Wamachinga wakiwa wamepanga biashara zao pembezone mwa barabara kubwa ya magari maeneo ya kituo bangi (Tanga)
Wamachinga wakiendelea kufanyabiashara zao katika kituo cha daladala Darajani Zanzibar
Mara nyingi serikali imekuwa ikipiga kelele juu ya wafanyabiashara hao kuwa wawe na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo na kuwatengea maeneo yanayostahili kuwapo. Lakini mbali na kutengewa maeneo wafanyabiashara hao hawapo tayari kuyatumia maeneo hayo wakihofia hawawezi kuwapata wateja wanaowategemea katika biashara zao.
Ni kweli wamachinga ni msaada kwa watu kwa maeneo wanayoyatumia ikiwa ni Stendi za mabasi , vituo vya daladala na pembezoni mwa barabara kwani wanawarahisishia wasafiri kupata mahitaji kwa ukaribu zaidi.
Tatizo kubwa linalopelekea kuwa ni kero kwa watu ni ile hali ya wafanyabishara hao kutumia maeneo ya watembea kwa miguu barabarani kuweka biashara zao hali inayohatarisha maisha ya watembea kwa miguu kwa kukosa sehemu ya kupita na kusababisha wapite barabara kubwa yanapopita magari. Kwa upande wa vituoni wanapelekea msongamano usio kuwa wa lazima na kusababisha hali ya wizi kuongezeka.
Baada ya kuonekana hayo kuna haja ya serikali kuangalia namna nyingine ya kuweza kuwasaidia wafanyabiashara wa namna hii ambao wapo karibia Tanzania nzima.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments