Wednesday, August 1, 2012

MRATIBU WA COCONUT FM ALI KHATIB DAI APATA AJALI MAENEO YA JKU

Ajali hiyo ilitokea maeneo ya JKU jana jioni baada ya gari hilo aina ya NOAH yenye nambari za usajili Z 167 CF kupasuka mpira wa mbele na kupelekea kuvamia machuma ya ukingo wa barabara.

Dereva wa gari hilo Ali Khatib Dai ambae ni mratibu wa Coconut FM alisema " Tulikuwa watu 6 tunatoka Dole tunarudi mjini mida ya saa 11 jioni tumefika maeneo ya JKU ghafla nikahisi kiza mbele yangu baada ya kiza kilichoendelea sikujua baada ya muda mfupi ndio nagundua kuwa tumepata ajali, Nilikuwa katika spidi ya kawaida sana lakini mungu amesaidia watu wawili wameumia kidogo sana mmoja alishtuka mkono na mwingine alijigonga mguuni lakini wote wako safi sasa hivi walienda hospitali na kupata matibabu".

Askari wa usalama barabarani waliwahi kufika eneo la ajali na kufanya kazi yao iliyowapeleka pale na kuruhusu gari kutolewa kwa ajili ya kupelekwa Kituo cha polisi Malindi.

Gari hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Primetime Promotion iliyopo jijini Dar es Salaam kwa jina la usajili lakini inatumiwa na kituo chao cha redio Coconut Fm Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments