Tuesday, July 31, 2012
USAFIRI WA ASILI YA UNGUJA NA PEMBA
Katika hali ya ubunifu huu ndio usafiri unaopendwa na wazawa wa Zanzibar na kuwa ni kivutio kwa wageni husuana watalii, ni gari la kawaida ila linabadilishwa muundo wa bodi lake orijino na kuweka bodi la asili kwa kutumia mbao na mabati kwa ajili ya kufunikia juu.
Monday, July 30, 2012
Friday, July 27, 2012
PACKING YA MAGARI UWANJA WA NDEGE WA ZANZIBAR (AMANI INTER. AIRPORT) VUMBI TUPUUUU..
Hii ni njia ya kuingilia sehemu ya kusimamishia magari ya watu wanaokwenda kupokea wageni wao
Parking ya magari ya aina zote
Hili ndio eneo maalum la kusimamishia magari ya watu wanaokwenda kupokea wageni wao uwanja wa ndege wa Zanzibar (Amani International Air Port).Endapo utakuwa umesimama eneo hili omba mungu kusije upepo mkali wa kunimua vumbi na endapo utakutana na upepo dakika kadhaa unapotezana na ndugu yako.
Habari isio rasmi kuna jamaa alienda kumpokea mpenzi wake alikuwa akitokea Uingereza alipotua uwanja wa ndege wa Zanzibar alikuwa amependeza sana alipokelewa na mpenzi wake vizuri wakakumbatiana sana kwa furaha, baada ya hapo walielekea liliko gari ambako ndio kama unavyoona kwenye picha hali ilivyo.
Basi baada ya kufika karibu na gari kulikuwa na watu wengi wametoka kupokea ndugu zao nao walikuwa wakijiandaa kuingia kwenye magari yao, hii ni june july upepo ni mkali wa kunimua vumbi ghafla ulipiga upepo ambao ulinimuwa vumbi kiasi cha kutoonana kama dakika 3 ulipokata ule upepokata kila mmoja alikuwa hamtambui mwenzie kwa jinsi sura zao zilivyokuwa kama vinyago yule mwanamke alipoambiwa na mpenzi wake ingia kwenye gari twende akamjibu kwani wewe ndio niliyekufuata akasisitiza kwani wewe ndio uliyekuja kunipokea we vipi embu achana na mimi hee jamaa alijua masihara kumbe mpenzi wake kamshau kwa jinsi alivyojaa vumbi na kuwa kama kinyago.
Serikali wananchi wanataka ile packing iwe saafi safi hata kama ni ya muda.
Thursday, July 26, 2012
MAMBO YA RAMADHANI HAYOOO
Mariam Hamza mtoto wa pili wa bi Hamida Maalim alipokuja kutembelea Coconut Fm leo
Mariam
Hamida Maalim kulia na Mama wa mitaani Aisha Omary kushoto wakibadidlishana mawazo kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wednesday, July 25, 2012
DAKU FREESH....MATARANGE RESTAURANT
Mdau wa Zee Town Lazaro Matarange akiwa katika pozi
Baga, Sambusa, Badia, Kachori, Maandazi, Ndizi, Chipsi na kuku saaaafi
Mdau wa Zee town Lazaro Matarange akiwa ofisini kwake
Mishkaki bomba ya nyama
Hii ndio sehemu wanayojivunia wakazi wa Chukwani kwa kujipatia daku mida ya usiku MATARANGE RESTAURANT ipo karibu na High View School.
SHABANI BILALI AKIPERUZI MAGAZETI YA LEO
Kusoma magazeti kunasaidia kusogeza masaa mbele endapo swaumu imepanda, hapa bwana Metaya Shotgun kama anakazia ivi kwa kupitia habari mbalimbali kwenye gazeti.
Sunday, July 22, 2012
UTAMUA WA RAMADHANI HUOOO
Vyakula vya mwezi mtukufu
Matunda aina ya shokishoki na dorian
Matunda na vyakula kupanda bei mwezi wa mtukufu wa Ramadhani imekuwa ni kawaida nani alaumiwe mfanyabiashara au mkulima?
Friday, July 20, 2012
KITAANI KIMENUKA
Kitaani kimenuka
Hii ndi hali ya mjini Zanzibara jioni ya leo
Chanzo cha hali hii inadaiwa kuwa ni muamsho
SERIKALI YA MUUNGANO WA TANZANIA YAAHIDI KOTOA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFUATIA AJALI YA MELI YA MV SKAGIT
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema akitoa Taafifa ya uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo Ofiosini Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozio Seif Ali Iddi akizungumza na Wabunge wa Muungano waliofika Zanzibar Kutoa mkono wa pole hapo katika ukumbi wa Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Mbweni kufuatia Ajali ya Meli ya M.V. Skagit.
Ujumbe huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji baadhi ya Watalii na wageni waliokuwa wakija Zanzibar kwa Meli ya M.V. Skagit iliyopata ajali juzi mchana karibu na Kisiwa cha Chumbe. Kulia ya Balozi ni Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Mh. Hamad Masoud Hamad.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua baadhi ya majeruhi wa M.V Skagit waliolazwa katika Hospiotali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Ali Abdulla Ali akiwa na Makatibu wake wakitoka nje ya Ukumbi wa Baraza hilo baada ya kuahirisha kwa siku moja kikao cha baraza la Wawaklilishi jana asubuhi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia msiba uliolikumba Taifa baada ya ajali ya Meli ya M.V Skagit iliyozama karibu na kisiwa cha Chumbe.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha alitoa kauli hiyo wakati akitoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mh. Nahodha akiuongoza Ujumbe wa Wabunge 20 wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa mkono huo wa pole alisema Vikosi vya Ulinzi mbali ya kusaidia operesheni hiyo pia litaendelea kuto msaada wowote utaohitajika katika kurejesha hali ya kawaida kwa wahanga hao wa ajali ya Meli.
Mh. Nahodha alisema maafa yaliyotokea jana yameigusa Jamii yote ya Watanzania hivyo Wananchi wote wanapaswa kuzidisha juhudi zao katika harakati zote za kurejesha hali ya utulivu na Amani.
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru ujumbe wa Wabunge hao kwa kuguswa kwao na msiba huo uliopelekea vifo vya Watu 53 hadi sasa.
Balozi Seif alisema wazamiaji pamoja na Vikosi vya Ulinzi bado wanaendelea na operesheni ya kuwatafuta Abiria waliopotea kwenye chombo hicho.
Alisema Serikali imechukuwa gharama za mazishi kwa Mazishi ya wale wote waliokufa katika ajali hiyo sambamba na kuhudumia usafiri wa maiti ambazo Familia zao ziko Tanzania Bara.
“ Hatupendi Meli zetu zizame lakini zinazama. Hatupendi Ndege zetu zianguke lakini zinaanguka. Hiyo ni kudra ya Mwenyezi Muungu”. Alisisitiza Balozi Seif.
Hata hivyo Balozi Seif alieleza kwamba bado ipo tabia ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri wa Baharini kusaidia kufuata taratibu za usafiri zilizowekwa na mamlaka husika badala ya kutawaliwa zaidi na Tamaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata fursa za kutembelea majeruhi wa ajali hiyo wanaoendelea kupatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Balozi Seif alielezwa kwamba jumla ya majeruhi 80 waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo wamesharuhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata tiba.
Mmoja wa Majeruhi hao ambae ni mfanyabiashara Kitwana Makame Ali ameipongeza Serikali na Vikosi vya ulinzi kwa juhudi zao za uokozi zilizopelekea wengi kati ya wahanga hao kuokolewa.
Hata hivyo Mfanyabiashara Kitwana ameishauri Serikali kuhakikisha sheria na taratibu za usafiri wa Baharini zinazingatiwa kwa lengo la kuepusha ajali.
Baadaye Balozi Seif aliwakagua Wageni na Watalii waliookolewa ambao walikuwa wakisafiri na chombo hicho hapo katika Hoteli ya Serrena Inn Shangani Mjini Zanzibar.
Wageni hao 14 ni Paul Smeulders kutoka, Eline Van Nistelrooy, Jaap Van Der Heyden, Joa Maouche, Inge Van Herwynen kutoka Uholanzi, Lauren Dent na Hilary Strasburg kutoka Marekani, Arne Sohns kutoka Ujerumani, Joas Gielen na Elvira Feyen kutoka Ubelgiji.
Wengine ni Bastiar Var Rennings,Lena Roker kutoka Ujerumani Chen Dagan na Nitzan Bodenheimer kutoka Nchini Israel.
Akiwa Ofisini kwake Vuga Balozi Seif alikutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Ispekta General Said Mwema kupokea Taarifa ya jeshi hilo tokea mwanzo wa harakati za uokozi wa janga hilo.
IGP Said mwema alimueleza Balozi Seif kwamba Jeshi la Polisi tayari limeanza uchunguzi wa awali na hitilafu kadhaa zimejichomoza kutokana na idadi halisi ya abiria waliokuwemo kwenye Meli hiyo.
Alisema mahojiano ya watu mbali mbali wakiwemo baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye chombo hicho pamoja na wahusika wa chombo chenyewe Mjini Dar es salaam yanaendelea vyema.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal amefanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mazungumzo hayo yalikuwa katika jitihada za kutoa mkono wa pole pamoja na kutafuta mbinu za namna gani Serikali zote mbili zitaendelea kushirikiana katika kukabiliana na Maafa hayo.
Dr. Bilal ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana vyema na vikosi vyote vya Ulinzi kwa jitihada zao za haraka zilizopelekea kuokoa idadi kubwa ya abiria waliokuwemo kwenye vyombo hivyo.
Dr. Bilal alimueleza Balozi Seif kwamba Serikali zote mbili ziendelee kutoa Msukumo wa msaada wa ziada kwa mamlaka zote mbili za Usafiri wa Baharini { SUMATRA na ZMA } ili kuona uimara na ukaguzi wa vyombo vya Baharini unazingatiwa vyema.
Taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imefafanua na kuthibitisha kwamba Meli hiyo ya M.V Skagit imeruhusiwa kuchukuwa abiria 250 tuu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/7/2012.
Picha na Saleh Masoud Mahmoud – OMPR-ZNZ.
Serikali ya Muungano wa Tanzania Kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa litaendelea kutoa ushirikiano na msaada kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit iliyotokea jana mchana karibu na Kisiwa cha Chumbe.

WATANGAZAJI WA COCONUT FM WAKITAKIANA RAMADHANI KAREEM
Meneja wa Coconut Fm ambae pia ni mtangazaji wa kipindi cha Nipe Nikupe akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kuzungumza na watangazaji wake.
Juu na chini ni picha ya pamoja ya watangazaji wa Coconut fm
Coconut fm yajipanga kufanya vipindi vizuru vitakavyoendana na mwezi
mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni siku chache zimebaki kuweza kuupokea mwezi
huo mtukufu.Meneja wa Coconut Fm Husna Abdul Megeni wa Bahari alisema "Coconut fm ni redio inayomhudumia vizuri mzanzibari katika kupata taarifa muhimu za ndani na nje na kwa upande wa burudani pia hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kumpatia huduma nzuri zaidi kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani" aliyaesema hayo jana alipokuwa akizungumza na watangazaji wa Coconut fm na kusisitiza kuwa vipindi vimepangwa vizuri kulingana na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Pia amewataka wasikilizaji wa Coconut fm kuendelea kusikiliza vipindi vizuri vilivyondaliwa kwa ajili ya mwezi mtukufu na kuwahakikishia kuendelea kutoa huduma bora itayokidhi haja yake kwa kipindi chote.
Kwa upande wa wafanyakazi na waendeshaji wa vipindi wamesema wamefurahishwa sana na mpangilio wa vipindi walioupanga kwa ajili ya Ramadhani.
RAISI KIKWETE ATUA ZANZIBA KUTOA RAMBIRAMBI KWA WALIOPATA AJALI YA MELI
Rais Mrisho Jakaya Kikwete na mama Salma Kikwete wakipita kuwafariji majeruhi waliolazwa hospitali kuu mnazi mmoja ( hapa wanamsikiliza bw. Kitwana Makame Haji mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo)
Raisi Mrisho Jakaya Kikwete na Raisi Dr Ali Mohamed Shein wakipita kutazama maiti za waliokufa kwenye ajali ya meli
Thursday, July 19, 2012
SHUGHULI ZA UOKOAJI ZINAENDELEA ...WATU WAENDELEA KUSUBIRIA MAITI ZINAZOENDELEA KUPELEKWA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA
Watu wakiendelea kusubiria kutazama maiti zainazoendelea kuletwa
Watu wakiwa kwenye mstari wakiingia sehemu ilipohifadhiwa maiti kwa ajili ya kutambua ndugu zao
Vikosi vya maafa wakishusha miili iliyopatikana leo
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa mchana wa leo katika viwanja vya maisara watu ni wengi wakiendelea kusubiria maiti zinazopelekwa hapo kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu zao.
Mpaka kufikia asubuhi ya leo maiti 30 zilipatikana ambapo kati ya hizo 20 zimetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao na watu 145 wameokolewa wakiwa hai hii ni kwa taarifa kutoka mamlaka ya serikali.
Wakati shughuli za uokoaji zinaendelea leo mpaka kufikia jioni hii maiti 30 zimepatikana na kupelekwa katika viwanja vya maisara ambapo watu bado wanaendelea kupita kutambua ndugu zao.
TAARIFA YA RAIS KIKWETE KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT
TAARIFA
YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE 18
JULAI, 2012, CHUMBE, ZANZIBAR
Jana
tarehe 18 Julai, 2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya
MV SKAGIT katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es
Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250,
watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.
Amiri
Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na
usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na Polisi waanze kazi ya uokoaji
mara moja.
Kazi
hiyo imefanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na meli za makampuni binafsi. Mpaka giza lilipokuwa limeingia na hivyo
kazi ya uokoaji kusitishwa mpaka kutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012, watu 136
walikuwa wameokolewa na maiti 31 zilikuwa zimepatikana. Aidha, mali zilizokuwa
kwenye meli hiyo hazikuweza kuokolewa.
Kufuatia
ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein,
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa vifo na majeraha waliyopata Watanzania
wenzetu na watu wasiokuwa raia wa Tanzania. Alimuomba afikishe salamu za
rambirambi kwa ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata
majeraha na maumivu maungoni mwao.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao
ni majonzi yake na ya Watanzania wote. Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea
kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na
shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wote wa ngazi mbalimbali
kwa uongozi wao thabiti tangu taarifa ya kutokea kwa ajali mpaka
sasa.
Aidha,
amewapongeza maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa
meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa
na maafa haya makubwa na ya aina yake. Amewataka waendeleze juhudi hizo leo na
siku zijazo.
Rais
amewataka wananchi wawe na moyo wa subira na uvumilivu wakati kazi ya uokoaji
inaendelea. Kama ilivyofanyika katika ajali ya MV Spice Islander miezi 10
iliyopita, uchunguzi wa kina utafanyika kubaini chanzo cha ajali.
Kutokana
na ajali hiyo na msiba huu mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza maombolezo ya taifa ya siku
tatu ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo, tarehe 19 Julai,
2012.
Asanteni
sana.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
19
Julai, 2012
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yatangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali ya meli ya Mv. Skagit
Na
Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi
Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit iliyozama karibu na
Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein
akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na
kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za
maombolezo.
Dk.
Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake
aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dk Shein amewahakikishia
wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za
mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.
“Nimesikitishwa
sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu
hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dk. Shein.
Mbali
ya taarifa hiyo, Rais Dk Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali,
vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika
eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.
Mbali
ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar
kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana
lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya
bajeti yake.
Baadhi
ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Shamsi Vuai
Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa
ajili ya utambuzi.
Mbali
ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli
zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli
za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo
kuwafariji waliopoteza ndugu zao.
Taarifa
kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30
zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku
wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la
Maisara.
Aidha,
katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali
nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Meli
ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es
Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na
mabaharia 6.
Kazi
ya utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika eneo la tukio ilikozama
meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha
Chumbe Zanzibar.
TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN, KUHUSU AJALI YA MELI YA MV SKAGIT YA KAMPUNI YA SEAGUL JULAI 18, 2012
BISMILLAH RAHMAN RAHIM
Ndugu Wananchi,
ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH
Kwa
masikitiko makubwa leo Jumatano, Julai 18, 2012 nchi yetu imepata tukio
la huzuni kubwa la ajali ya kuzama meli ya mizigo na abiria ya MV
SKAGIT tukio ambalo limesababisha vifo, majeruhi na kupotea mali za
watu.
Ajali hiyo imetokea wakati meli hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuja Zanzibar. Taarifa za awali za MV SKAGIT ni kuwa meli hio ilikuwa na jumla ya watu 290. Kati ya hao wafanyakazi ni watu 9, abiria watu wazima ni 250 na watoto 31. Meli hiyo ilipata maafa hayo maeneo ya Kisiwa cha Chumbe milango ya saa nane mchana. Mara
baada ya taarifa ya ajali hiyo kutufikia, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ikishirikiana na taasisi mbali mbali zikiwemo Idara Maalum za
SMZ, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mamlaka ya Usafiri wa
Baharini pamoja na vyombo vya usafiri wa baharini vya watu binafsi na
wananchi kwa jumla ilichukua hatua za haraka kufika eneo hilo kwa kazi za uokozi.
Mpaka
saa za magharibi hivi leo, idadi ya watu waliookolewa 136 na maiti 31
wamepatikana, wakiwemo watu wazima 24 akiwemo raia wa kigeni mmoja na
watoto 7. Jumla ya watu 123 bado hawajaonekana. Juhudi za uokozi ziliendelea hadi kuingia giza na zitaendelea mara kukipambuzuka. Hali ya bahari ilikuwa mbaya wakati huo na meli hiyo ilipinduka katika mawimbi makubwa.
Ndugu Wananchi,
Tukio
hili ni msiba mkubwa kwa wananchi wote wa Zanzibar na taifa la Tanzania
kwa jumla. Ni wakati mgumu kwetu sote na napenda kutoa wito kwa watu
wote tuwe na subira na wastahamilivu. Huu ni wakati wa kufikiria ndugu na watoto wetu waliopoteza maisha yao na tuwatakie rehema za Mola wetu. Aidha, tunawaombee nafuu waliopata majeraha.
Kwa niaba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar natoa pole kwa wafiwa wote na namuomba Mwenyezi Mungu awape subira. Kwa
wale ambao bado hawajapata taarifa za watu wao waliokuwa katika safari
hiyo, nawaomba wawe wavumilivu wakati tunafanya juhudi zote za uokozi na
utafutaji miili ya waliofariki.
Vyombo
vya ulinzi na usalama na taasisi mbali mbali vitaendelea kuchukua kila
hatua inayofaa katika kazi hiyo. Natoa shukurani zangu na za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa wenye vyombo vya bahari binafsi
vilivyoshiriki katika kazi za uokozi na kuokota maiti na pia wananchi
wengine waliojitolea. Kadhalika, navishukuru vyombo vya habari kwa
kuendelea kuwaarifu wananchi tukio hili kila hatua. Ni matumaini yetu kwamba wataendelea kushirikiana na sisi katika kushughulikia tokeo hili.
Ndugu Wananchi,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itasimamia gharama zote za mazishi ya wale
waliofariki na pia itatoa huduma ya afya, matibabu na nyengine kwa wote
waliopata majeraha. Tutatangaza mipango yote kupitia vyombo vya habari na njia nyengine.
Kutokana na msiba huu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatangaza siku tatu za maombolezi kuanzia kesho tarehe 19 Julai, 2012. Katika kipindi hicho sherehe na tafrija zote zinazatakiwa kusitishwa. Bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Nawasihi wananchi kuwa huu si wakati wa kutupiana lawama au kueneza habari zisizothibitishwa. Sote tushirikiane na kusimama pamoja katika tukio hili la msiba na maafa. Tukubali kuwa msiba huu ni amri ya Mwenyezi Mungu na umeandikwa kuwa mtihani kwetu. Mola wetu anatuambia kuwa binadamu tutapewa mitihani ya kupoteza maisha na mali. Huu ni mtihani mmojawapo wa hiyo. Tumuombe Mwenyezi Mungu atupe subira.
Wednesday, July 18, 2012
HILI NI ENEO MAALUM LILILOANDALIWA KWA AJILI YA WATU KWENDA KUTAMBUA MIILI YA NDUGU ZAO
Sehemu ya kuhifadhia miili ya marehemu kwa ajili ya watu kwenda kuwatambua ndugu zao ikifanyiwa maandalizi katika viwanja vya maisara
Umati wa watu wakiwa pembezone mwa bahari maeneo ya maisara wakiangalia boat za uokoaji zikirejea bandarini
Askari wa kikosi cha KMKM wakishirikiana na kikosi cha msalaba mwekundu kuipanga miili ya marehemu sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya watu kupita kutambua miili ya ndugu zao
Baadhi ya miili ya marehemu iliyotangulia kuletwa eneo hili maalum kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu zao
Tulipokuwa katika viwanja vya maisara na waandishi wenzangu kutoka kushoto ni Lazaro Philipo Matarange, Hussein Hamis Mgonanze na Mbaraka Said Boha.
Mpaka muda tulioondoka katika eneo hili ilikuwa jumla ya maiti 7 zimewasilishwa, maiti 3 za watoto na maiti 4 za wakubwa wakiwemo wanawake 2 mmoja ni mzungu ambae ni mgeni alikuwa na wenzake saba wameokolewa na wanaume 2. Kwa upande wa watoto haikuweza kufahamika kwa haraka jinsia zao. Kwa upande wa majeruhi walikuwa 24 akiwemo mtoto 1.
Kwa taarifa zaidi sikiliza Coconut Fm kwa wewe ambaye unaishi Ungunja kwa uliye mbali endelea kufuatilia kpitia blogg hii. Pia naomba radhi kwa picha ambazo hazikustahili kuwekwa humu.
Subscribe to:
Posts (Atom)