Monday, October 12, 2015

Taifa Stars yasonga mbele

Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) imesonga mbele katika michezo ya raundi ya kwanza kwa kanda ya Afrika ya mchujo wa kombe la dunia litakalofanyia huko nchini Urusi mwaka 2018.
Taifa stars wakicheza ugenini huko nchini Malawi walikubali kulala kwa kichapo cha bao1-0 dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya Malawi The Flames.
Bao lao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakia ya 41 na mchezaji Dave Banda.
Licha ya kuchapwa kwa bao hilo Tanzania wamesonga mbele kwa hatua ya pili baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Stars watacheza Raundi ya Pili na timu ya taifa ya Algeria, ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko Algiers hapo Novemba 17.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja

Dismond Platnumz, Vanesa Mdee, Ommy Dimpos wajinyakulia tuzo za Afrima

Diamond Platnumz akishow love na moja ya tuzo alizoshinda pamoja na mchekeshaji kutoka Nigeria Basketmouth.
"I do know what to say"
Picha hii Platnumz ameipost mtandao wa Twitter akionyesha hajui aseme nini kwa furaha alio nayo kwa kushinda tuzo hizo tatu.
Vanessa Mdee akiwa na tuzo.

Wanaboa - Samata



Msanii wa kizazi kipya Samata ambae pia ni mhandisi,mbali na kazi yake ya uhandisi anapenda sana muziki hali inayompelekea kutenga muda wake vizuri kwa ajili ya muziki.
"Wanaboa" ni wimbo wake ambao amehusisha hali ya maisha halisi ya  kila siku hasa uswahilini ambapo kuna tabia tofautitofauti za watu na tabia nyingi ni za ajabuajabu.

Bofya hapa upate kuicheki nyimbo hii WANABOA YOUTUBE LINK

Bonie-Norini + Ngina

 Bofya hapa kudownload https://mkito.com/song/ngina-ft-mamsi/16675 kupakua "NGINA" wa Bonie na HAPAhttps://mkito.com/song/norini/16676 kupakua "NORINI" kwa mahojiano/mawasilano zaidi check na Bonie kwa nambari +255 754 422 764 powered by @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com  @defxtro #vmgafrica #SupportYourOwn
--

Thursday, October 8, 2015

NEW HIT TRACK: KINGKAPITA FT. CANNIBAL - VIZABIZABINA


Baada ya kimya cha muda mrefu msanii King Kapita ambaye kwa mara ya mwisho ulimsikia katika wimbo wake wa "Kuna tatizo kwani?" ambao amemshirikisha Godizilla, amerudi nchini kutoka Africa ya Kusini ambako alikuwapo kimasomo.

Msanii huyo anaefanya muziki ni ujasilia mali amerudi kwa kasi mpya na kufanya ngoma ya VIZABIZABINA aliyomshirikisha Cannibal Shatta kutoka nchini Kenya iliyotengezwa na John B pamoja na Kanyeria. 
Baadhi ya nyimbo ambazo jamaa amewahi kufanya pia ni Shikamoo pesa, Mtoto mlito na Here we go alipokuwa ndani ya kundi la Wakacha kabla ya kuwa msanii wa kujitegemea.


Monday, October 5, 2015

Jojo aanza kueleweka na "Nakuhitaji"


Mwanadada Jojo ameanza kusomeka kitaani na ngoma yake Nakuhitaji ambayo siku chache zilizopita imeingia kitaa na kuanza kuchezwa na vituo mbalimbali vya radio

UTAMBULISHO WA NYIMBO YA 'SITAKI SHARI', RIZ CONC FEAT. SIR ZULU


Riz Conc anatambulisha nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la 'SITAKI SHARI', ambayo amemshirikisha rappa Sir Zulu. Itasikika katika Radio mbali mbali za Bongo na nje ya nchi kuanzia tarehe 05/10/2015. Nyimbo ya 'Sitaki Shari' imefanywa na producer ALONAME na kusimamiwa na Sudy Baya_KingMaarifa chini ya uongozi wa Pesasina Co. LTD.