Mkali toka Tanzania House of Talent (THT) maarufu kwa jina la Beka amekutwa akigonga lunch kwa mama ntilie mchana wa leo.
Msanii huyo kutoka THT ambaye yuko Zanzibar kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alioshirikishwa na Fan Kis toka Jupiter Rec amefunguka kusema kwamba "Zanzibar life is very expensive ukilinganisha na Tanzania bara" ametoa mfano hai kwa upande wa vyakula paoja na hoteli kuwa gharama zake ni kubwa kiasi ambacho kwa mtanania wa kawaida ni vigumu kuyamudu maisha haya.
Beka ameongeza kusema kuwa Zanziibar ni nchi ya kitalii na kuna watalii wengi sana ambao wanaishi kama wapo kwao hali inayowapelekea wafanyabishara wengi kufanya biashara zao kwa kuwatazama watalii hao kitu ambacho kinamuumiza mzanzibar wa kawaida kwa baadhi ya mahitaji muhimu hususan chakula.
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments