Dj dr b
Historia inaumuhimu mkubwa sana kwa vizazi
vipya na zamani na ndio maana kuna somo maalum mashuleni kupitia silabasi za elimu somo hilo linaloitwa Historia "History".
Historia ni somo ambalo linafundisha mambo ya kale na ukitaka kujua utamu wa somo la historia upate muda wa kutembelea sehemu mbalimbali za makumbusho kwa lengo la kujifunza kwa vitendo isiwe historia unayosoma darasani ukaona inajitosheleza tembea uone kama hivi.

Kama
nilivyosema historia ni somo muhimu sana na linafaida nyingi ila kubwa ni kumpa mtu nafasi ya
kujua yakale, yasasa na hata yajayo hali inayomfanya mtu kujiamini kwa
kujua wapi tulikotoka na tulipo na tunakokwenda. Lakini
hakuna chenye faida tu bila ya kukosa hasara, Historia pia ina hasara
zake hapa nakupa moja ya hasara kubwa ya historia kwa mtazamo wangu na wewe najua unazo zako kwa mtazamo wako.
Historia inajenga CHUKI.
Kitendo cha mtu kusoma historia ya vifo vya watu maarufu na wasio maarufu manyanyaso na mateso waliyofanyiwa ima kwa haki ama sio kwa haki kwa mtu mwenye kuvuta hisia ya mateso hayo na ikamuingia akilini inauma sana na hasa ikiwa ni ndugu yako rafiki au jamaa.
Historia inaeleza kila kitu unaweza kusema ni mchezo wa kuigiza lakini ni ukweli kila kinachoelezwa ndivyo kilivyokuwa.

Mfano hai juu ya CHUKI inayoweza kutokea ikiwa ni moja ya hasara ya historia: Kifo cha
aliyekuwa Raisi wa Libya Muammar Gadhafi.... kizazi chetu cha miaka ya hii yapo mengi tulioyashuhudia na kuyasikia matukio mengi ya kutisha na
kusikitisha mbayo tayari yamekuwa historia katika kizazi chetu pia yapo
ambayo tayari yameingia katika vitabu vya kufundishia.
Je
unafikiri nini kitafuata kutoka familia ya Gadafi kwa maumivu waliyoyapa
baada ya kuuwawa ndugu yao, hapo ni chuki ya kudumu baina ya
walioshiriki kufanya kitendo hicho na wanaukoo wa Gadafi kitu ambacho
lazima kitajenga hali ya malipizi ambayo lini yatatokea haijulikani pia
kumbuka msako aliokuwa akisakwa Osama Bin Laden mpaka kuuwawa kwake nini
kitaendelea kwa watu waliokuwa wanamwamini na kumtegemea Osama tayari
kuna chuki baina ya taifa moja na jingine na baina ya ndugu.
Hiyo
ni baadhi ya mifano ya kujenga chuki kwa vizazi vilivyopo na vijavyo
ambavyo ni lazima watasoma matukio hayo kupitia somo la historia na hivi
karibuni tumeona vitendo vya kinyama vinavyotokea nchini kwetu kwa
Zanzibar imeonekana kupitia Jumuia ya muamsho pale walipokuwa wakidai
nchi kisiwa chao kwa njia ambayo imeelezwa isiyo ya halali na kupelekea
vurugu za hapa na pale na kuathirika kwa baadhi ya watu pamoja na mali.
Mbali
na hilo wiki chache zilizopita tumeona unyama aliofanyiwa aliyekuwa
kiongozi wa mgomo wa madaktari docta Ulimboka ambaye alitekwa na kupigwa
vibaya ok ijapokuwa waliofanya hivyo hawajajulikana hadi sasa lakini
tayari kuna chuki imejijenga baina ya madaktari na serikali "what will
happen?"
Kanisa la kihistoria mjini Zanzibar
Kanisa hili lilianza kujengwa mnamo mwaka 1873 na kukamilika mwaka 1880 ni miaka 132 iliyopita mpaka leo hii, Edward Steere alihusika katika ujenzi wa kanisa hili la Angrican lililopo mkunazini mjini Znz.
Wengi huenda mkawa mnasikia tu mkunazini bila kujua "why" panaitwa hivyo. Mti unaoonekana pembeni ya kanisa hili unaitwa Mkunazi ni mti ambao matawi yake yalikuwa yakitumika kama fimbo ya kuwachapia ndugu zetu enzi hizo za biashara ya utumwa. kutokana na umaarufu wa mti huo unaoitwa mkunazi ndiko kulikopelekea mtaa huo kuitwa mkunazini.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments