Friday, October 31, 2014

Mic lon ft gosby & wakazi - Just pretend (official video)Important mainly because of the people in the conversation.

The official video for Just pretend by mic lon ft gosby and wakazi video shot by Ali of 'Mchume Digital'

DRUNK IN LOVE REMIX by GOSBYImportant mainly because of the words in the message.

Gosby lets off another tune from his upcoming mixtape, MISSTAPE . DRUNK IN LOVE REMIX'', mixed and mastered by CJAMOKER. Check it out below Gosby's hulkshare profile. LINK: hulkshare.com/j122hv72mmm8

Uraia katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoka katika Rasimu ya katiba inayopendekezwa

Uraia katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoka katika Rasimu ya katiba inayopendekezwa Uraia wa Jamhuri yaMuungano 65.-(1) Mtu ambaye, kabla ya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa Jamhuri ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano. (2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili na utapatikana kwa njia ya kuzaliwa au kuandikishwa. Haki ya uraia 66. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha raia kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri. Uraia wa kuzaliwa 67.-(1) Kila mtu aliyezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa kuzaliwa, mama au baba yake ni, au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano. (2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa mama au baba yake ni raia wa Jamhuri ya Muungano. (3) Endapo mmoja kati ya wazazi wake alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kana kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo. (4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atachukuliwa kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa. (5) Endapo uraia wa wazazi wa mtoto aliyepewa uraia chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4) utabainika kuwa si uraia wa Jamhuri ya Muungano, uraia wa mtoto huyo utasita. (6) Bila kuathiri masharti ya Ibara hii, Bunge litatunga sheria ambayo itaweka masharti na utaratibu wa: (a) upatikanaji wa uraia kwa watu waliozaliwa na raia wa Tanzania nje ya nchi; (b) kurudisha uraia wa watu ambao uraia wao ulifutwa baada ya kupata uraia wa nchi nyingine; na (c) mambo mengine ambayo yatatakiwa kutungiwa sheria. Uraia wakuandikishwa 68.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkaazi wa Jamhuri ya Muungano na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria za nchi anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano. (2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano na ambaye: (a) amedumu katika ndoa hiyo kwa kipindi cha miaka saba mfululizo; na (b) ametimiza masharti yaliyoainishwa katika sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), anaweza kuomba uraia wa kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano. (3) Endapo ndoa iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake wa Tanzania, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano. (4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika ibara ndogo ya (2), atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa. (5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake si raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kuasiliwa kwake, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuandikishwa. (6) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, kusimamia masuala yanayohusu uraia wa Jamhuri ya Muungano. Hadhi maalum ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania 69. Bila kuathiri masharti yaliyomo kwenye Sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi maalum kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.

Wednesday, October 29, 2014

KAMANDA RAS MAKUNJA AHOJIWA NA OFFENER CHANNEL (O1) YA UJERUMANI

AWAOMBA MAPOROMOTA KUWAPA NAFASI KUBWA WASANII WA TANZANIA ! ATAKIWA KUELEZA KWA NINI ? NGOMA AFRICA BAND IMEKUWA TISHIO !
Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja kiongozi mwanzilishi wa bendi maarufu Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni ya kule Ujerumani,juzi kati Kamanda Ras Makunja aliwekwa kiti moto au kigoda cha moto na kituo cha TV cha Offener Channel ya Ujerumani. mwengozaji wa kipindi katika mahojiano hayo Bw.Fischer alimkutanisha Kamanda Ras Makunja na wataalam na wadau wa muziki wa kimataifa. Akikaribishwa katika kipindi hicho mwanamuziki Ras Makunja ametajwa kuwa jamii ya ujerumani inauthamini na kuukubali mchango mchango wake wa kutumia muziki katika kutokomeza ubaguzi,historia imemtaja Kamanda Ras Makunja na kikosi kazi Ngoma Africa band kuwa kuanzia mwaka 1993 alikubali kuzunguka ujerumani nzima kufanya maonyesho ya "WE ARE ONE" onyesho liliofanikiwa kuwaunganisha wageni na wenyeji kazi ambayo haikuwa rahisi lakini ilifanikiwa. Lakini pia wadau wa muziki na mtangazaji walitaka kujua inakuaje ? kwa muda wa miaka 21 Ngoma Africa band inadumu na kuendelea kuwanasa washabiki kwa wingi ?? Kamanda Ras Makunja akijibu swali hilo japokuwa alionekana si wakutaka kuweka hadharani kila mbinu,lakini alifunguka kwa kusema kuwa muziki unachezeka lakini pamoja na kuchezeka pia wanamuziki wa bendi ya Ngoma Africa band ni watumishi wa washabiki na wadau wa muziki kwa maana hii bendi inamilikiwa na washabiki na wadau ambao wao ndio wanayoitangaza. Sisi tuna vyombo vya muziki tu.Mimi naongoza bendi tu lakini wamiliki ni washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa band , bandi hii ni sauti ya umma wa kimataifa pia ni sauti ya wasio sikika "Voice of speachless" ambayo inasikika kimataifa Ras Makunja alisema. RAS MAKUNJA ALIPOITUMIA FURSA KWA KUWAOMBA MAPOROMOTA KUWAPA NAFASI WASANII WA TANZANIA !! walio nyumbani Kama kawaida yake Kamanda Ras Makunja bila kujisihau wapi anatoka yaani mtanzania aliyekunywa maji ya bendera! alipoulizwa juu ya vipaji vya wafrika? Kamanda Ras Makunja moja kwa moja aliwaomba wadau na maporomota wa kimataifa kuwapa nafasi kubwa wanasanii waliopo nyumbani Tanzania kuja kushiriki maonyesho ya kimataifa, Ras Makunja aliwaomba na kuwashawishi maporomota na wadau hao kuwa nchi ya Tanzania ina utajiri wa maelfu ya wasanii wenye vipaji vya ajabu wakiwemo wanamuziki,watengenezaji wasanaa za mikono wanawake kwa wanaume,wacheza maigizo,sarakasi,wachoraji,nendeni Tanzania mkaonane nao ,wapeni nafasi wasanii hawa muone jinsi watakavyo kuja kufanya sanaa ambazo hapa ulaya ni adimu sana . Ninawaombeni nendeni Tanzania na mkitaka msaada wangu wa kuwaelekeza mimi nipo Tayari - Kamanda Ras Makunja alimalizia kwa kuwaomba wadau na maporomota. Kamanda huyu wa Ngoma Africa Band Ras Makunja alionekana kutumia fulsa kwa kuwapigania wasanii wa nyumbani ili wapate nafasi zaidi ya kimataifa. Nje ya uringo alipoulizwa mbona ameifagilia Tanzania sana na swali lilikuwa wasanii wa Afrika, Makunja alijibu kwa mkato heti hata Umoja wa mataifa kila nchi ina balozi wake na akatimua zake. burudika nao at www.ngoma-africa.com wape shavu at www.facebook.com/ngomaafricaband

BONDIA WA KIKE MWAFRIKA ACHUKUA UBINGWA WA NGUMI ULAYA !

BINTOU YAWA SCHMILL aka "THE VOICE"
Frankfurt,Germany, Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill,mkazi wa Ujerumani siku ya ijumaa 26.September 2014 alifanikiwa kuchukua taji la ubingwa wa ngumi za kulipwa unatambuliwa na IBF,Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake bondia Mirjana Vujic kwa K.O katika raundi ya 3,. Pambano hilo lilionyeshwa Live katika TV channel ya euro sport na ktazamwa na maelfu ya watu wakishuhudia bondia wa kike mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radu. Bintou Schmill (30) aka The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,Katika pambano la Ijumaa 26.September 2014 liliofanyika kwenye ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied,lifanikiwa kumpa wakati mgumu mpinzani wake kuanzia round ya kwanza hadi ilipofika raund 3 bondia Mirjana Vujickatika alipigwa kwa KO na Bintou Schmill aka "The Voice" kutangazwa ndie bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani ulaya na kuvikwa mkanda huo unatambuliwa na IBF.Bintou Schmill aka 'The Voice' anaye fananishwa na Simba Jike (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani ! Mengi kuhusu bondia Bintou Schmill aka 'The Voice" usikose at For more information write to

NAVY KENZO - I JUST WANNA LOVE YOU

Tuesday, October 21, 2014

FILAMU YA DOGO MASAI YASHINDA TUZO MAREKANI

Na Myovela Mfwaisa TCA. FILAMU ya kitanzania ya Dogo Masai iliyotengenezwa na kuongozwa na muongozaji Timoth Conrad ‘Tico’ imeibuka kidedea baada ya kushinda katika tuzo za Silcon Valley African Film Festival (SVAFF) kama Filamu Bora kutengenezwa Afrika (The best African Production Movie ) tuzo hizi zimetolewa California Marekani. Mtayarishaji wa filamu hiyo Timoth kupitia kampuni yake ya Timamu African Media amesema ushindi huo ni wa Tanzania ndio maana hata kama hakupewa Support na taasisi yoyote kutoka Serikalini lakini amefurahia kulitangaza Taifa kwa juhudi zake binafsi. “Nimepokelewa hapa California kama mfalme kwa ajili ya kuwania tuzo kubwa na yenye thamani kubwa, hapa nimeongelea fahari ya Taifa langu Tanzania, ni ushindi mkubwa sana nimepeperusha Bendera ya Tanzania,” “Ninayo furaha kubwa sana kushinda tuzo hii kupitia filamu yangu ya Dogo Masai, tuzo hii kwangu ni ya pili, baada ya tuzo ya Mdundiko kushinda, na tumeona ni bora kutumia gharama kutafuta tuzo kubwa kwetu hatuna tuzo,”anasema Tico. Filamu ya Dogo Masai imeshinda baada ya kuzibwaga sinema kutoka South Africa, Malawi, Egypt, Nigeria, pamoja na Uganda. Ni ushindi wa Afrika Mashariki kwani ilikuwa ni Tanzania na Uganda ndio walifanikiwa kuingia katika tuzo hizo kubwa, bado kuna sababu ya kujivunia kama ushindi wa kishindo. Changamoto kubwa ni kwa Basata ambao inasemekana wamekuwa wakizuia watayarishaji wasiandae kwa sababu zao ambazo hazijengi tasnia zaidi ya kudumaza, leo mtanzania anakwenda Marekani na kuibuka mshindi akitangaza Bendera ya Tanzania. Ushindi wa filamu ya Dogo Masai ni ushindi mkubwa kwa Tanzania ni kitu cha kujivuania na iwe njia kwa watayarishaji wengine kushiriki katika tuzo mbalimbali za filamu hata Oscar, huu ni mwanzo mzuri kwa kazi za Tanzania. Tico anawashukru wasanii wote walishiriki na kufanikisha utengenezaji wa filamu ya Dogo Masai, familia yake rafiki yake Dorice, timu nzima ya Timamu Casting Agency na kila mtu aliyeshiriki kwa mawazo na ushauri na anasema kuwa milango imefunguka kwani filamu yaDogo Masai imeingia katika kugombea tuzo nyingi. Dogo Masai pia imechaguliwa kuingia kwenye tuzo nyingine ya Rome Independent Film Festival (RIFF) za nchini Italy, na tayari kuna dalali za kuibuka na ushindi kwani watengenezaji wa filamu wamekuwa wakiiongelea katika mitandao mbalimbali, tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwakani mwezi wan ne Dogo Masai ni balozi kuitangaza Tanzania

Sunday, October 19, 2014

LAMAR FT YAMOTO BAND NITAJUTA THE REFIXImportant mainly because it was sent directly to you.

TMT MOVIE KULETA MAPINDUZI MAKUBWA BONGO

ILE Filamu kubwa kabisa kutengenezwa katika viunga vya Tanzania ya Tmt movie imeanza maandalizi yake kwa kurekodi filamu mpya huku wasanii waliopatikana kutokana na shindano la Tanzania Movie Talent kuibeba sinema hiyo wakiwashirikisha wasanii wengine waliochaguliwa katika sinema hiyo. Akiongea na FC mratibu wa filamu hiyo Staford Kihore amesema kuwa moja ya malengo makubwa ya Proin Promotion ni kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa, katika kuwasimamia wameanza nao kurekodi sinema TMT Movie. “Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford. Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahilihood. Filamu kubwa ya Tmt Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo. Sterring wa sinema hiyo ni milionia wa kutoka Mtwara Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Bongo wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima. &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&& LETA FILAMU YAKO DAR FILAMU FESTIVAL 2014 SASA KAMPUNI ya Haak Neel Production na Filamucentral waandaaji wa Tamasha la Dar Filamu Festival wanawakaribisha watengenezaji wote wa filamu zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutuma au kuwakilisha filamu zao katika ofisi za Haak Neel Production zilizopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere. TAMASHA kubwa kabisa la filamu Swahilihood hilo linapokea kazi zilizotoka mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha kubwa linalounganisha wadau na watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwengu na kutoa fursa kwa wadau wengi kutengeneza soko lingine. Akiongea na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula amesema kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani litafika kila kona ya Wilaya za Dar es Salaam na kutoa burudani ya kazi nzuri zinazotengenezwa na watanzania. “Kama ilivyo kauli mbiu yetu inasema “FILAMU ZETU, MAISHA YETU” ni kauli mbiu ya kutia matumaini kwa watengenezaji na watazamaji kwani filamu tuaamini kuwa ni kazi inayoweza kutengeneza ajira kubwa kwa kila mtu,”anasema Katula. Tamasha hili ambalo limelenga kukuza Lugha ya Kiswahili na kufanya kuwa ni biashara na alama kubwa kwa filamu zetu zinateka soko Afrika ya Mashariki kwa kuongea Kiswahili kitamu na kinzuri kinachovutia kwa wanaAfrika mashariki na Ulaya. Mtengenezaji wa filamu au mtayarishaji unatakiwa kuwakilisha filamu nakala mbili za filamu ambayo imetoka mwaka na kuonyeshwa kwa mwaka 2014, ikiwa samba na utambuzi wa mtayarishaji, imekaguliwa na Bodi ya Filamu pamoja na taratibu husika katika taasisi za filamu. Kwa mawasiliano na jinsi ya kuwakilisha filamu zenu wasiliana na +2552773113, +255754 578 730, +255754 260 688 Ongea na Dada Unce anakupatia maelekezo ya kufika katika ofisi za Haak Nell Production.

Saturday, October 18, 2014

KIPINDI KIPYA CHA BAMBA KWA BAMBA KUJA CHANNEL TEN

Picha ya chini ni Mtangazaji wa Bamba kwa Bamba Khalid Ali akiwa Mtaani
Hiki ndio Kipindi kipya cha Bamba kwa Bamba kinachokuja kwa kupitia Runinga ya Channel Ten mwezi huu. Mtangazaji wa Kipindi cha Bamba kwa Bamba Khalid Ali akiwa kazini. Mtangazaji wa kipindi cha Bamba kwa Bamba akiwa katika ya foleni akirekodi kipindi kwa ajili ya kuruka siku ya Jumamosi. Kampuni ya Saseni Media ya jijini Dar es Salaam imekusudia kuleta amani katika baadhi ya familia ambazo zimekuwa zikijikuta zinaingia katika sintofahamu baada ya mwanafamilia mmoja kuchelewa kurudi nyumbani kwa sababu ya foleni. Kupitia kipindi cha Bamba kwa Bamba ambacho kitaruka kwa nusu saa, jamii itapata kujionea hali halisi ambayo huwakuta abiria warudipo majumbani au asubuhi wanapowahi kwenda makazini, kwani hata kuna siku ambazo unawahi lakini foleni inakukwamisha na kupoteza malengo. Inakadiriwa kwamba wananchi waishio Dar es Salaam hukaa kwenye foleni kwa takribani masaa mawili mpaka matatu kwa siku au zaidi. Swali ni je muda wote huwa wanafanyanini? Au Wafanye nini? BAMPA KWA BAMPA ni kipindi kipya cha Televisheni kinachozalishwa na kampuni ya Saseni Media na kurushwa na Channel 10 siku za Jumamosi saa 12:00 mpaka 12:30 jioni. Bampa kwa Bampa ni kipindi cha kwanza cha Runinga kinachotoa fursa na uwanja wa mawazo kwa Watanzania wote. Ambao kwa muda huo wanakuwa kwenye foleni na walioko majumbani kushiriki katika kujadili na kutoa maoni, mawazo, mapendekezo na ushauri kuhusiana na mada mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa, nakupendekeza nini kifanyike ili kuleta maendeleo ya Taifa la Tanzania, katika Nyanja kadha wa kadha. Msemo wa ‘Bampa Kwa Bampa’ unaashiria namna magari ya kisogelea na kwaukaribu sana kiasi cha bampa la gari mbele (nyuma) na lile la nyuma (mbele) kuacha upenyo mdogo au pikipikikupita. Hii hutokea hasa nyakati za asubuhi na jioni. Mahojiano na watu walioko katika foleni, wakiwa ndani ya vyombo vya usafiribi nafsi au vya abiria, iwe ni gari dogo, kubwa, daladala, bodaboda, bajaj, baiskeli au una kwenda kwa miguu hii inakuwa ni fursa ya kukutana na mtangazaji wa kipindi Khalid Ali. Khalid Ali ni mhitimu wa Digrii ya Mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari na mwenye dhamira yakutafiti, kuchanganua, kuibua changamoto na kukusanya maoni na fikra za wananchi kuhusu maendeleo yao akiongozwa na falsafa ya kwamba maendeleo yetu, yataletwa na sisi wenyewe tukizungumza, kukumbushana nakujifunza kwa kupitia TV na hasa kipindi cha Bampa kwa Bampa.Pia wananchi wengine wanaweza kuchangia maoni yao katika mada za kila wiki kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Bampa Kwa Bampa kwa kutembelea Facebook na Twitter. www.facebook.com/BampaKwaBampa www.twitter.com/bampakwabampa Kipindi hiki kitakuwa kikirushwa kupitia Channel TEN kila siku ya Jumamosi, Saa 12:00 Jioni, kuanzia mwezi Oktoba 2014

EXCLUSIVE FOR DJ's & PRESENTERS......VEE MONEY FT LAMAR N GODZILA

Hii ni Exclusive kwa ma dj na presenters ngoma ya mwanadada Vanessa Mdee aka VEE MONEY akiwa amemshirikisha mkali wa kutayarisha muziki Lamar pamoja na mzee wa Lakuchumpa Godzila imetambulishwa rasmi katika radio stations. Hope fans there are waiting to here the nice flaver ya VEE Money from you.

Dorice Luvanda - Una Lana

Mwanadada Dorice Luvanda adondosha ngoma yake mpya kitaani alioipa jina "Una Lana"

Tuesday, October 14, 2014

Brand new

Msanii chipukizi anaekuja vema katika game la muziki wa kizazi kipya "Ras P" baada ya usimamizi wa producer Dela P wa Lost Poet Records ametambulisha single yake iitwayo "Kirusi" vocal zimefanyika Noizmekah Studios. --

Dizassta ft. Chibwa & Small J - Sindimba

Leo kitaa

Launch with Lady Jaydee

Baada ya mapumziko ya miezi 4, Lady Jaydee is BACK!!! tarehe 31 October pale MOG Bar & Restaurant (zamani NYUMBANI LOUNGE)

MIRACLE - NAELEKEA IKULU (Produced by Duke Touchez)Important mainly because it was sent directly to you.

Msanii MIRACLE toka DDC (Dom Down Click)ametambulisha Ngoma yake itwayo NAELEKEA IKULU ikiwa ni Single ya kwaza kuachiwa katika Project ya The Element ya DUKE kutoka M - LAB ikishiriki​ana na AJ Records chini ya usimamizi wa Producer DUKE TOUCH.

Lamar FT Dully Sykes TOGOLA REFIX

Brand New Single "Mselaa' - HardcroniX ft Ordinally wa Jambo Squad

Niaje niaje good people?najua nimepotea kwa mda kidogo hapa,nilikua nakimbizana tu na kuweka mambo sawa kidogo, narudi kwa kuanzia na vijana wa Kijenge juu utengwani HardcroniX likiwa ni kundi linaloundwa na Black Spear ambaye kadondoka verse ya kwanza na K Doo ambaye kafunga kwa verse ya pili,,,hapa wakiwa na Ordinally wa Jambo Squad wanakwambia "Mselaa" wakiwa wanaelezea namna msela wa kweli anatakiwa kuwa..." Huo ni ujumbe niliopokea kupitia email ya Leo kitaa toka kwa John Blass(John B) mtayarishaji wa muziki Grandmaster Records.

Brand new song toka kwa Seenga S " Sikusaidii" ipo kitaani

Msanii chipukizi Seenga S aachia ngoma yake "Sikusaidii" HipHop Category toka Noizmekah Studios

Saturday, October 11, 2014

Nocoz ft BouNako-Ka​ma Unaweza (NOIZ)

Kundi la Nocoz linaloundwa na wasanii "S Wa Maves pamoja na D Nocoz" wakiwa wamemshirikisha BouNako wameingiza ngoma mpya kitaani iitwayo "Kama Unaweza"

Tuesday, October 7, 2014

Monday, October 6, 2014

Mashaalaa Eid ilikuwa sawa like that kwa baadhi ya Watanzania waishio nchini South Africa






Baadhi ya Watanzania waishio nchini South Africa wajumuika pamoja kusherehekea sikukuu ya Eid.

Saturday, October 4, 2014

Brand new track Ras Mego - Kata (NOIZ)

Msanii Ras Mego aachia ngoma yake iitwayo "KATA" iliyotengenezwa Noizmekah Studios Arusha