Saturday, June 11, 2016

Mel Gibson kuja na muendelezo wa filamu ya The Passion of the Christ

Muongozaji mahiri wa filamu nchini Marekani, Mel Gibson amepanga kuja tena na muendelezo wa filamu yake ya mwaka 2004, The Passion of the Christ.
Screenwriter Randall Wallace aliyeandika filamu nyingine ya Gibson, Braveheart — hivi karibuni aliiambia tovuti ya The Hollywood Reporter kuwa ameanza kufanyia kazi muendelezo wa filamu hiyo iliyoonesha saa 12 za mateso aliyopata Yesu Kristo.
Filamu ya pili itajikita kwenye ufufuko wake.
The Passion of the Christ ilikuwa na bajeti ya dola milioni 30 na kuingiza dola milioni 611 na kuwa filamu ya kujitegemea iliyofanikiwa zaidi kwenye historia.
Chanzo Bongo5.com

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments