Friday, August 24, 2012

HALI YA BARABARA YA KUELEKEA IKULU TANGA

Hii ndio barabara kubwa ya kuelekea IKULU mkoani Tanga.
Hali ya kusikitisha kuona wasimamiazi wa barabara hawajali ubovu wa barabara za mitaani hatimae uharibikaji wa barabara hizo kuongezeka siku hadi siku. Imezoeleka kuona matengenezo ya barabara nyingi kufanyika pale inapotokea ziara ya kiongozi mkubwa wa nchi anahitajika kupita katika barabara hiyo, hapo utaona wahusika wanavyoanza matengengenezo ya barabara hizo hali inayowavunja moyo wananchi kuona kwamba hawana thamani katika nchi hii ndio maana matengenezo ya barabara yanafanyika pale wanapohitajika kupita Viongozi ambao ndio wanaonekana kuwa na thamani. Hali ya barabara hii ambayo ndio barabara kubwa ya kuelekea IKULU ya Mkoa wa Tanga kama inavyoonekana ni miezi mingi imepita hali hivyo ilivyo ndivyo wananchi wanavyoitumia barabara hiyo ambao imekuwa ni kero kwao, lakini "itapotokea Mh Raisi anakwenda Mkoani Tanga utaona matengenezo yanaanza" hivyo ndivyo wananchi walivyokuwa wakilalamika

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments