Saturday, June 29, 2013

Africa kusini waandamana kupinga ziara ya Rais Obama

Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa
wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa
Raisi Obama nchini Humo wakati wa
maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa
Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika jana
Jioni - Juni 28
Endelea hapa Jamii forums

Published with Blogger-droid v2.0.10

Friday, June 28, 2013

Hili ndio duka lenye pamba za kijanja mjini Tanga, lipo barabara ya 13 karibu na jengo la maabara.

Msimu wa sikuku umefika sasa wajanja wote mnaohitaji kupendeza kwa mitoko ya kisasa, tembelea duka hili lililopo barabara ya 13 mjini Tanga.

Nguo za aina mbalimbali kwa kinadada na kibakaka zinapatikana, viatu, nguo za watoto, madera, top, skin, tait, sketi usiulize utapendezaje nenda ujionee mwenyewe.

Kwa urahisi wa kufika dukani hapo fuata maelekezo haya
Ukitokea Taifa road mtaa wa 13 maarufu mtaa wa maduka ya wachaga unaenda mpaka barabara ya sokoni ngamiani kushoto utaona jengo limeandikwa maabara, utanyoosha kama unaelekea kituo cha daladala za donge upande wa kulia kwako utaona maduka ya simu fuata laini hiyo mpaka utapoona duka la dawa za asili duka linalofuata hapo utakuwa umefika.
Kwa mawasiliano piga 0713 700 951 au 0767 600 951
Nyote mnakaribishwa.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Mwizi wa Baiskeli achezea kichapo asubuhi hii

Umati wa watu wakiwa wamemzonga mwizi aliyekuwa akichezea kichapo kwa kuiba baiskeli, picha halisi ya mwizi huyo sikuweza kuipata kutokana na umati wa watu kuwa mkubwa.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Thursday, June 27, 2013

Made in Tanzania

Watanzania tunaweza hii ni mashine ya kuchomelea (wolding) ambayo imetengenezwa hapa hapa nchini Tanzania.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Madampo ya Soko la Ngamiani.

Manispaa ya jiji la Tanga wana jitihada kubwa za kuhakikisha mji unakuwa safi kwa kuweka vyombo maalum vya kuhifadhia matakaka.

Hapo unavyoona ni asubuhi ya leo wahusika wakiwa wapo kwenye harakati za kuzoa taka hizo maeneo ya soko la Ngamiani.

Pamoja na jitihada zinazoendelea kuchuliwa na Manispaa ni vema kuhakikisha vifaa hivyo vya kuhifadhia taka mitaani havijai kuputiliza ili kuepuka taka hizo kuendelea kuwa ni uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa ya maeneo hayo.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Tuesday, June 25, 2013

Jengo la ghorofa 6 linalofikiriwa kuwa la kwanza kwa urefu Tanga mjini.

Tanga ni miongoni mwa miji iliyopewa hadhi ya Jiji nchini Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tabora.

Mji wa Tanga ni mji mkuu wa Mkoa wa Tanga
uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi. Tanga
ina bandari kubwa kabisa katika sehumu ya
kaskazini mwa Tanzania . Njia ya reli kwenda
Mji wa Moshi inaanza hapa.
Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la
Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni:
Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara
upande wa mto na Shamba juu ya mlima, neno
hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei
ambalo ni wenyeji wa mkoa huo linamaana ya
shamba, wao hulitamka N'tanga.

Vilevile Tanga ni mji ambao unapata maendeleo kila kunapokucha wawekezaji wa ndani wanajitihada kubwa ya kuwekeza majengo ya kisasa na kuonyesha mabadiliko ya mji huo.

Published with Blogger-droid v2.0.10
Published with Blogger-droid v2.0.10

Nyumba yabomolewa barabara ya 9 Tanga, wenyeji waendeleza makazi.

Takribani wiki ya pili sasa tangu Nyumba hii iliopo barabara ya 9 mjini Tanga Ilipovunjwa kwa madai kuwa imeuzwa laikini wenyeji bado wanaendeleza makazi katika nyumba hiyo.

Published with Blogger-droid v2.0.10

Harakati za mjini

Published with Blogger-droid v2.0.10

Maisha bora kwa kila mtanzania

Published with Blogger-droid v2.0.10

Tanganyika 1961 hadi 1964

Bendera ya Jamhuri ya Tanganyika 1961 hadi1964

Published with Blogger-droid v2.0.10

Ulezi wa kuku

Published with Blogger-droid v2.0.10

Ujumbe wa leo

Published with Blogger-droid v2.0.10

Wednesday, June 12, 2013

KERO KWA MADEREVA TANGA

Tangu msimu wa mvua uanze mpaka umeisha
mfreji huu uliopo barabara ya jamaa umekuwa
ni kero kwa waendesha baskeli, pikipiki na
magari kutokana na kuongezeka kwake kila
kukicha.
Pamoja na kuwa kero kwa madereva pia
umekuwa ukihatarisha maisha ya watembea
kwa miguu kutokana na vyombo vya usafiri
kupita pembeni sana kwa ajili ya kukwepa
mfereji huo.

Tuesday, June 4, 2013

Mambo ya kitaa hayo

Maafisa wa Polisi kikosi cha usalama Barabarani wapewa somo juu ya matumizi ya kifaa cha kipimia ulevi madereva

Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (kulia) na Mkurungezi wa Operesheni Upturn Group Co - Mr. Muhata Denis (kushoto) wakijadiliana jambo kuhusu kifaa cha kupimia ulevi (alcohol test) wakati wa semina ya Siku mbili ya
kipima ulevi (alcohol test) yaliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam- Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Bofya kwa habari zaidi

Monday, June 3, 2013

DOGO FETY AKIWA NA KINYAMBI NA CHAMOYO

Msanii chipukizi Fatuma Abdalah Jengo aka Fety akiwa katika pozi na mastar anaowakubali kutoka Vituko Show Kinyambi na Chamoyo.
Fety ni msanii chipukizi aliopo katika kundi la King Majuto lenye maskani yake mjini Tanga.
Kwa sasa Fety ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya Seminary Hanga mkoani Ruvuma, yupo katika maandalizi ya mtihani wa kuingia darasa la tano.
Fety mpaka sasa hajawahi kushiriki katika movi yoyote kutokana na hali ya masomo kumuweka bize.

Kwa mujibu wa mipangilio yake kwa sasa hayupo tayari kucheza filamu yoyote kwa kuhofia kujisahau katika masomo "Ni kweli sipo tayari kushiriki filamu kutokana na hali ya masomo kuwa taiti, naelewa kuwa hakuna filamu ya kuchezwa siku moja kwa hiyo zile siku ambazo nitakaa kambi kwa ajili ya kushuti zitaniathiri sn kasomo".

Kitu ambacho anakitarajia ni kutumia muda wake wa likizo kuweza kushiriki filamu ambayo itakuwa inafanyila kwa kipindi hicho.