Saturday, September 15, 2012
Saturday, September 1, 2012
Friday, August 31, 2012
KUNGURU WAMEKUWA KERO KITUO CHA MABASI TANGA
Kila ifikapo majia ya jioni imekuwa ni kawaida kwa kunguru hawa kukusanyika kwenye miti iliyopo kwenye kituo cha mabasi ikiwa kama hifadhi yao kwa ajili ya kulala.
Hali hii ni yamuda mrefu ambayo imekuwa ni kero kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaokuwepo eneo hilo kwa muda wa jioni.
Mara kwa mara kunguru hao wamekuwa wakiwanyea watu na kuwapigia kelele ikikapo mida ya jioni.
Mkurugenzi wa mji hili linakuhusu sana katika kutafuta namna ya kuweza kuhamisha makazi ya kunguru hao ili wananchi wako waweze kuwa na amani wakaapo katika eneo hilo.
Hali hii ni yamuda mrefu ambayo imekuwa ni kero kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaokuwepo eneo hilo kwa muda wa jioni.
Mara kwa mara kunguru hao wamekuwa wakiwanyea watu na kuwapigia kelele ikikapo mida ya jioni.
Mkurugenzi wa mji hili linakuhusu sana katika kutafuta namna ya kuweza kuhamisha makazi ya kunguru hao ili wananchi wako waweze kuwa na amani wakaapo katika eneo hilo.
BIBI BOMBA NAMBA 3 AREJEA ZANZIBAR
Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.
Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)
Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.
Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.
Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.
Thursday, August 30, 2012
KWANI WAMACHINGA NI KERO?
Wamachinga wakiwa wamepanga biashara zao pembezone mwa barabara kubwa ya magari maeneo ya kituo bangi (Tanga)
Wamachinga wakiendelea kufanyabiashara zao katika kituo cha daladala Darajani Zanzibar
Mara nyingi serikali imekuwa ikipiga kelele juu ya wafanyabiashara hao kuwa wawe na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo na kuwatengea maeneo yanayostahili kuwapo. Lakini mbali na kutengewa maeneo wafanyabiashara hao hawapo tayari kuyatumia maeneo hayo wakihofia hawawezi kuwapata wateja wanaowategemea katika biashara zao.
Ni kweli wamachinga ni msaada kwa watu kwa maeneo wanayoyatumia ikiwa ni Stendi za mabasi , vituo vya daladala na pembezoni mwa barabara kwani wanawarahisishia wasafiri kupata mahitaji kwa ukaribu zaidi.
Tatizo kubwa linalopelekea kuwa ni kero kwa watu ni ile hali ya wafanyabishara hao kutumia maeneo ya watembea kwa miguu barabarani kuweka biashara zao hali inayohatarisha maisha ya watembea kwa miguu kwa kukosa sehemu ya kupita na kusababisha wapite barabara kubwa yanapopita magari. Kwa upande wa vituoni wanapelekea msongamano usio kuwa wa lazima na kusababisha hali ya wizi kuongezeka.
Baada ya kuonekana hayo kuna haja ya serikali kuangalia namna nyingine ya kuweza kuwasaidia wafanyabiashara wa namna hii ambao wapo karibia Tanzania nzima.
Wednesday, August 29, 2012
MAKARANI WA SENSA WANAPAMBANA MENGI ....."MABLACK AMERICA WAHESABIWA LEO"
Hii ndio hali halisi wanayokutana nayo makarani wa sensa nyakati za asubuhi.
Kijna akijibu maswali anayoulizwa na karani
Maelezo yalikuwa yakiendelea
Karani akihakiki maelezo aliyopewa
Karani wa sensa akiweka tiki baada ya kumalisha kuhesabu wenye kaya
Nyumba iliyohesabiwa inawekwa tiki namna hii.
Tuesday, August 28, 2012
WAFANYABIASHARA SEGERA MAMBO MAGUMU
Wafanyabiashara ya machungwa wakikimbilia basi la abiria kwa ajili ya kuwauzia abiria machungwa
Segera ni kituo kikubwa cha wafanyabiashara ndogondogo ya machungwa, mahindi na biashara zingine zinazoendana na msimu, wateja wao wakubwa wanaowategemea ni wasafiri wa mikoani pamoja na nje ya nchi ambao wanapita eneo hilo.Inafahamika hakuna biashara inayokosa mitihani bila kujali ukubwa wa biashara yenyewe, Bwana Saidi Juma mmoja wa wafanyabiashara ya machungwa alieleza changamoto wanazokutana nazo katika biashara yao "Biashara yetu ni nzuri sana kwa sababu haipiti siku bila kuuza japo mifuko kumi na kuendelea na hapa ni sehemu ambayo mabasi mengi yanayokwenda Arusha, Nairobi, Kampala, Moshi, Tanga na sehemu nyingine lazima yapite na yako mengi sana".
Mbali na biashara kuwa nzuri pia kunamatatizo mengi wanayokabiliana nayo wafanyabiashara hao ikiwa ni pamoja na abiria kuondoka na machungwa bila ya kulipa ama kushindwa kurudishiwa chenji hali ambayo inawapelekea kuoneka waizi "Wakati mwingine mteja anachukua machungwa kabla hajatoa pesa basi linawahi kuondoka ama anaweza kutoa pesa kubwa kabla hujampa chenji basi likaondoka kwa hiyo inakuwa hasara kwetu ama kwa mteja hali ambayo inatujengea picha mbaya ya kuonekana sio waaminifu na inatokea wakati mwingine tunapata ajali kutokana na kazi yetu hii lazima ukimbilie basi kwa sababu mabasi mengine hayasimami na unakuta abiria anahitaji kununua machungwa" Hayo alisema Shekhan Abdalah.
Waliongeza kusema kuwa ugumu wa biashara yao unasababishwa na hali ya kutokuwa na kituo kikubwa cha kuweza kusimama mabasi kwa nafasi hivyo madereva wanachukulia ni sehemu ambayo hawastahili kusimama endapo hana abiria anaeshuka ama anaepanda. Wapo wateja ambao wanapita na magari binafsi ambao ndio wateja wao wazuri kwa kuwa wanapata muda mwingi wa kusimama na kuagiza machungwa mengi na kuchagua mwenyewe ambayo ni mazuri zaidi.
Wafanyabiashara hao wametoa wito kwa serikali wajengewe kituo maalum eneo hilo ambacho kitapelekea mabasi kuweza kusimama kwa nafasi na abiria wakapata muda mzuri wa kuweza kununua machungwa kwa utaratibu mzuri ili waweze kuachana na kukimbiza magari hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.
Friday, August 24, 2012
HALI YA BARABARA YA KUELEKEA IKULU TANGA
Hii ndio barabara kubwa ya kuelekea IKULU mkoani Tanga.
Hali ya kusikitisha kuona wasimamiazi wa barabara hawajali ubovu wa barabara za mitaani hatimae uharibikaji wa barabara hizo kuongezeka siku hadi siku.
Imezoeleka kuona matengenezo ya barabara nyingi kufanyika pale inapotokea ziara ya kiongozi mkubwa wa nchi anahitajika kupita katika barabara hiyo, hapo utaona wahusika wanavyoanza matengengenezo ya barabara hizo hali inayowavunja moyo wananchi kuona kwamba hawana thamani katika nchi hii ndio maana matengenezo ya barabara yanafanyika pale wanapohitajika kupita Viongozi ambao ndio wanaonekana kuwa na thamani.
Hali ya barabara hii ambayo ndio barabara kubwa ya kuelekea IKULU ya Mkoa wa Tanga kama inavyoonekana ni miezi mingi imepita hali hivyo ilivyo ndivyo wananchi wanavyoitumia barabara hiyo ambao imekuwa ni kero kwao, lakini "itapotokea Mh Raisi anakwenda Mkoani Tanga utaona matengenezo yanaanza" hivyo ndivyo wananchi walivyokuwa wakilalamika
TRENI KUSHNEEEEEEEEY TANGA ...HALI YA RELI YA KATI IPO HIVI
Kwa sasa ni majani ndio yaliotawala kwenye Reli ya Kati mkoani Tanga hali inayoonyesha hakuna matumaini ya kurejeshwa tena usafiri wa Treni kwa reli ya kati.
COCONUT DIGITAL SASA IPO KITAANI
Baada ya kupata mateso kwa muda mrefu kwa kutumia ving'amuzi visivyo na kiwango na vinavyoongoza kukwamakwama nakujikuta malipo yako ya mwezi hayaendi kihalali sasa Coconut Digital imekuja kukidhi kiu yako kwa channel bomba za burudani na michezo.
Fika ofisi za Coconut Digital zilizopo jengo la Coconut Fm ujipatie kingamuzi bora chenye uwezo mkubwa wa kuonyesha vizuri bila kusitasita.
Fika ofisi za Coconut Digital zilizopo jengo la Coconut Fm ujipatie kingamuzi bora chenye uwezo mkubwa wa kuonyesha vizuri bila kusitasita.
Thursday, August 23, 2012
HAPA NDIO ZERO KILOMETA MKOA WA TANGA INAPOANZIA
Mnara huu umejengwa mwaka 1901 ambao ndio unatumika kama alama ya kuanzia kuhesabu kilometa za mkoa wa Tanga (Zero Kilometa),
KITUO BANGI CHAPIGWA RIPEA
Kituo cha daladala maarufu kama kituo bangi kilichopo mjini karibu na stendi ya mokoa chafanyaiwa matengenezo baada ya kuwa kero kwa madereva daladala kwa kuwa na mashimo kupita kiasi.
WAKAZI WA MBAGALA WAONGEZEWA UPANA WA BARABARA
Barabara ya Mbagala ujenzi unaendelea
Serikali kwa kulitambua hilo imeambua kuongeza upana wa barabara hiyo inayotumika na wakazi wa Mbagala ambayo itakapokamilika itakuwa na barabara tatu hadi nne kwa baadhi ya maeneo hali ambayo itapelekea kuondoa kero kwa wakazi hao.
Subscribe to:
Posts (Atom)