Tuesday, August 28, 2012

WAFANYABIASHARA SEGERA MAMBO MAGUMU

Wafanyabiashara ya machungwa wakikimbilia basi la abiria kwa ajili ya kuwauzia abiria machungwa
Segera ni kituo kikubwa cha wafanyabiashara ndogondogo ya machungwa, mahindi na biashara zingine zinazoendana na msimu, wateja wao wakubwa wanaowategemea ni wasafiri wa mikoani pamoja na nje ya nchi ambao wanapita eneo hilo.

Inafahamika hakuna biashara inayokosa mitihani bila kujali ukubwa wa biashara yenyewe, Bwana Saidi Juma mmoja wa wafanyabiashara ya machungwa alieleza changamoto wanazokutana nazo katika biashara yao "Biashara yetu ni nzuri sana kwa sababu haipiti siku bila kuuza japo mifuko kumi na kuendelea na hapa ni sehemu ambayo mabasi mengi yanayokwenda Arusha, Nairobi, Kampala, Moshi, Tanga na sehemu nyingine lazima yapite na yako mengi sana".

Mbali na biashara kuwa nzuri pia kunamatatizo mengi wanayokabiliana nayo wafanyabiashara hao ikiwa ni pamoja na abiria kuondoka na machungwa bila ya kulipa ama kushindwa kurudishiwa chenji hali ambayo inawapelekea kuoneka waizi "Wakati mwingine mteja anachukua machungwa kabla hajatoa pesa basi linawahi kuondoka ama anaweza kutoa pesa kubwa kabla hujampa chenji basi likaondoka kwa hiyo inakuwa hasara kwetu ama kwa mteja hali ambayo inatujengea picha mbaya ya kuonekana sio waaminifu na inatokea wakati mwingine tunapata ajali kutokana na kazi yetu hii lazima ukimbilie basi kwa sababu mabasi mengine hayasimami na unakuta abiria anahitaji kununua machungwa" Hayo alisema Shekhan Abdalah.

Waliongeza kusema kuwa ugumu wa biashara yao unasababishwa na hali ya kutokuwa na kituo kikubwa cha kuweza kusimama mabasi kwa nafasi hivyo madereva wanachukulia ni sehemu ambayo hawastahili kusimama endapo hana abiria anaeshuka ama anaepanda. Wapo wateja ambao wanapita na magari binafsi ambao ndio wateja wao wazuri kwa kuwa wanapata muda mwingi wa kusimama na kuagiza machungwa mengi na kuchagua mwenyewe ambayo ni mazuri zaidi.

Wafanyabiashara hao wametoa wito kwa serikali wajengewe kituo maalum eneo hilo ambacho kitapelekea mabasi kuweza kusimama kwa nafasi na abiria wakapata muda mzuri wa kuweza kununua machungwa kwa utaratibu mzuri ili waweze kuachana na kukimbiza magari hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments