Mwaka 2000 ndo ulikuwa mwaka uliomtambulisha na kumfungulia milango ya mafanikio msanii wa kike kutoka Tanzania Lady Jay Dee baada ya kutoka na album yake ya kwanza aliyoipa jina la machozi.
Sio jambo jepesi kwa msanii kutoa album hasa hapa Tanzania ila kwa Jay Dee ni tofauti kwani amefanikiwa kuwa na album sita hadi sasa tangu kuanza muziki, heshima yake kwa jamii na wasanii imezidi kuongezeka kutokana na ujasiri alionao katika kupambana na harakati za muziki na changamoto za maisha yake, "hapo ndipo watu huamini kuwa huyu kweli ni komando".
Maisha yake baada ya kutengana na aliyekuwa mumewe ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Clouds fm Gadna G Habash Captain, wengi walidhani Jay Dee hawezi kufanya vizur katika muziki wake, mambo yamekua tofauti baada ya kuja na ngoma "Ndi Ndi Ndi" ambayo inazidi kufanya vizuri audio na video.
Tarehe na mwezi kama wa leo huko mkoani shinyanga katika familia ya watoto kumi alizaliwa Judith wambura Lady Jay Dee
Happy Born Day Judith Lady Jay Dee.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments