Thursday, December 10, 2015

Ngoma Mpya | Nipende Kama Nilivyo - Ram Life ft Makamua & B the Boss Man

Msanii  wa hip hop "Ramlife" ameachia ngoma mpya maskioni mwa watu ambayo ameitambulishwa rasmi kupitia www.eriqure.com , Wimbo unaitwa NIPENDE KAMA NILIVYO ulioandaliwa na Producer KAJU BEATS, Amemshirikisha "Makamua na B The Boss Man"
Download & Share Link > http://bit.ly/1Nacj50

Best Nasso kuja na mkwaju mpya


Baada ya Kusemekana Best Nasso amekamatwa nchini Congo na madawa ya kulevya hatimae ameweka wazi wa mashabiki wake kua tuhuma hizo si za kweli na kutambulisha  wimbo wake mpya.

Wimbo huo ameupa jina la "RUMBA" na ameshafanya video yake amesema kuwa wimbo huo utaanza kupatikana kwenye mtandao wa Mkito.com kuanzia jumamosi tarehe 12 mwezi wa 12 ambayo ni siku yake ya Kuzaliwa.

EWI (Environmental Warriors Of Ilboru) yaachia ngoma "Kumbusho kwa Rais"

EWI (Environmental Warriors Of Ilboru)  yaachia ngoma mpya "KUMBUSHO KWA RAIS" HipHop yenye sauti ya mkali Bounak, Spac Dawg, Boox, Chindo pamoja na Gnako mkono toka kwa defxtro noizmekah Studios.

Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli atangaza baraza la mawaziri wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza. 

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. 

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

WIZARA
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina

Ajira, walemavu: Jenista Joakim Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Abdallah Possi. M ambae ni mhadhiri Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.
Endelea hapa http://www.jamiiforums.com

Tuesday, December 8, 2015

Manispaa ya mji Unguja yaombwa kuondosha majaa yaliopo maeneo ya makazi ya watu.

Kibao kinacho onya utupaji wa taka eneo hili.


Wakati mvua zikiendelea kuonyesha mjini Zanzibar huku magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu ikiwemo kipindu pindu yanaendelea kujitokeza.
Baadhi wa wakazi wa Mombasa Unguja wanakabiliwa na wakati mgumu pindi inaponyesha mvua kutokana na maeneo ambayo wanaishi kuwa ni sehemu ya kutupa taka.
Wananchi hao wamesema pamoja na manispaa kudhiti watu wasitupe taka eneo hili kwa kuweka vibao vinavyokataza lakini wamekuwa wakiendelea kutupa taka nyakati tofauti hasa usiku.
Hivyo wameomba Serikali ifanye jitihada ya kuziondosha taka hizo na kusafisha eneo hilo.