Sunday, July 28, 2013

Arusha haitawaliki, wahuni kuchimba kaburi la mafisadi


Nikile kinacho sadikika au kufahamika kuwa gumzo kubwa mitaa ya Arusha ni mixtape ijayo ya KABURI LA FISADI linalochimbwa na rapa mhuni na wahuni wote kwa asilimia kubwa

Arusha linazidi kushika kasi baada ya Rapa machachari KAPUKU DIGITAL kuachia track kali kila anapo ibuka kutoka vichochoroni inasadikika kuwa anaweza kua rapa ambaye ataongeza nguvu kwenye mziki wa Arusha.

Nyimbo za msanii huyu zimekua gumzo baada ya kuonyesha umahiri wake wa kucheza na beats za zamani ambazo huwakumbusha wapenzi wa hip hop enzi zile za hip hop ya kweli.

Kapuku digital alianza kwa kuachia nyimbo ya kwanza ya mixtape inayoitwa Mapinduzi na kisha leo hii kaachia nyimbo mbili kali na intro ya mixtape “A town haitawaliki” na “Kaburi la fisadi” kama nyimbo iliyobeba jina la mixtape hiyo.

Kapuku kasema mixtape imesha kamilika ila itaachiwa rasmi January 2014 na ameidedicate kwa Mwl nyerere kama raisi wa kuigwa ,ameidedicate pia kwa Sokoine kwakua waziri mkuu wa kuigwa na kwa king of da kings hip hop legendary Faza nelly kama msanii wa kuigwa Arusha.maskini wote wakae mkao wa kwenda msibani.
posted from Bloggeroid


My Blog Name

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments