Wednesday, July 31, 2013

"Same Same Girl" Muungano wa Akilimali na Paradise


Msanii wa dancehall AkiliMali aungana na Paradise,Msanii wa bongo fleva mwenye makazi yake mjini Arusha kuunda "Same Same Girl" track iliyofanyikia Noizmekah Production,

Ngoma hiyo ya miondoko ya dancehall pata kuusiikiliza HAPA na endelea kusapoti muziki wa Tanzania kwa mawasiliano,mahojiano zaidi check na Akilimali kupitia +255 767 955 405 powered by vmgafrica.com

Naibu Waziri wa Afya, Mh. Dr. Seif Rashid Afungua Kongamano la Kujadili Dawa Bandia

Kongamano la siku 3 kujadili dawa
bandia limefunguliwa leo na naibu
waziri wa afya, Mheshimiwa Dr Seifu Rashid. Kongamano hili linahudhuruwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali Africa zikiwamo Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Malawi, Botswana, South Africa, Zambia, Eritrea, Ethiopia, Madagascar, Zimbabwa, Namibia na
Mozambique. Pia kuna wawakilishi toka USA na makao makuu ya shirika la afya dunia (WHO).

Wajumbe wa kongamano watapata
nafasi ya kujifunza mfumo mpya wa kompyuta wa jinsi ya kutoa na kupata taarifa mbalimbali juu ya dawa bandia.

Kongamano linafanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), uliopo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Mr Hiiti B. Sillo, Mkurugenzi wa TFDA akitoa utangulizi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.

Naibu waziri, Dr. Seifu Rashid akifungua rasmi kongamano hio, kulia kwake ni Michael Deats kutoka makao makuu Shirika la Afya Duniani (WHO)

Sehemu ya washiriki wa kongamano.
Chanzo Michuzi blog
My Blog Name

Ommy Dimpoz akiendendeleza tour yake nchini burundi

Tuesday, July 30, 2013

Harakati za kuwahi futari wakazi wa magomeni,mabawa,magaoni

Muonekano wa stend kuu ya mabasi Tanga usiku huu

Maini ya kuku yastaajabisha watu.


Kuku mmoja aliyechinjwa na bwana Boha jioni ya leo amekutwa na Maini makubwa yanayokadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya robo kilo hali ambayo sio ya kawaida kwa kuku kuwa na ukubwa wa Maini kiasi hicho.
Mr Boha anaeishi Nguvumali kagera mjini Tanga alishangazwa sana na ukubwa wa Maini hayo hali iliyopelekea kuwa na hofu kubwa juu ya nyama ya kuku huyo.

Furaha ya leo brand new track ya msanii dream


Msanii Dream kutoka Dar ameachia Track mpya inayoitwa "Furaha ya leo"
So wakati wako sasa wa kuitafuta track hiyo uisikilize na kumpa sapoti kijana navmuziki wa Tanzania.
Kwa mawasiliano bongofreva contact info dreammalaika@yahoo.com.

Monday, July 29, 2013

Mchizi Mox ajitolea usafiri wa bure kwa wakazi wa Dar


Msanii anayewakilisha kundi la WATEULE MCHIZI MOXIE jana majira ya mchana aliamua kujitolea kukodi gari la abiria kampuni ya UDA kwa muda wa masaa manne na kuanza
kuwasafirisha abiria bure. Safari hiyo ilianzia maeneo yaliyokuwa na tatizo la usafiri Kimara, Mbezi kutokea Ubungo
na safari nyingine ilitokea Mwenge kuelekea Ubungo.
Mox aliamua kufanya hivyo kwa lengo la kuwasaidia abiria hao waweze kuwahi shughuli zao mbalimbali.

Hili ndio basi kampuni ya UDA lililokodiwa na msanii Mox kuwasafirisha abiria.

It's friday and the party is on, join the legends tonight @ isumba lounge with Dj JD, Dj Fast Eddy and Dj Y Kelvin. Entry 10k, doors open 9pm, mjulishe na mwenzako.


<

Wafanyakazi wa Benki ya NBC watembelea kituo cha watoto yatima na kuwakabidhi misaada


Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni, wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia Orphanage cha Sinza
walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya
NBC kurudisha sehemu ya faida
waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika
kituoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Wengine ni watumishi wa kituo hicho.

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma
wa Benki ya NBC Tanzania, Cornie Loots
(kulia) akikabidhi msaada wa vyakula,
mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua
kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima
cha Ijango Zaidia Orphanage , Bi. Zaidia
Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC
kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

Mtoto anayelelewa katika kituo cha
watoto yatima cha Ijango Zaidia
Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea
mafuta ya ngozi kwa niaba ya wenzake
vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC
kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo,
Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni
hapo, Sinza, jijini Dar es Salaam. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua.

Mfanyakazi wa Benki ya NBC,
Mwanaisha Nassoro Ayosi (kulia)
akikakabidhi misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

Mtoto anayelelewa katika kituo cha
watoto yatima cha Ijango Zaidia
Orphanage, Amina Twahilu, akipokea
moja ya vyandarua kwa niaba ya
wenzake vilivyotolewa msaada na Benki
ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki
hiyo, Anyelwisye Enock Mwakatobe
(kulia) kituoni hapo, Sinza, Dar es
Salaam juzi. Benki hiyo ilikabidhi
msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia
na sabuni.
Chanzo michuzi blog

Naibu mkuu wa Mji akagua mradi wa maji walaya ya Rombo


Naibu waziri wa maji Dk Binilith
Mahenge akikagua miradi ya maji katika wilaya ya Rombo.

Mhandisi wa maji wilaya ya Rombo
Andrew Tesha akitoa maelezo kwa
naibu waziri wa maji Dk Binilith
Mahenge alipotembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo.

Naibu waziri wa maji Dk Mahenge akikagua mradi wa maji
wa kilichopo eneo la hifadhi ya mlima Kilimanjaro(KINAPA).

Habari na Picha Na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii Moshi.


WIZARA ya maji,imeelezea
kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa
kampuni ya usambazaji maji wilayani
Rombo ya Kiliwater kwamba
haijajipanga kibiashara na ingeweza
kupata faida kubwa kuliko hali
waliyonayo sasa kama wangekuwa
makini.
Naibu waziri wa maji Dk Binillith
Mahenge alitoa kauli hiyo baada ya
kupokea taarifa ya kampuni hiyo kuhusu
usambazaji wa huduma za maji na
mipango yao katika ununuzi wa mita
kwa ajili ya kuwafungia wateja wao.
“Kwa mipango hii mliyonayo kama
kampuni hii ingekuwa imekabidhiwa
mfanyabiashara yeyote
makini,angeshindwa kupata faida?”
alihoji huku mwenyekiti wa bodi ya
kampuni hiyo, Silayo akikiri kwamba
faida ingepatikana.
Aliitaka kampuni hiyo kujipanga upya
kwani wanayo fursa ya kupata faida
kama wakijitahidi kupunguza maji
yanayopotea lakini pia kuhakikisha
wanaondokana na mfumo wa ulipaji
anka kwa ‘Flat rate’ bali wawafungie
wateja mita za maji.
“Huu mfumo wenu wa watu wote kulipa
maji kwa viwango sawa unawapotezea
mapato, wapo wanaoyatumia kwa ajili
kumwagilia migomba kasha watalipa sh
3,000 kwa mwezi, ninyi mnaona hilo ni
sahihi,badilikeni”alisema.
Katika baarifa yake kwa naibu waziri
meneja wa Kiliwater, Prosper Kessy
alisema uzalishaji wanakabiliwa na
uzalishaji mdogo wa maji usiokidhi
mahitaji kwani upo upungufu wa mita
za ujazo 13,000 sawa na lita 13,000,000
kwa siku.
Alisema pia wanakabiliwa nupungufu
wa mita za ujazo 22,000 sawa na litaza
ujazo 22,000,000 wakati wa kiangazi na
hivyo kuongeza tatizo la maji kwa
wateja wake.
“Kiwango kikubwa cha asilimia 78 ya
maji yasiyouzwa kutokana na uchakavu
wa miundombinu,wazi wa maji,wateja
wasio na mita na wale wenye mita lakini
hutumia maji kiholela”alisema.
Hata hivyo alisema kampuni hiyo
inahitaji zaidi y ash milioni 600 kwa
ajili ya kuwafungia mita wateja wake
kama njia moja wapo ya kuongeza
mapato

Jumuia ya kuhifadhi Qur'an Tukufu Tanzania na Tanzania Muslim Hajj Trust inawakaribisha waislam wote katika mashindano ya kuhifadhi Qur'an tukufu ya kimataifa


FAINALI KWA WASICHANA
Jumamosi , Tarehe 03 Agosti 2013,
Saa 3:00 ASUBUHI
Ukumbi: Star Light Hotel Hall
(Waalikwa Wanawake tu).
FAINALI KWA WANAUME
Jumapili , Tarehe 04 Agosti 2013,
Saa 3:00 ASUBUHI
Ukumbi:Diamond Jubilee Hall
(Waalikwa Wanaume na Wanawake).
Changia kuendeleza kuhifadhisha
QUR’AN Tukufu Tanzania kupitia
Mtandao wetu www.quran.or.tz
Tunawashukuru na kuwatakia Funga
Njema yenye Baraka na kukubaliwa Dua
zetu ambazo tunazo ziomba , Amiin .
Karibuni Sana Tutafurahi sana kama
Wadau wa Blog ya Jamii mkiongozwa na
kaka Michuzi na Timu yako kuhudhuria
kwenu .
Kwa Niaba ya Kamati ya Maandalizi.
Ghalib Nassor Monero l Azhary

Sunday, July 28, 2013

Dogo janja aachia track mpya


Mkono mkali toka studio za Noizmekah Arachuga,Janjaro anarudi round nyingine kwa style ya tofauti sana inayoitwa "serebuka".
Katika tasnia hii ya muziki utapomtaja msanii Dogo janja moja kwa moja utapata hisia ya ladha tofauti kutoka na ubunifu wa msanii huyo ambae ni ndogo sana kiumri,
Wimbo huo wa serebuka ambao ni special kwa fans wote wa Dogo janja "JANJARO" amesha utambulisha kupitia baadhi ya vituo vya redio na inaaminika ni moja ya wimbo utaotambulisha ujio mpya wa Janjaro.

Mtuhumiwa wa wizi anusurika kufa kwa kipigo cha wananchi


Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa watu wenye hasira.
MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-
Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam.
Mtu huyo ambaye jina lake halikueza kupatikana mara moja inadaiwa
alikutwa akiruka geti kuingia ndani
kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya
matukio wakati mtuhumiwa huyo
alipokuwa akipata kichapo hicho.

Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi hao wenye hasira.

Mtuhumiwa wa wizi akiomba
kusamehewa wakati mtu mwenye hasira akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo

Lakini kutokana na kipigo akaanguka
hadi hatua iliyofanya watu hao wenye
hasira kutawanyika eneo la tukio,
wakidhani mtuhumiwa amekufa. PICHA
ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
Chanzo michuzi blog.

Berry Black atoa track mpya ft Ali Kiba - Ishara

Cindy Rulz atoa brand new hit



posted from [Bloggeroid https://market.android.com/details?id=pl.przemelek.

Ssen Lubi na Sir Tino ft Vumilia - Penzi la super star the brand new track


Muungano wa wasanii wakali wa muziki wa
kizazi kipya bongo fleva Ssen Lubi na Sir Tino
wameachia single ya mpya walioipa jina la Penzi la super star.
Single hiyo ambayo imekuwa gumzo mitaani baada ya kusikika katika vituo mbalimbali vya redio wamemshirikisha mwanadada Vumila.
Wimbo huo umetengenezwa studio za Seductive chini ya producer MT. T Touch umekubalika sana na mashabiki kutokana na jinsi ya upangiliaji mzuri na maudhui ya wimbo huo.
Ssen na Sir Tino wanaomba sapoti kutoka kwa mashabiki zaidi pamoja na wadau wa muziki ili kuendelea kukuza muziki wa Tanzania.
Kwa mawasiliano unaweza kuwasiliana nao SSEN ni 0719 208 090 na Sir Tino : 0713 621 454.
posted from Bloggeroid

My Blog Name
My Blog Name

Arusha haitawaliki, wahuni kuchimba kaburi la mafisadi


Nikile kinacho sadikika au kufahamika kuwa gumzo kubwa mitaa ya Arusha ni mixtape ijayo ya KABURI LA FISADI linalochimbwa na rapa mhuni na wahuni wote kwa asilimia kubwa

Arusha linazidi kushika kasi baada ya Rapa machachari KAPUKU DIGITAL kuachia track kali kila anapo ibuka kutoka vichochoroni inasadikika kuwa anaweza kua rapa ambaye ataongeza nguvu kwenye mziki wa Arusha.

Nyimbo za msanii huyu zimekua gumzo baada ya kuonyesha umahiri wake wa kucheza na beats za zamani ambazo huwakumbusha wapenzi wa hip hop enzi zile za hip hop ya kweli.

Kapuku digital alianza kwa kuachia nyimbo ya kwanza ya mixtape inayoitwa Mapinduzi na kisha leo hii kaachia nyimbo mbili kali na intro ya mixtape “A town haitawaliki” na “Kaburi la fisadi” kama nyimbo iliyobeba jina la mixtape hiyo.

Kapuku kasema mixtape imesha kamilika ila itaachiwa rasmi January 2014 na ameidedicate kwa Mwl nyerere kama raisi wa kuigwa ,ameidedicate pia kwa Sokoine kwakua waziri mkuu wa kuigwa na kwa king of da kings hip hop legendary Faza nelly kama msanii wa kuigwa Arusha.maskini wote wakae mkao wa kwenda msibani.
posted from Bloggeroid


My Blog Name

Thursday, July 25, 2013

Pamoja Nite

Pamoja Nite is a get together reggae event, intended to showcase the best reggae DJs, quality sounds and interactive atmosphere. The event aims to gather the youths and everyone who accepts the invitation to come and enjoy quality entertaining moment. The night will also feature the display of handmade crafts which has always blended well with the theme of reggae as a way of networking and acknowledging efforts of our local artists. The event is scheduled to take place on 16 th August, 2013 at New Msasani Club from 9pm TILL DOWN!!!!!,


Published with Blogger-droid v2.0.10

Mwambie mwenzie

SOUND CLOUD LINK HERE....https://soundcloud.com/tiddy-hotter/stamina-ft-darasa-warda


*DETAILS*

*TRACK NAME: Mwambie Mwenzio


ARTIST NAME: Stamina Ft Darasa & Warda


COMPOSED BY Stamina


PRODUCER: TIDDY HOTTER


STUDIO: ONE LOVE FX


*CONTACTS*

+255 656 48 77 48 +255 712 56 02 01/ +255 754 44 06 11


Published with Blogger-droid v2.0.10

Zed Mill "Naita majina"

Msanii Chipukizi toka Tabora,ZedMill mbaye kwa sasa yupo jijini Arusha kimasomo adrop ngoma yake "Neaita Majina" download HAPA usikilize uwezo wa kijana huyo. Powered by www.vmgafrica.com


Published with Blogger-droid v2.0.10

Frank memoiri & Maychedda "Nimejitoa sadaka"

Ikiwa ni muda kidogo tangu

kutoa Single,Rapper Frank Memori aja tena

akishirikiana na mwanadada MayC aka

Maychedda katika ngoma brand new

"Nimejitoa Sadaka" ilopikwa katika studio za

noizmekah arusha chini ya Producer defxtro,

pata kudownload wimbo HAPA na endelea

kusupport muziki wa Tanzania


Published with Blogger-droid v2.0.10

Mmilili wa Home Shopping Center akiwa hospitalini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali

Mfanyabiashara maarufu na Mmiliki wa
maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said
Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita
alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City
Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika
Kusini kwa matibabu zaidi
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni,
mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na
mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara
baada ya kutenda tukio hilo, mhusika
alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu
kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya
kuteleza na kuanguka.
Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa
kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri
aina ya pikipiki.
Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa
anaweza kuzungumza japo amefungwa
mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia
kupumua.
Matukio ya watu kumwagiwa tindikali
yameonekana kushamiri nchini katika siku za
hivi karibuni.
Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa
Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni
takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma
Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa
kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni
tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani
kwake.
Chanzo kingjofa.blogspot.com

Published with Blogger-droid v2.0.10

Maadhimisho ya siku ya mashujaa mkoani Morogoro

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu
ya Mashujaa iliyofanyika leo Mkoani
Morogoro.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Swahili Tv mtaani

Na Alex Kassuwi
Kwa wanakijiji wenzangu, miaka 30
iliyopita nisingeliweza kuamini ninayo
yaona na kuishi hivi sasa. Kwa kifupi
tuliona wakija kijijini kama mapadri,
wataalamu wa mashirika toka nje ama
walimu.
Nilijenga imani kila mzungu ni msomi
na tajiri. Nilipohamia ughaibuni
nimekuta ni tofauti sana, wapo wazungu
wengi mbumbumbu na wanabangaiza tu.
Ushauri kwa dada zangu wanaowinda
kuolewa na wazungu "kila king'aacho
sio dhahabu"

Published with Blogger-droid v2.0.10

Bad Q ft Jambo squad & Breeze "Huna hela"

Msanii Bad Q toka G.A-Unit arachuga ameachia wimbo wake alomshirikisha Breeze toka kundi la Machizi flani pamoja na Ordinary toka Jambo Squad "Huna Hela"
Kwa kuisikiliza na kudownload wimbo huo bofya HAPA endelea kutoa support muziki wa Tanzania usonge mbali zaidi.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Msanii chipukizi El Jons "Ukweli wangu"

Anaitwa El Jons, msanii chipukizi anayeishi Jijini Arusha. ameachia wimbo wake alioupa jina la "ukweli wangu" download HAPA ,powered by www.vmgafrica.com ------------------------------http://www.hulkshare.com/dl/4qhf6lnia88w/El%20jons-ukweli%20wangu%20(noiz)?d=1

Published with Blogger-droid v2.0.10

Washindi wa Tuzo za Wimbo bora wa reggae

Washindi wa Tuzo za Wimbo bora wa reggae katika Kilimanjaro Music Awards, Warriors from the East wanakuja na nyimbo mpya kabisa "Bongo Reggae" ikiwa ni single ya kwanza kabisa itakayopatikana katika album ya "Bongo Reggae" Pata kudownload HAPA na endelea kusupport muziki wa Tanzania. powered by www.vmgafrica.com -----------------http://www.hulkshare.com/dl/ah5icrgr7oxs/Warriors%20from%20the%20east-bongo%20reggae%20(noiz)?d=1

Published with Blogger-droid v2.0.10

Finca wajibebea chao baada ya mkopaji wao kushindwa kulipa deni

Taasisi inayojihusisha na mikopo kwa wajasiliamali FINCA leo wameibuka dukani kwa Mr Mmasi Barabara ya 13 na kubeba kila kitu kilichokuwepo dukani hapo baada mteja wao huyo kushindwa kulipa deni. Bwana Mmasi ambae anafanya biashara ya nguo dukani hapo amefikwa na hali hiyo kutokana na hali ya kushindwa kutimiza masharti ya mkopo wake. Finca Imefikia hatua ya kuchukua bidhaa hizo zilizokuwepo dukani hapo ikiwemo nguo pamoja na meza baada ya kumpatia muda wa kutosha bwana Mmasi katika kulikamilisha deni hilo

Published with Blogger-droid v2.0.10

Ajali pikipiki na baskeli Barabara ya 13 Tanga jioni hii

Mtoto mwenye kanzu agongwa na pikipiki Barabara ya 13, picha inawaonyesha wote wakiwa wameinuka baada ya ajali hiyo hakuna aliyeumia katka ajali hiyo.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Man Tuzo aachia ngoma mpya "Mwambie atulie"

Ngoma mpya ya Man tuzzo msanii toka Mtwara ambae ameamua kuleta mapinduzi kwenye muziki wa bongo fleva.

Man tuzo ni kijana mwenye uwezo mkubwa kwenye tasnia ya music wa kizazi kipya ambae kwa sasa makazi yake yapo Zanzibar kutokana na shughuli zake za kikazi, "Mwambie atulie" ndio ngoma yake mpya alioiachia hivi karibuni toka Island records Zanzibar, Laza'k na Labizo ndio producer walio simamia ngoma hiyo.

Kwa mawasiliano ya interview au show wasiliana nae kwa namba yake ya simu ya mkononi 0718387925 Au 0682457001.

Endelea kusapoti muziki wa Tanzania.
Bofya hapa kusikiliza na kudownload..

Song; Mwambie atulie Artst: Man Tuzzo Studio: Island Records Zanzibar Producer: Raza'k & Lab One

Published with Blogger-droid v2.0.10

Tuesday, July 23, 2013

Afariki dunia papo hapo kwa kugongwa na daladala jijini Dar.

Mkazi wa Dar es Salaam ambaye jina lake
halikuweza kupatikana mara moja leo
amefikwa na umauti baada ya kugongwa
na gari aina ya Nissan ambalo linafanya
shughuli za kubeba abiria kati ya Gongo la
Mboto na Kariakoo jijini Dar es Salaam
namba za usajili T 288 AZB na namba ya
njia ni S 264D.
Kwa mujibu wa mashuhuda wameiambia
Father Kidevu Blog kuwa, marehemu
aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka
barabara ya Nyerere eneo la Mtava karibu
na Quality Centre leo asubuhi.
Endelea hapa

Published with Blogger-droid v2.0.10