Saturday, June 30, 2012

Friday, June 29, 2012

Thursday, June 28, 2012

PUNDA AKIJITAFUTIA RIZKI YAKE

Punda ni mnyama mtaratibu na mwenye busara katika mfumo wake wa maisha na ni mnyama aliyejaaliwa na Mungu uwezo mkubwa wa kustahamili tabu za aina mbalimbali ni mnyama aliyebahatika kuwa mmojawapo katika mifugo ya binadamu.
Mara nyingi punda amekuwa ni msaada mkubwa katika shughuli ndogondogo za binadamu kama vile kubeba mizigo au kubeba watu katika safari za hapa na pale.
Jukumu kubwa la mfugaji wa punda ni kumpatia huduma muhimu mnyama huyo ikiwemo chakula, maji, sehemu nzuri ya kulala pamoja na matibabu.
Lakini imekuwa ni tofauti kwa baadhi ya wafugaji huenda ni kutojua umuhimu wa punda ingawaje ni mfugaji, mfano mdogo ni huyu punda unaemuona hapo akiwa yupo jalalani kwa ajili ya kujitafutia chakula huenda mmiliki wa punda huyu hajui nini maana ya kumfuga mnyama huyu na badala yake anamtumia katika kukamilisha shughuli zake tu pindi anapohitaji msaada kutoka kwa punda huyu.
Je unafikiri ni haki kumlea mnyama kama punda pasipo kumpatia mahitaji muhimu? Na kwa hali hii ya kula majalalani kweli ataepukana na maradhi ya kudhoofisha afya yake?

Ndani ya jengo hili kuna ofisi ya ...Coconut fm, Jupiter Rec & Chando Consultant


Mambo ya majuu hayooooo


Wednesday, June 27, 2012

WAVUVI WAKIWA MZIGONI ASUBUHI YA LEO


RAHA YA PEMBA POLO....

Kwa wale wenyeji wa Kisiwani Pemba na wale waliowahi kwenda japo kwa mara moja tu wanajua kuwa safari ya Pemba ...Polo bana,,, kama si kwenda basi kurudi lazima kitu cha Polo kihusike na safari yako.

RICO SINGLE AKIWA T TOP REC

Katika harakati za kuboresha, 

Tuesday, June 26, 2012

PRESIDAAAAAA....CAN YOU IMAGINE? AU HAYA NDIO BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA?



KUMBE SWAHILI GONGANA HADI SERIKALINI

Hali hii ni lugha tuliyozaliwa nayo watanzania vipi kwa upande wa lugha za wakina welcome huko serikalini?

Monday, June 25, 2012

Thursday, June 21, 2012

Wastara Ashukuru Watanzania-"Baada ya Miezi Mitatu Sajuki Anaweza Kuanza Kuigiza"

Maombi ya watanzania pamoja na michango yao ya fedha vimesaidia kumfikisha mwigizaji Sajuki hapa alipo baada ya kupata nafuu kubwa toka apelekwe India kuitibiwa. Wastara akizungumza exclusive na millardayo.com amesema Sajuki anaweza kuanza kuigiza hata sasa kwa sababu nguvu imesharudi, anaweza kutembea kwa muda mrefu na hata hali yake ya sasa imebadilika sana tofauti na mwanzo. Amesema “baada ya miezi.......click here to cont.... Source Bongoflavortz.blogspot.com

Monday, June 18, 2012

TRACED YAMSAIDIA MSICHANA ELIZABERTY MSHANA

Msicha  Elizaberty Mshana(26) mkazi wa Kihonda Mbuyuni kata Mafisa akiwa katika kiti cha magueudumu alichopewa na shirika linaloshughulika na watoto wenye ulemavu TRACED, kushoto ni Cont..

MOJA YA MTAA MAARUFU JIJINI NAIROBI

Mbali na maeneo mengi nilyotembelea mjini Nairobi kuwa yako safi na yanavutia lakini bado jitihada kubwa ya miundo mbinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo zinahitakijika kwa lengo la kuupelekea mji wote kuwa katika hali ya kufanana. Picha unayoiona hapo juu ni mtaa maarufu sana kwa wafanyabiashara mbalimbali ambao upo nje kidogo ya mjini na hiyo ndio barabara inayopita daladala zinazotoka mjini kuelekea huko (kibongo bongo hii ni kariakoo) mtaa huu wote ni mchafu kama unavyoonekana hapo na ni hali inayowapa shida watembea kwa miguu kama unavyoona wanakatisha barabara hiyo kwa shida sana kutokana na tope zinazojitokeza wakati wa mvua...Cont...

Friday, June 15, 2012

AJALI YA GARI KILIMANI BAR

Gari aina ya Nissan Premier yenye nambari za usajili Z 621 DB ikiwa imeacha njia baada ya kugongwa kwa nyuma na gari ndogo aina ya Vits yenye nambari za usajili Z 999 CX maeneo ya kilimani bar mchana wa leo.
Madereva wa magari yote mawili hawakuweza kupatikana majina yao ila kwa taarifa kutoka kwa walioshuhudia ajali hiyo wamesema dereva wa toyota premier ambaye gari yake imegongwa kwa nyuma aliwahishwa hospitali ya Arahama lakini dereva wa Vits hakuumia hata kidogo. Pia walielezea kwa jinsi walivyoishuhudia wao ajali hiyo kwa kusema..
Dereva wa toyota premier alikuwa akitokea njia ya uanja wa ndege kufika maeneo ya kilimani bar akasimama pembeni ya barabara ambapo hakujulikana anafanya nini muda mfupi akaondoa gari na kutaka kuhamia upande wa pili wa barabara ili arudi alikotokea. Wakati anaingia barabarani kulikuwa kuna Vits nyeusi inakuja bila ghafla wakashangaa vits imegonga nyuma ya Premier.
Baadhi ya walioshudia wameongeza kusema kuwa dereva wa toyota premier hakuwasha indicator kunyesha kama anahamia upande wa pili ndio mana dereva wa Vits hakuwa na wasiwasi kwa mwendo wake wa kawaida aliokuwa nao na kujikita kalivamia gari hilo.

Vits iliyopata ajali ikiwa imeegeshwa pembeni ya barabara wakisubiri askari wa usalama barabarani.

UNAONAJE HALI HII?


ISON AGONGA VIDEO YA HALOO BABA

Msanii maarufu mjini Zanzibar aliyekuwa akiigiza kwenye kundi la Black Roots almaaruf kama Mwinchande akicheza party ya Mr President kwenye video ya Haloo baba ya Ison, Mr President akiwa kwenye kikao muhimu na kamati yake pamoja na waandishi wa habari alijikuta akipokea simu kutoka kwa mtoto wake na kusahau kama yupo kwenye kikao muhimu alijikuta akinyanyuka kikaoni na kuondoka akaacha mshangao mkubwa kwa wanakikao pasipo kujua ni kitu gani kimemsibu mheshimiwa.
Producer wa T Top Chief Elia akiwa amecheza kama mwandishi wa habari akiwemo Dj Dr B wa Coconut Fm, Hussein Hamis wa Coconut Fm, Donisia Thomas wa Bomba Fm wote wakiwa kama waandishi wa habari hapa wakiwa wamepigwa na butwaa kuona Mr President anaongea na simu na kusahau kama yupo kikaoni.

SAFARI NJEMA


Ajali kazini, gari life lakini mzigo ufike

LORI LA MAMLAKA YA BANDARI LATUMBUKIA MTARONI.

Chanzo cha habari hii ni Michuzi blog baada ya pitapita za hapa na pale alilifuma lori hili linalomilikiwa na mamlaka ya bandari likiwa limetumbukia maroni barabara ya kuelekea Kilwa. Kwa mujibu wa mwanahabri hakuna mtu aliyeumia.

WAZEE WAKISELEBUKA KITAANI


Monday, June 11, 2012

MAZINGAOMBWE BADO YAPO

Mmoja wa Mwanamazingaombwe wa mjini Iringa aliyejitambulisha kwa jina la Almas a.k.a Afande Sele akionesha akadabla akadabla zake mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,mjini Iringa wakati wa utambulisho wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo itaendelea kutambulishwa tena katika mkoa wa Arusha na baadaye jijini Mwanza
Source  http://djchoka.blogspot.com/