Thursday, June 28, 2012

PUNDA AKIJITAFUTIA RIZKI YAKE

Punda ni mnyama mtaratibu na mwenye busara katika mfumo wake wa maisha na ni mnyama aliyejaaliwa na Mungu uwezo mkubwa wa kustahamili tabu za aina mbalimbali ni mnyama aliyebahatika kuwa mmojawapo katika mifugo ya binadamu.
Mara nyingi punda amekuwa ni msaada mkubwa katika shughuli ndogondogo za binadamu kama vile kubeba mizigo au kubeba watu katika safari za hapa na pale.
Jukumu kubwa la mfugaji wa punda ni kumpatia huduma muhimu mnyama huyo ikiwemo chakula, maji, sehemu nzuri ya kulala pamoja na matibabu.
Lakini imekuwa ni tofauti kwa baadhi ya wafugaji huenda ni kutojua umuhimu wa punda ingawaje ni mfugaji, mfano mdogo ni huyu punda unaemuona hapo akiwa yupo jalalani kwa ajili ya kujitafutia chakula huenda mmiliki wa punda huyu hajui nini maana ya kumfuga mnyama huyu na badala yake anamtumia katika kukamilisha shughuli zake tu pindi anapohitaji msaada kutoka kwa punda huyu.
Je unafikiri ni haki kumlea mnyama kama punda pasipo kumpatia mahitaji muhimu? Na kwa hali hii ya kula majalalani kweli ataepukana na maradhi ya kudhoofisha afya yake?

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments