WHATTSAPP AU TUTEXT NAMBA YAKO INBOX TUKUTUMIE NYIMBO. KAMAUNAPENDA KUCHANGIA VIDEO SHOOTING TUTEXT HAPA 0628 602 863
Ujumbe huu kutoka kwa Kapuku digital nimeupost kama alivyotutumia sapoti yako ni muhimu katika kupinga mauaji ya ndugu zetu.

Peter Msechu adondosha wimbo mpya na Banana Zoro "MAMA"


Zipo nyimbo nyingi sana ambazo zimekuwa zikizungumzia ukuu wa mama malezi yake na heshima yake kiujumla, thamani ya mama haina mfano Peter Msechu na Banana Zoro wameendelea kueleza na kutangaza thamani ya mama katika familia na hasa akijaribu kuonyesha thamani kubwa ndani yao katika familia zetu.
Utofauti wake unakuja pale tu tulipoamua kuonyesha kuwa hata wale tunaoishi nao kama wake zetu ama wapenzi wetu wana nafasi kubwa ya kututunza na kutulea kama wazazi wetu wafanyavyo. 
Unakumbuka pia katika hit song za Banana wimbo wake wa Mama ulipenya vizuri kutokana na ujumbe wake unaohusu Mama.

Saturday, June 11, 2016

Mel Gibson kuja na muendelezo wa filamu ya The Passion of the Christ

Muongozaji mahiri wa filamu nchini Marekani, Mel Gibson amepanga kuja tena na muendelezo wa filamu yake ya mwaka 2004, The Passion of the Christ.
Screenwriter Randall Wallace aliyeandika filamu nyingine ya Gibson, Braveheart — hivi karibuni aliiambia tovuti ya The Hollywood Reporter kuwa ameanza kufanyia kazi muendelezo wa filamu hiyo iliyoonesha saa 12 za mateso aliyopata Yesu Kristo.
Filamu ya pili itajikita kwenye ufufuko wake.
The Passion of the Christ ilikuwa na bajeti ya dola milioni 30 na kuingiza dola milioni 611 na kuwa filamu ya kujitegemea iliyofanikiwa zaidi kwenye historia.
Chanzo Bongo5.com

Samia x Best Nasso - Dharau (Official Music Video)

Best Nasso adondosha audio na video mpya "Ukweli Uko wapi?

Bofya hapa kudownload video "Ukweli uko wapi?': https://www.youtube.com/watch?v=VH9JYCxVDhY

Kapuku Digital aachia wimbo maalum kwa ajili ya maadhimisho ya albinism duniani june 13



Msanii wa hip hop machachari  Kapuku Digital wa Arusha anaungana na wanaharakati mbalimbali duniani kwa kutunga wimbo yenye tungo za hasira ya kuazimisha siku ya albinism duniani tarehe 13 June kila mwaka..kwa kupinga mauaji ya ndugu zetu albino...

Baada ya kusikiliza nyimbo hii unaweza ukavunja vunja viti au kupandwa na hasira na kupiga mtu au unaweza ukapandwa na hasira na ukalia uka umia sana kwa mateso wanayo ya pata ndugu zetu.. 'Kila nikiimba wiimbo huu napandwa na hasira. nimepatashida sana kurekodi wimbo huu kwasababu ilikua inanipandisha hasira nililazimika kusimama kila wakati wakati narecord.pls' maneno ya Kapuku Digital.

DOWNLOAD HAPA MKITO https://mkito.com/song/11609 au HAPA MDUNDO http://mdundo.com/dl/48436/high NA SHARE ILIKUPINGA MAUAJI YA ALBINO NA kama unapenda kuchangia video shooting ya wimbo huu wasiliana Kapuku kupitia email kapukudigital@gmail.com 
Kapuku ameongeza kusema kuwa 'kama kuna director atatuungamkono kwakushoot video mungu atambariki sana' 
'PLEASE DOWNLOAD AND SHARE THIS SONG TO FIGHT AGAINST KILLING OF OUR FRIEND WITH ALBINISM WORLD WIDE****PLEASE MA DJ NA MAPRESENTER TUNAOMBA USHIRIKIANO MAPAMBANO HAYA MPAKA ITAKAPO FIKIA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA ALBINISM DUNIANI TAREHE:13 JUNE'