Msanii anayewakilisha kundi la WATEULE MCHIZI MOXIE jana majira ya mchana aliamua kujitolea kukodi gari la abiria kampuni ya UDA kwa muda wa masaa manne na kuanza
kuwasafirisha abiria bure. Safari hiyo ilianzia maeneo yaliyokuwa na tatizo la usafiri Kimara, Mbezi kutokea Ubungo
na safari nyingine ilitokea Mwenge kuelekea Ubungo.
Mox aliamua kufanya hivyo kwa lengo la kuwasaidia abiria hao waweze kuwahi shughuli zao mbalimbali.
Hili ndio basi kampuni ya UDA lililokodiwa na msanii Mox kuwasafirisha abiria.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments