Sunday, April 27, 2014

Afrika Kusini huru yatimiza miaka 20




Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekuwa
akiongoza sherehe za kutimiza miaka 20 ya
demokrasi na kumalizika kwa utawala wa
ubaguzi wa rangi.
Akihutubia taifa Rais Zuma alisema Afrika
Kusini inaanza kupona vidonda vya historia ya
ukatili na mgawanyiko na taratibu inajenga
umoja wa taifa.
Lakini alisema bado kuna kazi ya kukamilisha
lengo la kuondosha umaskini, tofauti za pato
na ukosefu wa ajira.
Sherehe hizo zinafanywa kabla ya uchaguzi
mkuu ambapo chama tawala cha ANC
kinakabili upinzani dhidi ya uongozi wa nchi
tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa
rangi mwaka wa 1994.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments