Friday, July 20, 2012

WATANGAZAJI WA COCONUT FM WAKITAKIANA RAMADHANI KAREEM

Meneja wa Coconut Fm ambae pia ni mtangazaji wa kipindi cha Nipe Nikupe akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kuzungumza na watangazaji wake.
Juu na chini ni picha ya pamoja ya watangazaji wa Coconut fm
Coconut fm yajipanga kufanya vipindi vizuru vitakavyoendana na mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni siku chache zimebaki kuweza kuupokea mwezi huo mtukufu.

Meneja wa Coconut Fm Husna Abdul Megeni wa Bahari alisema "Coconut fm ni redio inayomhudumia vizuri mzanzibari katika kupata taarifa muhimu za ndani na nje na kwa upande wa burudani pia hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kumpatia huduma nzuri zaidi kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani" aliyaesema hayo jana alipokuwa akizungumza na watangazaji wa Coconut fm na kusisitiza kuwa vipindi vimepangwa vizuri kulingana na mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Pia amewataka wasikilizaji wa Coconut fm kuendelea kusikiliza vipindi vizuri vilivyondaliwa kwa ajili ya mwezi mtukufu na kuwahakikishia kuendelea kutoa huduma bora itayokidhi haja yake kwa kipindi chote.

Kwa upande wa wafanyakazi na waendeshaji wa vipindi wamesema wamefurahishwa sana na mpangilio wa vipindi walioupanga kwa ajili ya Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments