Wednesday, July 18, 2012

MB DOGG NOW IS BACK

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 Mb Dogg alitamba katika game na ngoma zake kali kama Si Uliniambia, Mapenzi Kitu Gani, Latifa, Naona Raha na akaja kupotea ghafla baada ya ngoma ya Sagablasha ambayo ilifanya vizuri kiasi. Hizi ni baadhi ya ngoma ambazo ziliweza kumweka juu msanii huyu Afrika Mashariki.

Baada yakimya cha muda mrefu sana mengi yamezungumzwa na mashabiki kuhusiana na Mb Dogg wapo waliodiriki kusema game limemshinda na wengine kusema amefulia bila kukumbuka kwamba Mb ndio muasisi wa muziki wa kuimba hapa nchini, lakini hayo yote hakuonyesha kujali yeye binafsi kwa kuwa alikuwa anajua kitu gani ambacho amekipanga.

"Nilikuwa kimya kwa muda mrefu hivi niliamua kucheki na bisnes nyingine kwani maisha hayatafutwi kwa kung'ang'ania kitu kimoja, muda wote huo nilikuwa nipo South Africa nikifanya biashara zangu" hayo alifunguka Mb. pia aliongeza kusema kwamba wengi walidhani kupotea kwake kwenye game kumesababishwa na kuondoka kwake kwenye kundi la Tip top connection kitu ambacho amesema sio kweli.
"Sasa naanza kuwapa kitu kimoja kimoja mashabiki wangu wafurahie naomba wanipokee kama walivyonipokea mwanzo kwani uwezo wangu umezidi kukua hiyo ngoma ya "The only one" ni mwanzo tu wa ujio wangu mpya" MB alisema.


Now Mb Dogg is back na brand new song "The only one" hii ni kwa kuwafurahisha mashabiki wake na kuwakumbusha kwamba bado yupo na anawajali wapenzi wake waondoe shaka sasa ni wakati wa kufurahia ile ladha waliokuwa wameimisi.
Mb Dogg - The only one

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments