Mfanyabiashara maarufu na Mmiliki wa
maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said
Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita
alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City
Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika
Kusini kwa matibabu zaidi
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni,
mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na
mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara
baada ya kutenda tukio hilo, mhusika
alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu
kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya
kuteleza na kuanguka.
Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa
kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri
aina ya pikipiki.
Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa
anaweza kuzungumza japo amefungwa
mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia
kupumua.
Matukio ya watu kumwagiwa tindikali
yameonekana kushamiri nchini katika siku za
hivi karibuni.
Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa
Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni
takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma
Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa
kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni
tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani
kwake.
Chanzo kingjofa.blogspot.com
Thursday, July 25, 2013
Mmilili wa Home Shopping Center akiwa hospitalini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali
Published with Blogger-droid v2.0.10
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments