Kwa mujibu wa wakazi mkoani Tanga usafuiri wa Baiskeli pamoja na Pikipiki sio kero kwao kutokana na kuwa ndio usafiri tegemezi kwa watu wengi takribani robo tatu ya wakazi wa mkoa huo ndio usafiri wao.
Wengi wao ambao ni watumiaji wa usafiri wa aina hiyo wamesema kuna bodaboda za baiskeli na pikipiki hivyo kila mtu anaagalia uwezo wake na safari yake, Usafiri wa bodaboda wa baiskeli unaanzia kiasi cha shilingi mia tano (sh.500/-) kwa safari ya karibu na usafiri wa Pikipiki unaanzia shilingi 1000/-, pia zipo baiskeli ambazo zinakodishwa kwa saa shilingi 300/- dereva ukiwa ni wewe mwenyewe.
Kwa hiyo usafiri wa baiskeli na pikipiki sio kero kwa wakazi wa mjini Tanga kwakuwa unarahisisha shughuli zao ndogondogo za hapo mjini.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments