Sunday, July 14, 2013

Sheikh mkuu wa wilaya ya Arumeru Said Juma Makamba amwagiwa tindikali

Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said
Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa
kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku
akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.
Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye
Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount
Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya
usoni, kifuani na mgongoni huku
akiendelea na matibabu.
Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa
kuamkia jana nyumbani kwake kwa
Mromboo Arusha, wakati akijiandaa
kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya
Tarawei.
Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu
wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha,
alisema baada ya swala hiyo alirejea
nyumbani kwake akisindikizwa na vijana
wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja
na kuingia ndani ya nyumba yake ili
kulala.
Alisema hata hivyo, kabla ya kulala
alikwenda kujisaidia katika choo cha nje
na kwamba wakati akirudi ili aingie
ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla
alimuona mtu akiwa amesimama jirani na
mlango.
Chanzo Juma Mtanda

Published with Blogger-droid v2.0.10

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments