Sifa ya dereva mzuri ni kuzijua sheria na alama za barabarani kama zinavyohitaji kitu ambacho ni lazima kwa dereva azijue na hii ndio hali iliyopelekea kuwe na vyuo maalum vya kufundisha udereva lakini katika hali halisi sio kila aendeshae gari amefuzu kuwa dereva.
Katika hali halisi ya maisha ya mwanadamu kuna mengi yanayoweza kutekea yakiwemo mazuri na mabaya pia kila mahala kuna taratibu zake kisheria lakini kuzifuata hizo taratibu vile ambavyo zinataka ndio mtihani kwa watu wengi sana, wakati mwingine unaweza kuwapa lawama watu kama hao wanaokwenda kinyume na taratibu zinavyotaka kumbe hawastahili lawama kwasababu bila ya kufanya hivyo basi sheria zitakuwa hazina kazi yoyote na pengine hazitakuwa na haja ya kuwepo.Watoto wa mjini wakwambia sheria zimewekwa ili zivunjwe ndipo zifanye kazi.
Gari unazoziona hapo zimesimama katika eneo lisiloruhusiwa kusimamisha magari hali iliyopelekea zipigwe loki na wasimamizi wanaohusika kuweka mji katika hali ya usalama.
Madereva muwe makini mnapokuwa barabarani hakikisha unafuata sheria na alama za barabarani kama zinavyohitaji isipelekee mtu ajiulize maswali juu ya udereva wako.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments