Zipo nyimbo nyingi sana ambazo zimekuwa zikizungumzia ukuu wa mama malezi yake na heshima yake kiujumla, thamani ya mama haina mfano Peter Msechu na Banana Zoro wameendelea kueleza na kutangaza thamani ya mama katika familia na hasa akijaribu kuonyesha thamani kubwa ndani yao katika familia zetu.
Utofauti wake unakuja pale tu tulipoamua kuonyesha kuwa hata wale tunaoishi nao kama wake zetu ama wapenzi wetu wana nafasi kubwa ya kututunza na kutulea kama wazazi wetu wafanyavyo.
Unakumbuka pia katika hit song za Banana wimbo wake wa Mama ulipenya vizuri kutokana na ujumbe wake unaohusu Mama.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments